Leo hapa Lumumba hakukaliki.Hakusemeki jema. Hasira zimetanda. Nyaraka kalikali zinapita kutoka huku kwenda kule. Ofisi zetu hapa leo zinakuwa chungu.Kisa,UKAWA kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM kama Monduli. Makada wanalaumiana,vikao visivyoisha.Lakini,ni vikao kwa kukalishwa na si kukaa.Kukalishwa na kusimangwa. Kukemewa. Kushambuliwa.
Inasemwa hapa kuwa lengo la CCM halijatimia.Iitakiwa CCM ishinde kwa asilimia 90. Hadi sasa,hali ni tete.Mikoa yetu tuliyokuwa tunaitegemea imetuangusha. Majimbo yetu yaliyokuwa imara,yamesambaratika. Wabunge wetu wanaojitutumua Bungeni kama majembe ya chama, hawajasaidia kupatikana asilimia 90. Mambo ni shaghalabaghala. Mchafukoge!
Kambi za Urais na Escrow zinatajwa kama sababu kuu. Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana. Hakuna pa kushika,hakuna wa kumtupia lawama za moja kwa moja. Lakini,wakuu wanamtafuta wa kumwangushia 'jumba bovu'.Mchawi wa matokeo haya.
Kwani ni dhambi wapinzani kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
unafiki tu...
Unafiki tu...
Wewe ni sikio la kufa, ccm tumewapoteza mbaya kata zote tulizo chukua ni za ccm. Hivyo UKAWA wanaweza na wameweza, ccm chali.Unafiki tu...
Hao wamewapiga hela management yao, unajua wametafuta namna ya kupiga hela.Ziara za kinana na nape niza kuwahadaa wananchi..imagine wanapiga pocha wakiendesha mitumbwi, mara wakikifanya wana jenga wanapiga picha wakibeba tofali au wakilima au wakipanda treni yaani usanii mtupu.sasa matunda yake ndio hayoo mtabakia ma mapingamizi
Matokeo yatatolewa lini?
Huu ni mwanzo, bado tutawanyongea chini na katiba yenu ya CCM hapo April na kuwaua kabisa itapofika October
Unafiki tu...
Unapogangwa ni vema na ni busara ... kuvumilia uchungu wa sindano kwani kusema kweli .. ni dawa tu .. dawa inaingia.
Tulieni Vumilieni ... Taifa linapona.
Ulitegemea kura zitapatikane wapi kwa mbinu kama hizi zilizopitwa na wakati.Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana.
Ulitegemea kura zitapatikane wapi kwa mbinu kama hizi zilizopitwa na wakati.
![]()
Ulitegemea kura zitapatikane wapi kwa mbinu kama hizi zilizopitwa na wakati.
![]()