CCM and UDASA, this is shameful

Wangeitisha mdahalo ccm Kama taasisi akuna mwananchi mwenye uchungu na nchi hi Kama angeenda.
Ccm ni chama cha ovyo sana.
 
huelewek mzee try to write in gud sense ukiwa unatoa hisia zako
kama kweli unafuatilia au mfatiliaji mzuri wa midaharo,hasa wa leo STAR TV ni rahisi kuelewa. Kwa kifupi Lukuvi kamuomba Dr.Kitila kufanya utafiti kama UKAWA wana nia nzuri ya kuleta katiba mpya.
 
Hata wasira kuchelewa ilikuwa janja tu ... Everything was planed !! But we are brave ! We can
 
Hii sio siasa, huko ni kufanya biashara tena ya magendo!
 
Kuna yule Mzee alianza kuleta za kuleta kumtukana Warioba mbona tulimshusha jukwaani, tutapambana nao mpaka kieleweke. Mwaka huu hawana pa kutokea katiba inazidi kuitesa ccm naona raha sana maana Ukawa wanahoja nzito
 
Wacha waendelee kujimaliza kisiasa kwa uelewa wao mdogo na buku saba wanazopewa
 
Washaurini UDASA waandae mdahalo utakaokuwa balanced kama mnafikiri huu haukuwa wa kwao!
 
Hakuna lolote hayo ni maneno au maandishi yaliyoandikwa kwenye karatasi hakuna utekelezaji.

Nyie wafuasi wa Mbowe tumewachoka na kujifanya mnajua tafsiri ya kila jambo, kukicha mnawaza UKAWA jua likizama UKAWA hata kabla hamjalala badala ya kumuomba Mungu mnaomba UKAWA aagh! mnatia kichefuchefu.
 
Majuzi Sitta kaomba serikali 2 iendelee kwa miaka 5 kisha waangalie mfumo mwingine wa serikali.Yaani ccm wanaweweseka tuu
 
Hivi UDA tatu zinaweza jaza Nkuruma? Mimi mwenyewe nilikuwa pale and majority tulikuwa wanachuo tunaofahamiana - hivi Mnyaa, Kafurila, Lweitama, Makaidi, etc nao waliletwa na UDA?
 
wakati wewe unataka achangamke ili alipwe unaweza kukuta kumbe alishalipwa kitambo sana !
 
Bado mnapambana na Dr. Kitila? Kama ccm kusomba watu wao tumewazoea lakini hii ya udassa inalalamikiwa.
 
Wanajamvi, naomba niwawekee kipande nilicho comment kwenye uzi wa Yericko Nyerere ili kuweka hoja zangu sawa.
Hili jambo lina sehemu mbili, inavyoonekana watu wanaongozwa na hisia na ushabiki.

1. Kuna sehemu ya UDASA/Kitila
2. Kuna sehemu ya UKAWA/Makene

UDASA
Tuliandika kumuasa Dr Kitila Mkumbo kuwa endapo anataka mdahalo wa UDASA basi akanushe madai ya kutumika pesa kutoka kwa Rochi kama alivyosema Yericko Nyerere, Mwita Maranya na wengine.
Tulisema Kitila aelewe wanaweza kuwepo mamluki watakaotumia mdahalo huo kuingiza mambo yao.

Tulisema, kitendo cha Kitila kuita jamvi hili kiwanda cha uongo lazima aangalie kwanza mazingira yake.
Bahati mbaya Kitila akaingia kichwa kichwa na kukanusha habari hiyo kana kwamba haipo.

Leo Mabasi ya UDA yameonekana yakipeleka watu katika mdahalo wa kitaalamu.
Hakuna shaka iwe ni makusudi au bahati mbaya Dr Mkumbo amekula matapishi yake.

Sasa kuna kila sababu za kumu-implicate na scandal hii na moja kwa moja kuingiza UDASA katika fedheha kubwa.

Tumaini Makene
Hakuna sababu za kulalamika, walichokifanya UDASA na Kitila ndicho walichokusudia.
Hili ni tatizo lenu UKAWA kutokuwa na intelejensia, au kupuuzi habari na kuzembea kufanya uchunguzi.

Kulikuwa na kila kiashiria kuwa kuna jambo linatengenezwa.
Ilikuwa wajibu wenu mjiridhishe kuwa habari hizo si za kweli kabla ya kutuma watu wenu.

Kwa bahati nzuri, mashuhuda ni wanachama wenu akina Mwita Maranya, Yericko ambao mngeweza kuwatumia kupata habari zaidi juu ya hujuma dhidi yenu.

Hata pale mlipogundua kuna hujuma bado mliacha watu wenu waendelee kuogeleaa katika sewarage.
Mlikuwa na nafasi ya kuwaondoa na kuwaacha wenyewe wajadili rasimu yao.

Intelejensia yenu ilishindwa hata katika hisia. Lini Wassira ameshiriki midhalo mikubwa kama hii. Hilo tu ni ushahidi kuwa alikuwa na uhakika wa kile anachokwenda kuzunguza na katika mazingira yaliyo murua.

Intelejensia yenu ilishindwa kubaini kuwa Kitila Mkumbo hayup nanyi na wala hana jema atakalo lifanya kwa ajili yenu wala taifa hili.

Kitila ni majeruhi mkubwa wa siasa na katika kuporomoka asingependa aende shimoni mwenyewe.
Amefanikiwa kuwakama suruali kwasababu ya uzembe wenu.

Hakuna sababu za ninyi kulalamika.
Muulizeni Tundu Lissu, je hakujua mazingira aliyokwenda kuongelea jambo hilo.
Muulizeni Tundu lissu ni kwa uwezo gani anaweza kshawishi watu katika mazingira yaliyojitokeza.

Tumaini Makene , CCM wamecheza karata zao vyema.
Hakuna sababu ya kuwalaumu wao au UDASA kwasababu wametimiza mpango waliokusudia.

Mjilaumu wenyewe kwa kutokuwa makini kiintelejensia, na kiuchambuzi.

Hii ni intejensia felia yenu na wala msilalamike. Mnachopaswa kufanya ni kukaa kimya at least kwa sasa.

...spade as spade.
 
Last edited by a moderator:
Zinduka wewe zoba..
Suala ni kukodi watu si haki ya mtu! kila mtu aende kwa hiari, si kununuliwa.

1. kwani hao watu walio hudhuria wameleta fujo yoyote?
2.kwani wao sio wananchi wanaopaswa kuhudhuria kwwenye mdahalo?
3. kwani watu wengine walikatazwa kukusanya watu wao kwa lengo la kuwaongezea eliu zaidi?
 
I experienced the same kwenye Mijadala ya ITV nayo iko upande mwingine! Sijui tunapokwenda!!! Kenya wao wanatuacha!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…