CCM kwachafuka,mchawi anatafutwa

CCM kwachafuka,mchawi anatafutwa

Salamu zangu kwa mkuu jk mpitishe msafishe professor muongo alionewa tutamuomba radhi ila 2015 ndiyo hakuna kulala hadi kieleweke hatutaki wali wala bia zabure
 
Huu ndio mtizamo sahihi.
CCM kabla ya uchaguzi wa mitaa na CCM baada ya uchaguzi wa mitaa .. ! Ipi imeshinda kwa kishindo. ?
Yeah! tunataka tuone CCM imeongeza vijiji/mitaa mingapi na imepokonywa vijiji/mitaa mingapi vile vile tuone upinzani kwa ujumla(UKAWA) wameongeza vijiji/mitaa mingapi wamepokonywa mingapi.

Kwa maneno megine ili ufike unakoenda unatakiwa kuangalia umepiga hatua ngapi mbele na umepiga hatua ngapi nyuma, bila kuangalia hivyo unaweza kufikiri unasonga mbele kumbe unarudi nyuma.
 
Hawana jipya hao, ukitazama nyuzi zao walizoleta humu wanazotangaza ushindi utacheka, wanashangaza kwanini hawaoneshi waliposhindwa?

Hapo sasa.

Kibibi hichooo.'' mna hara tu. Na bado.

BRING BACK OUR MONEY.
 
CCM hizi laana alianza kuzileta SAMWELI SITTA alipowatusi viongozi wa DINI...na hii laana ipo tu inafuta vivuli vyenu mpaks mtakapoanguka

Bwamdo element zako zina matatizo nani kakwambia matokeo ya metoka kushinda mtaa moja tu imekuwa kelele ccm inashinda kwa elimu yao kubwa nyinyi vilaza hamna elimu kazi yenu kupiga kelele tu
 
Kesho warioba anafanya kongamano la hatari katiba mpya
 
Kambi za Urais na Escrow zinatajwa kama sababu kuu. Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana. Hakuna pa kushika,hakuna wa kumtupia lawama za moja kwa moja. Lakini,wakuu wanamtafuta wa kumwangushia 'jumba bovu'.Mchawi wa matokeo haya.
Usanii wa hawa jamaa umewasaidia sana Watanzania kujua sura halisi ya hiki chama.
Wengi walishaamua kuwa 'zimwi likujualo....' lakini kwa usanii ule hata waliokuwa hawaelewi wamejua kuwa nia ya ccm kwa watanzania sio nzuri!
Walianza na polisi na watamaliza na polisi.

Unafiki tu...

Mwaka huu utataga, arusha tumewapiga ile mbaya sombetin mmeambulia 2 tu, na ww ndo ulikuwa kiherehere sn huyo unayemwambia ni mwanaccm mwenzako na yupo huko Lumumba, sasa ww kanunguyeye bado umelal badilika acha kutumika mwambie na huyo dem wako AMINANGOLO
 
Hali ni mbaya kwa tathmin ndogo niliyofanya watu weng wamepania kuwaondoa magamba mwakan na mnukuu kafulila anasena"kashfa ya escrow account itaivua nguo ccm" nakumbuka sana kinachokuja n massive destruction kwa ccm polen ccm mlichelewa kujipanga sasa yatatimia ya mwalimu nyerere.
 
Naona mnajipa moyo.

Unanikumbusha hadithi ya "kufungwa twafungwa lakini chenga twawala".

Angalia msije kukataa takwimu.

Mkuu kukataa takwimu za kupika hakupo, CDM na UKAWA nzima ni wastaarabu tu. Mbona ile ya mwaka 2010 ya kuchakachulia matokeo Sea View Upanga CDM walikuwa na amani tu. CDM haina vurungu bila CCM!!! Pili hata kama mkishinda si kwa tsunami ya 90% mliojitabiria bali kwa kushuka kwa kishindo. Je mlitegemea hili? Mwenzio Lizaboni amekubali kuwa sasa ushindi kwa asilimia yoyote ni ushindi tu!!! Tehe Tehe!!! Amekubali yaishe!! CDM hata kushinda kwa 40% ni ushindi wa kishindo!!! CCM kushinda kwa say 50% ni kushindwa kwa kishindo tena baada ya kuiba na kufanya mbinu chafu!!! Ungekuwa uchaguzi wa huru na haki hata asilimia 20 CCM isingepata katika uchaguzi huu.
 
Last edited by a moderator:
Huu uandishi huu unafurahisha sana sana iaseeee naam. MSALANI kajitutumua kujibu hapo, asante kwa kuokoa jahazi maana hii aibu ya mwaka hii. Kha CCM chama dume, imeshageuka CCM tezi dume mara hii??

CCM, Tezidume?

Ha! ha! ha! ha! haaaa!!!
 
Last edited by a moderator:
Lengo lako ni kumnadi Lowasa.

Halafu wewe mtu mzima unayeshinda siku nzima humu mitandaoni kuwatetea wenzako wanaotembea na maVx ya kodi za wananchi ujue karibu kitumbua kinaingia mchanga. Hakikisha kuanzia sasa ukipewa hela unazitumia vizuri wangalau kufungua mradi wa kuelewaka, bado muda mfupi hizo mayenu unazovaa na kuendesha kaIST used zitakata na wewe umri umeenda sijui kama hapo Dar utapaweza tena. Ukumbuke njia za konakona ndio hivyo zinazidi kubadilika kila kitu ni malipo kwa mtandao hakuna huyu ni mwenzetu wa ccm wala kabila langu. Kitengo cha propaganda kitakosa hela kwani mtakuwa wachache kwenye maamuzi na hela ya hazina itatoka kwa matumizi sahihi, vitega uchumi vilivyojengwa na wananchi kabla ya mfumo wa vyama vingi itabidi virudi serekalini kwa faida ya wote. Kwa hali hiyo kama huna mradi na elimu yako ya kidato cha chini ni lazima uabike, zile hela ambazo unapata na mkeo hajuai unatoa wapi zitatoweka hivyo nakushauri piga hela za mwisho mwisho na uhakikishe unafungua hata mradi wa kuku kwa kununua shamba nje ya hapo Dar ili usije kuaibika. Ni angalizo tu ndugu hutaki unaacha.
 
Leo hapa Lumumba hakukaliki.Hakusemeki jema. Hasira zimetanda. Nyaraka kalikali zinapita kutoka huku kwenda kule. Ofisi zetu hapa leo zinakuwa chungu.Kisa,UKAWA kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM kama Monduli. Makada wanalaumiana,vikao visivyoisha.Lakini,ni vikao kwa kukalishwa na si kukaa.Kukalishwa na kusimangwa. Kukemewa. Kushambuliwa.

Inasemwa hapa kuwa lengo la CCM halijatimia.Iitakiwa CCM ishinde kwa asilimia 90. Hadi sasa,hali ni tete.Mikoa yetu tuliyokuwa tunaitegemea imetuangusha. Majimbo yetu yaliyokuwa imara,yamesambaratika. Wabunge wetu wanaojitutumua Bungeni kama majembe ya chama, hawajasaidia kupatikana asilimia 90. Mambo ni shaghalabaghala. Mchafukoge!

Kambi za Urais na Escrow zinatajwa kama sababu kuu. Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana. Hakuna pa kushika,hakuna wa kumtupia lawama za moja kwa moja. Lakini,wakuu wanamtafuta wa kumwangushia 'jumba bovu'.Mchawi wa matokeo haya.

Kwani ni dhambi wapinzani kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Na hapo Mzee wangu anza kutafuta Jimbo,tupo wa kukupigia debe.Waache hao wafu wazikane.Ila waambie isingekuwa ile Mizengwe ya kutuchakachua nakututoa tusigombee kwa hiana leo yangekuwa mengine.
 
Leo hapa Lumumba hakukaliki.Hakusemeki jema. Hasira zimetanda. Nyaraka kalikali zinapita kutoka huku kwenda kule. Ofisi zetu hapa leo zinakuwa chungu.Kisa,UKAWA kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM kama Monduli. Makada wanalaumiana,vikao visivyoisha.Lakini,ni vikao kwa kukalishwa na si kukaa.Kukalishwa na kusimangwa. Kukemewa. Kushambuliwa.

Inasemwa hapa kuwa lengo la CCM halijatimia.Iitakiwa CCM ishinde kwa asilimia 90. Hadi sasa,hali ni tete.Mikoa yetu tuliyokuwa tunaitegemea imetuangusha. Majimbo yetu yaliyokuwa imara,yamesambaratika. Wabunge wetu wanaojitutumua Bungeni kama majembe ya chama, hawajasaidia kupatikana asilimia 90. Mambo ni shaghalabaghala. Mchafukoge!

Kambi za Urais na Escrow zinatajwa kama sababu kuu. Ziara za Katibu Mkuu wa chama nazo zinapondwa kwa kukosa matunda ya maana. Hakuna pa kushika,hakuna wa kumtupia lawama za moja kwa moja. Lakini,wakuu wanamtafuta wa kumwangushia 'jumba bovu'.Mchawi wa matokeo haya.

Kwani ni dhambi wapinzani kushinda vijijini na kwenye ngome za CCM?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ahahaha,u made ma day,viva ukawa,ila waambie revolution will never be televised
 
Hawana jipya hao, ukitazama nyuzi zao walizoleta humu wanazotangaza ushindi utacheka, wanashangaza kwanini hawaoneshi waliposhindwa?

Hapo sasa.

Kwanini wewe usiwekee hayo matokeo ambayo mmeshinda?...ndo maana ukapewa jina la bibi bomba wa jf koz upeo wako unaakisi uzee
 
Back
Top Bottom