CCM inahitaji pongezi nchi hii, tulipotoka tunapajua wenyewe. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni

Kabla ya 1961 palikuwa na mfumo wa Vyama vingi.

Umewahi kujiuliza vingeendelea kuwepo, na chama cha upinzani kingechukua uongozi mwaka 1970,

Tungekuwa wapi kama Nchi hivi Leo?
Angalia historia ya vyama vyote vile na ulinganishe ubora na weledi wake na chama cha TANU.Fanya hivyo kwanza afu tuendelee kujadili kaka.Karibu sana
 
Kwa wale waliozaliwa miaka ya 60 na 70 na 80 wanaelewa tunaposema japokua mapungufu yapo ila serikali ya Tanzania chini ya CCM inahitaji pongezi kwa tulipofika mpaka sasa.

Vijana wa nchi hii wanahitaji kuelimishwa zaidi katika hili maana wamekua mabingwa wa kulalamika tu. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni.
Hakuna mtu atalalamika kama wote tutakuwa tunaishi kama mawaziri. Siku zote malalamiko hutokana na kutoridhishwa na hali na jambo hilo hutokana na kukosekana usawa.

Kuna matabaka makubwa sana ya watu kwenye jamii hii hii ambayo hao wana CCM wana mchango mkubwa sana kuitengeneza. Hakuna usawa ila inapokuja swala la haki. Hiki ndio kiini cha malalamiko ya vijana.

Haiwezekani mtu anaelipwa laki 4 anyimwe allowance na benefits za utumishi ila anaelipwa million 20 ajaziwe allowances na benefits kibao pamoja na seminar na masafari. Yani mwenye uwezo wa kukabili ugumu wa maisha kwa basic salary anaongezewa mihela kibao. Ambaye hawezi anapambana na matozo.
 
Tumefika wapi eti? Hebu tuelezee maana mie sioni kwakweli.
 
TANU ilikuwapo tangu 1954 Hadi 1977.

Miaka 23 Bado haikutosha kuruhusu vyama vingi, ndo kwanza kikaanzishwa chama kimoja CCM.

Ni dhahiri CCM inapaswa ikae pembeni ijitafakari.
 
Back
Top Bottom