Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni; Nasimama na Rais Magufuli

Kizito Dickson

Senior Member
Sep 24, 2018
174
208
Ndugu zangu;

Wahenga walisema,"Mnyonge Mnyongeni ila Haki yake Mpeni"

Ni ukweli usiopingika kwa Rais Wetu Mtukufu John Pombe Magufuli sio mkamilifu na kama kiongozi wa nchi ana mapungufu kama ambavyo watu wote wanayo mapungufu yao.

Sipingani na wale ambao wanamkosoa na kumshutumu kwa yote ambayo wanaona hayako sawa hata paela ambapo wanafanya kumkomo kwani naamini unapoamua kuwa kiongozi basi hayo yote yanaweza kutokea na hio ni sehemu ya changamoto za uongozi.Kwa kuamini hilo nasimama naye nishutumiwe pamoja naye bila aibu.

Najua kwa ambao hawaelewi ni kwamba mimi binafsi naamini katika uwajibikaji kwa maslahi mapana ya nchi na katika hilo naona Magufuli anafanya vizuri sana.
Nimesoma Ripoti ya CAG na kwa jinsi ilivyo nafikiri kama wazalendo tunapaswa kuona jinsi ilivyo muhimu kwa Rais kuwa mkali kama Chuma.Pesa zetu zinaliwa waziwazi.Watendaji hawawajibiki ipasavyo,wananchi hawapati huduma zozote zile za msingi na hili linamaana kwamba watanzania wengi wanyonge bado wanadhulumiwa.

Nasimama na Magufuli kwa sababu naamini katika dhana ya uwajibikaji na kwamba kwa hali ilipofikia anapaswa kukaza zaidi.Haiwezekani tuendelea kupiga siasa wakati watu wanapiga pesa zetu.

Mimi naamini kwamba kama wanacnchi tunapaswa kusimama naye.Tusema kweli na kutoa taarifa sahihi za viongozi ambao hawawajibiki ili wawajibshwe.Tuache ushabiki na upambaji usiokuwa na maana tufanye kazi

Narudia tena nasimama Na Magufuli kwa sababu naamini katika kile anachokisimamia na niko hapa kujibu hoja kwa hoja kwa yeyote anayefikiri kwamba kuna mahali Magufuli anakosea ili tujadili kwa hoja na sio vihoja

Nawakilisha

Mungu Mbariki John Pombe Magufuli
 
Toka link akawa mtukufu? Umesahau kuweka namba za simu , awe mkali kwenye ufisadi, wizi wa pesa za serikali vipi zile tilioni 2.4 za voti namba ishirini ya ikulu ?
 
Back
Top Bottom