CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Niliipandisha hii thread, 2010, sasa tuko 2014, tukielekea 2015, jee Chadema imejipanga, inajipanga, unaendelea kujipanga?!.
Pasco
 
Hii thread kipindi kile niliichukulia ni ya kawaidaa. leo nimeisoma tena nimeiona kama ni mpya aisee!
 
Sema nini watanzania 99% hatuna uzalendo kabisa
hili pia ni Tatizo. Nyie wachambuzi kina Pasco mnaliona je hili.?
 
Sema nini watanzania 99% hatuna uzalendo kabisa
hili pia ni Tatizo. Nyie wachambuzi kina Pasco mnaliona je hili.?
Uzalendo ni pale unapoipigania nchi yako na ikibidi kuifia!.
Kitendo tuu cha kuendelea kuichagua CCM miaka nenda miaka rudi, na huu umasikini kilicholitumbukiza taifa hili, ni uzalendo tosha!.

Pasco
 
ccm imechokwa nikweli tupu ila chadema kutojipanga apo nadhani iko ivi, watanzania wamechoshwa na siasa za ulaghai na ndoo maana vilipovuma vyama vingi kama TLP,NCCR,CUF, watanzania walivisuport but at the end wakakosa direction coz watanzania wanaexpect mambo makubwa toka upinzani, more than the power wanayoipa upinzani katika kutetea haki zao.i belive chadema for now watanzania wengi wanaikubali coz ina mikakati iliyo wazi, na tumaini jipya kwa waliowengi ila je, ni wangapi waliotayari kuyapokea mabadiliko?i mean chadema ina nguvu na nguvu ni ya wananchi ila wananchi bado wanaitaji kuelimishwa na kuandaliwa katika kuyapokea mabadiliko.with new constitution i belive tutafika kuliko sahihi
 
Uchambuzi wako uko safi!!!
 
Pasco,

Naikumbuka hii thread kama jana, wengi sana tunawapigia debe CDM kubadilisha mfumo. Mimi personal niliongea na Zitto mwaka 2007 nikamwambia lazima mbadilishe mfumo, hii model mliyonayo sio ya kuongoza taifa. Mwaka 2009 tukasema tena kwamba senior management yenu haina vision wala mission ni personal goals tuu.

Leo hii yamejiri sasa, hata kama CCM ni senior Kalenga CDM walitakiwa wale lunch kwenye plate ya CCM hata kwa 44%. Swala la malumbano ya Zitto limepoteza direction ya chama na 2015 ni mwakani, sioni mapinduzi hapa.

Hii ACT iliyo anzishwa nayo ni walewale tuu njanja. Mh. Lowassa jitoe huko CCM tuanzishe chama huku mtaani. Yes, naona bora Lowassa aje sababu ana fund za kuanzisha chama, kuanzisha party need CASH sio hadithi hadithi.
 

Hatimaye hili sasa limeanza kuwezekana, haya niliyasema 2010!, leo ndio 2014, japo its almost too little too late, safari ni hatua, chelewa ufike, na better late than never!.

Hongera sana Chadema, Hongera Mhe. Mbowe, sasa huku ndio kujipanga kunaanza!.

Pasco.
 

Mkuu Chadema imejipanga ndo maana imefika hapa
 
Wanabodi,
Kwa vile CCM imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu kujipanga muwe na sura ya kitaifa, Watanzania wawaamini wawakabidhi nchi mwaka 2015.
Pasco
Naendelea kuifuatilia hii thread kwa mwaka wa nne sasa!, huku nikiupima msingi wa hoja kuu mbili za uzi huu, kwanza ni CCM imechokwa!, hivi sasa tunapoichungulia 2015, jee CCM bado imechokwa?, CCM ni dholfu bin taaban, au CCM imepunguza uchovu?. Nilisema Chadema haijajipanga, jee sasa imejipanga, inajipanga na itajipanga?!.

Pasco
 

As far as i hate to write i am going to write below, this is the reality of the situation 4 years later.

CHADEMA IMECHOKWA, CCM IMEJIPANGA, heading to 2015 General Elections.

CDM mkitaka kujua Sababu ya mambo kuwa vice versa na CCM kujipanga, nendeni Lumumba mumtafute bwana mmoja mwenye Kipara, na weledi mkubwa wa mipango mkakati.
 
Rais wetu Kikwete tumia fursa uliyonayo kukikoa chama cha mapinduzi kilicho katika mapande kuanzia bungeni hadi mitaani. Nikiwa kama kada wa CCM kukumbusha kuwa huku mitaani hali ni mbaya kiasi kwamba kampeni za uchaguzi wa mitaa zinaenda ndivyo sivyo; wapinzani na wananchi kwa ujumla wanatumia mtaji wa ESCROW kutoa kashfa dhidi ya CCM; DSM imekuwa ngumu kueneza sera za CCM kipindi tulichoko cha uchaguzi kwa vile wananchi wamekuwa hodari kutuzomea na kutuita ESCROW HAO!, WEZI! tupitapo mitaani kuelekea katika mikutano ya uchaguzi. TAFADHALI JK CHUKUA HATUA NA FUKUZA WATUHUMIWA VINGINEVYO MAJI YATAINGIA KATIKA JAHAZI!
 
Ajifukuze na yeye? Hii kitu ni ngumu kumesa yero!!
 
CCM wakimeza shida wakitema kifo duh wallahi wameshikwa pabaya na bado mapambano yanaendelea tunasubiri jan, tulipue jingine
 
hii zomeazomea ni kweli kabisa, jana nilikuwa maeneo ya rombo hotel ya shekilango, ccm walipita na magari yao ya kampeni wakazomewa kwa kuitwa wazi haoooooooo! ccm na magari yao wakatoka speed ya mwanga.
 
Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ni uthibitisho wa kuchokwa kwa CCM, jee pia ndio uthibitisho wa kujipanga kwa Chadema?!.

Pasco
 
Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ni uthibitisho wa kuchokwa kwa CCM, jee pia ndio uthibitisho wa kujipanga kwa Chadema?!.

Pasco

Huu ni mwanzo wa historia mpya lakini Chadema wanatakiwa nao wajifunze kitu kimoja hapo "wanasiasa" hawatakiwi kuwa watendaji wa serikali na hii ndio siri ya wao kuonekana wakifanya kazi nzuri sababu waliikosoa serikali mchana kweupe sababu hakuna mgongano wa kimaslahi sasa na wao kama wanamaanisha hii kazi kwa maana ya kumaanisha basi kujipanga kwao ni lazima wakubali watendaji wa kweli hawana muda sana na siasa za kivyama na wakubali kufanya kazi na watu ambao politically wako neutral ingawa objectively wako tight na committed kwenye kazi!!!!

Wako tayari kwa hilo, au watataka watendaji wakuu wa serikali wapatikane kwa mfumo wa wabunge wa viti maalumu???!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…