CCM kwachafuka,mchawi anatafutwa

CCM kwachafuka,mchawi anatafutwa

Huamini kuwa UKAWA wameongeza mitaa/vitongoji/vijiji tofauti na ilivyokuwa awali? Huamini chama chako kimepoteza mitaa/ vitongoji/vijiji vingi tofauti na uchaguzi uliopita? Ningependa kujua msimamo wako. Kama hizo hypotheses hapo juu ni sahihi nani anapaswa kuitwa mshindi kwa maana ya kupiga hatua.? Unipe majibu baada ya kupata hayo ya rasmi unayoyasubiri

UKAWA? toka lini ukawa ikawa na awali? rudi tena kafanye homework yako.
 
Ulitegemea kura zitapatikane wapi kwa mbinu kama hizi zilizopitwa na wakati.

th

Uwiiii eti anakamua maziwa. Halafu iweje?
 
Sisi tunangoja matokeo ya nchi nzima halafu tuwaone mtaingilia wapi.

Wala wasi hatuna tunawasoma viwanda vya uongo mkiwa kazini baada ya malipo ya viroba.

Ni yae yale kama Kalenga kama Chalinze kama chopa tatu kata tatu, mlikuwa mkibwabwaja

sana, matokeo rasmi yalipotoka, wote mkawa kimya. Naleo hakuna tofauti, wembe ni ule ule tu.

yae yale = yale yale
 
UKAWA? toka lini ukawa ikawa na awali? rudi tena kafanye homework yako.

Umeelewa Sema unajitoa ufahamu. Japo uchaguzi uliopita hawakuwa katika ushirikiano lakini viti walivyokuwa navyo CDM, CUF na NCCR kwa pamoja vitakuwa vimeongezeka kwa wingi baada ya kuungana kwenye uchaguzi huu. Haya nishafanya hmwork yangu....naomba unijibu maswali yangu kwenye post uliyoniquote ukipata matokeo rasmi
 
Leo hapa Lumumba hakukaliki.Hakusemeki jema. Hasira zimetanda. Nyaraka kalikali zinapita kutoka huku kwenda kule. Ofisi zetu hapa leo zinakuwa chungu.Kisa,UKAWA kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM kama Monduli. Makada owanalaumiana,vikao visivyoisha.Lakini,ni vikao kwa kukalishwa na si kukaa.Kukalishwa na kusimangwa. Kukemewa. Kushambuliwa.

Inasemwa hapa kuwa lengo la CCM halijatimia.Iitakiwa CCM ishinde kwa asilimia 90. Hadi sasa,hali ni tete.Mikoa yetu tuliyokuwa tunaitegemea imetuangusha. Majimbo yetu yaliyokuwa imara,yamesambaratika. Wabunge wetu wanaojitutumua Bungeni kama majembe ya chama, hawajasaidia kupatikana asilimia 90. Mambo ni shaghalabaghala. Mchafukoge!

Kambi za Urais na Escrow zinatajwa kama sababu kuu. Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana. Hakuna pa kushika,hakuna wa kumtupia lawama za moja kwa moja. Lakini,wakuu wanamtafuta wa kumwangushia 'jumba bovu'.Mchawi wa matokeo haya.

Kwani ni dhambi wapinzani kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kosa kubwa la CCM,kushindwa kujibu hoja na matatizo ya kiuchumi na kijamii.
Vilevile,baadhi ya wanasisa wao kuendelea kuwashutumu watendaji,badala ya kujibu hoja za msingi,jambo ambalo wananchi wanaona kama usanii.
Kinana amekuwa anatumia mbinu hii, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha(magesa Mulongo),hata Nape yupo kwenye mbinu hii ya siasa.
Tukumbuke maeneo ya mjini na ambayo yana watendaji,CCM imekuwa inapigwa.kwa sababu watendaji wanaamini kuwa hawastahili kulaumiwa kwani mapungufu mengi yanasababishwa na Sera na viongozi wa kisiasa wa chama tawala.
Mwaka 2010,Kikwete alisema hataki kura za wafanyakazi ,athari ya kauli yake CCM wanaikumbuka!
 
Haya ndio maneno yaliyobaki mdomoni mwako, pole sana tena mshukuru mbinu mliotumia ya uandikishaji wa siri na mapingamizi ya hovyo


wapi bibi yako FaizaFoxy aje akusaidie


Msalani, Majs, Ritz, Nape Mnauye, Bibi Faizafoxy, Ifeleeo, Mzee Tupatupa na wengineo wanajua fika na kuelewa kuwa CCM hii bila ya polisi, Usalama wa Taifa, Jeshi la wananchi, Wakuu wa makuwadi (MaDC na MaRC) kamwe chama chao hiki cha kiraghai cha maghirini, Chama cha Majambazi wa mali za uma Chama cha magaidi, wauaji wa wanyonge na Makuwadi wa Akina Sethi, Wauaji wa Tembo! Kamwe hawawezi kushinda katika uchaguzi wowote ule hata wakisimamishwa na mawe hawawezi kushinda! Hilo wanajua na kulitambua ndio maana daima huwatisha watumishi wa umma ambao hawako tayari kukubaliana na matakwa yao. Ndio maana daima wao kufanya ghiriba za wazi hawaoni tabu. Sura zao zimejaa unafiki na uuaji wa hali ya juu.
Natamani kuiona CCM ya wakati ule iliyokuwa na viongozi waliojali na kuuheshi utu wa kila mtu lakini sii hii.... CCM walikufa nayo waanzilishi wake.
 
Na watahaha sana kama mnara wa Babeli hakuna kuelewana ni machafuko tu kila kona, wala wasitafute mchawi maana mchawi wao ni wao wenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi UKAWA wamepata asilimia ngapi ya jumla ya mitaa/vijiji? VUTA-NKUVUTE
 
Last edited by a moderator:
Hapa ukawa wanajifariji tu na ukweli wanashindwa kuusema, ngoja takwimu zitoke uone watakavyoingia mitini.

CCM imechukuwa tena ushindi wa kishindo Tanzania nzima.

Ushindi wa mapingamizi, hila , wizi wa kura na nguvu ya dola nao ni wa kujivunia?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom