Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
Kama kaka HALISI amethibitisha hapa basi nasema sasa ni muhimu kujiuliza tumefikaje huku na tutawezaje kuepuka tunapoelekea?

Naomba nithibitishiwe hapa kama MTAWA alikuwepo katika hiyo mikutano ama alitajwa na JAMBAZI MARWA ili kuhalalisha ujinga huu?

Tanzanianjema
 
Mwanakijiji,
Mkuu unazungumza na mtu anayefahamu kwa undani zaidi acha hizo habari kwani tunaelewa haya maswala yamesukwa na mnaendelea kuyasuka kama mlivyoyasuka kwa Sheikh Kassim..
Mkuu unajua Ukerewe walijenga chuo cha kiislaam kinaitwa Al Jazeera, mkuu yalisemwa mengi sana na marehemu kaka yangu became a victim within his own party...isitoshe kimekuwa chini ya uchunguzi kwa miaka karibu 6 hadi leo na kinapigwa vita vibaya sana hadi kesho maneno hayaishi kila siku kinatungwa jambo..tumezoea ndio maisha yetu topka Uhuru..

Kwa hiyo sishangai na habari kama hizi hata mkusinyiko wa Waislaam itakuwa hatari..
Mkuu nilijua haya yanakuja na hakika utabiri utatimia wala sii muda!

I doubt if you are anything near to positive mentality
 
cha ajabu ni kuwa mwanakijiji alianzisha thread kuuliza who is albert marwa

few minutes baadaye amemwaga hiii utadhani naye alikuwa na ofisi pale slamander

hakuna kitu humu na sana sana naona ni sign of desperation kutaka kuonyesha kuwa bado the so called flow of DATAZ bado ipo

ukweli ni kuwa hakuna kitu na sana sana naona hii inaweza ikawa ni SLANDER kwa sababu hakuna ushahidi

Halafu mnashangaa kwa nini standards zimekuwa LOW
Kwa hiyo yaani unabisha ingawa kuna Video na audio? sasa mnataka kitu gani ili isiwe udaku? Yaani hata majina na namba za magari zipoo. Yasingekuwepo hayoo kweli ingekuwa ya ajabu.
 
Hizi dini zitatumaliza. Wewe angalia hata watu ambao ungetegemea wapinge hoja kwa hoja..likija swala la dini wanachanganyikiwa kabisa.

Kwani fisadi si ni fisadi tuu? haijalishi kama Chenge ni muislamu au mkristo, kama RA ni muislamu au mkristo..wote wanaiba fedha ambayo ingesaidia waislamu na wakristo!

Hivi jamani mtu huwezi kutetea maslahi au hoja za waislamu bila kuingiza uislamu? au wakristo bila ukristo? Jamani lets be serious...taratibu tunaanza fanaticism ambayo haitufikishi popote. Na hizi zote ni dalili za kushindwa! Our country has failed and more so our leaders have failed us. Sasa waanaoshindwa uongozi wanaingilia sensation issues kama dini ku-advance agenda zao. Hivi mpaka leo hatujawagundua jamani?

Habari ya mwanakijiji inaweza kuwa na walakini, lakini kwanini asipingwe kwa hoja? katika hiyo makala hakuna alipoongelea UISLAMU kwa nini wale ambao hawakubaliani naye wasitoe hoja zao? Jamani JF can do better. Tunategemea kwamba kama mtu unauwezo wa kuingia JF uelewa wako ni mkubwa! Tujenge hoja tuache hysteria!

Kuna hoja nyingine unasoma unaona kabisa imejaa chuki na bigotry ingawa watu wanajimask kwa kupenda Utanzania! na make no mistake...mtu mwenye njaa can do anything! katika nchi masikini kama Tanzania..ni rahisi kutumia pesa kuadvance evil. Wote tumeyaona.

Tunaona habari ambayo hatupendi kusikia, tunaiita udaku! Lakini mjue..nchi yetu itaingia kwenye matatizo na tutaanza kusema...Ohh..we wish we knew if this could happen.....

Hizi zote ni alama za umaskini..tunashindwa kushughulikia matatizo yetu..tunaanza kufikiria kwamba solution lies somewhere else! I tell you..hata kama leo Tanzania ingeingia IOC na mashirika mengineyo.....our lives will NEVER be better. Solution to our problems lies with us not somehwere else.
 
Hii ni nchi yetu sote, si ya Mwanakijiji (at least yuko kijijini) si ya Masatu, si ya Mkandara wala si ya Mbowe na Halisi. Kinachotokea, udini, ukabila na mengineyo ni sumu mbaya sana ambayo tiba yake ni ngumu mno kuipata kwa urahisi na mifano iko Rwanda, Burundi, Kenya na kwingineko.

Watu wenye akili wamesema, "nchi imeingia pabaya" na kwa kweli musidhani ukabila utamtafuna Mbowe na Mengi pekee, utaingia kote. Jamani kuna hatari kubwa hapa na tusipoangalia NCHI ITAINGIA PABAYA.

UWT wameona na wanasema, "TUSHIRIKIANE SOTE, NCHI NI YETU SOTE"... tuwe na tofauti zetu za kila aina, tutafute fedha kwa njia zote hata wale wachafu watakamatwa na wengine kusamehewa kama wa EPA lakini tusithubutu kutafuta fedha kwa kupandikiza chuki za udini na ukabila.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU TUBARIKI WATOTO WA TANZANIA
 
Inawezekkana huo mpango uliokuwa unapangwa ni tofauti kabisa kwa maana
walikua wanatumia lugha ya kinteligensia so ikawa interpreted hivyo. Kwa haraka haraka
jinsi mpangilio wa vikao vyao ulivyokuwa unaendeshwa ni watu atleast wanao ujuzi walao
mdogo wa kupangilia mambo kukwepa kuwa suspected.

Nimekuwa confused kidogo. Mpango wowote unaopamgwa visivyo halali na ambao hautaki ujulikane ni ujasusi! Wewe unafikiri watu ambao hawataki wawe suspected wana nia nzuri?
Cheers Mzee Mwanakijiji bring more news.
 
Majina karibu yote aliyoyataja mwanakijiji ni ya wahubiri wa dini linganishi. Mikutano na magari wanayotumia sio siri.

Mwanakijiji anamtumiwa tangu enzi za sakata la Ukabila BoT, TRA nk. Tunafahamu waliomlipa kwa kazi ile na kiwango alichopewa. Sasa anataka kila suala linalowagusa wachaga kulifanya dili!

Mengine ni uzushi, uchochezi na propaganda!
 
Kwa hiyo yaani unabisha ingawa kuna Video na audio? sasa mnataka kitu gani ili isiwe udaku? Yaani hata majina na namba za magari zipoo. Yasingekuwepo hayoo kweli ingekuwa ya ajabu.

hakuna kitu

kama video ingekuwepo tungeiona

hii dunia ya YOUTUBE its just a matter of kurekodi kisha kuiveka hewani

ushajiuliza mbona hakuna aliyeiweka online?

kwa sababu watu wana mambo muhimu zaidi kuliko udaku
 
Majina karibu yote aliyoyataja mwanakijiji ni ya wahubiri wa dini linganishi. Mikutano na magari wanayotumia sio siri.

Mwanakijiji anamtumiwa tangu enzi za sakata la Ukabila BoT, TRA nk. Tunafahamu waliomlipa kwa kazi ile na kiwango alichopewa. Sasa anataka kila suala linalowagusa wachaga kulifanya dili!

Mengine ni uzushi, uchochezi na propaganda!

Hii habari haikuletwa na Mzee Mwanakijiji, imeletwa na Mkuu Sekenke...Mzee Mwanakijiji amekuja baadaye kuongeza kile anachokijua. Someni kwa makini thread kuanzia mwanzo bila nia ya ubishi mtaona na kuelewa.

HABARI HII IMEONYESHWA ITV, WATANZANIA ZAIDI YA MMOJA WAMEONA HEBU PIGENI SIMU KWA NDUGU ZENU TANZANIA MUWAULIZE.

hakuna kitu

kama video ingekuwepo tungeiona

hii dunia ya YOUTUBE its just a matter of kurekodi kisha kuiveka hewani

ushajiuliza mbona hakuna aliyeiweka online?

kwa sababu watu wana mambo muhimu zaidi kuliko udaku

Game Theory

Mbona unashangaza ulimwengu mkuu...yaani kama video haipo Youtube basi ni kwamba habari haina ukweli.....!!!!!!!!!!

Kama hii ndio janja yako ya kutaka watu waweke video kwenye youtube omba kwa nidhamu badala ya kutumia mbinu zilizofilisika kama hizi za kubisha ili mradi kubisha.
 
Na Mwandishi Maalum

KLHN yaweza kuripoti kwa uhakika kabisa kuwa mpango wa kuanzisha uchafuzi wenye mlengo wa kidini na kikabila nchi umeundwa na sasa umefichuliwa. Mpango huo ambao unawahusisha watu mbalimbali wenye majina makubwa umedhihirika kuanzia siku ya Ijumaa iliyopita.

Mpango huo ulianza kusukwa wiki chache zilizopita na hatimaye kuanza kutekelezwa siku ya Ijumaa iliyopita. Kwa wanaokumbuka siku ile (ya Ijumaa) kulikuwa na mkutano wa Waislamu kuelezea masuala mbalimbali ya maslahi yao na hasa suala la OIC. Baadhi ya viongozi wa Waislamu toka mikoani walikuwa jijini pia.

Ilikuwa ni katika nafasi hii timu iliyokuwa imeanza kukusanywa iliweza kuwakutanisha viongozi mbalimbali hao wa Waislamu kwa kuandaa mkakati kamambe ambao kwa madai yao mipango yake inatoka ndani na juu kwenye serikali. Katika kufanya hivyo viongozi kama 9 hivi wa Kiislamu waliweza kupatikana na kukutanishwa katika hoteli ya Regency siku ya Ijumaa.

Miongoni mwao ni mashehe na viongozi wengine wa kidini; baadhi yao ni pamoja na Shekhe Mazinge, Mwaipopo, Said Liko, Chifu Msokwa, Ustaadh Twaha, Dr. Salehe, Abubakar Bonde, Sheikh Amour Jongo, Rajabu Jazba, na Ustaadh Ramadhani. Waliokuwemo kwenye mkutano huo pia ni pamoja na Albert Marwa (inadaiwa ni mtoto wa kulelewa wa Generali Marwa) pamoja na mtu mmoja aitwaye Mtawa (huyu yasemekana ni mtumishi wa ngazi ya Juu ikulu). Walikuwepo baadhi ya watu wengine ambao wanadaiwa kuwa ni maafisa wa Usalama wa Taifa ambao kutokana na sheria hatuwezi kuwataja majina yao.

Mpango huo ambao “vijidudu” vya uchunguzi viliweza kuunasa kwa picha na kwa sauti kimsingi una malengo yafuatayo.

a. Kuwaonesha waislamu kuwa Bw. Reginald Mengi na Freeman Mbowe ndio maadui wakubwa wa maslahi ya Waislamu nchini.
b. Kwamba Mengi na Mbowe wana mkakati wa kuhakikisha kiongozi anayekuja ni kutoka kabila la Wachagga. Katika hili la dhidi ya “Uchagga” wanamkakati walikuwa wana uhakika wa kutobughudhiwa na polisi kwenye mikutano ambayo waliipanga kuifanya hasa wakiamini kuwa IGP Said Mwema yuko upande wao. Hata hivyo mmoja wao aliapa kuwa aliwahi kuambiwa na Dr. Nchimbi kuwa Mwema ni Mchagga (sijui kwa upande wa mama) na hivyo wasitarajie sana.
c. Walioleta mpango huo wamemhusisha kiongozi wa juu serikalini kuwa ndiye aliyewatuma kutekeleza mpango huo hasa kuonesha kuwa vyombo vya IPP vinatumika kueneza Ukristu, kukandamiza Waislamu, na kuinua Wachagga. Hili litaelezwa ili Waislamu waanze kuvisusisa vyombo vya habari vya IPP.
d. Kuendelea kuwahusisha Mengi na Mbowe katika vifo vya Chacha Wangwe na Gavana Ballali.

Katika kutekeleza mpango huo timu hiyo ilikuwa ijipange na kuandaa bajeti ya kiasi kisichopungua shilingi milioni 100 ambazo zitagawanywa kati yao na kwa wale ambao watakuwa tayari kutekeleza mpango huo. Kiasi ambacho cha awali ambacho kila mmoja alikuwa agawiwe ni kama milioni tatu tatu huko mmoja wa wanamkakati huo akiahidi uwezekano wa kupata fedha zaidi kutoka kwa Bakhresa. Kiasi cha awali kinadaiwa kutolewa na mfanyabiashara Yusuph Manji wa Quality Group.

Siku ya Jumamosi kundi hilo la wanamkakati lilikutana kwenye hoteli ya Golden Tulip kuendelea na mipango yao ambayo ka nzi ka KLHN kalikuwa kanafuatilia kila hatua tena kwa ukaribu kabisa.

Wakiwa na magari yenye namba za usajili za T267 ABT na T87 ABG wanamkakati wakiongozwa na Mazinge Mwipopo (spelling yaweza isiwe sahihi) na Chifu Msokwa walihamisha kikao chao kingine kutoka Golden Tulip kuelekea Msikiti wa Mtambani ambapo waliamua kubadilisha na kuelekea Msikiti wa kwa Mtoro. Ka nzi kaliweza kunasa habari za kutosha.

Siku ya Jumapili kikao chao kiliendelea huko Kinondoni mtaa wa Kazina nyumba (censored) ambapo kuanzia saa tisa hadi majira ya Magharibi waliendelea na mipango yao na maazimio yao ikiwemo la kuhakikisha kuwa viongozi watakaoshiriki katika mkakati huo wa kuitisha mikutano mbalimbali mikoani wahakikishe na wao wanapata watu angalau 20 chini yao.

Kutoka kwenye vikao hivyo iliazimiwa uitishwe mkutano wa waandishi wa habari ili kuweza kufafanua madai yao dhidi ya Mengi na Mbowe na hivyo kuanzisha mchakato huo wa kueneza propaganda hii ya udini na ukabila. Baadhi ya wajumbe walikuwa wameshaondoka siku ya Jumatatu kuelekea mikoani kuanza kazi hiyo na hilo ndilo lililosababisha vyombo vya ITV kurusha hivyo walivyonavyo.

KLHN imepata nafasi ya kusikiliza masaa ya kutosha ya mazungumzo ya kundi hili na jambo moja ambalo tunaweza kusema kwa uhakika ni kuwa linatia hofu na kuuliza tumefikaje hapa.

Hata hivyo mpango huo haujaenda vizuri kama ulivyotarajiwa hasa baada ya kutokea mabishano ya kiasi cha fedha huko baadhi ya wajumbe wakiamini kuwa Bw. Albert Marwa amepewa fedha zaidi kuliko alizowapatia wajumbe hao. Wengine wameanza kudai kuwa Bw. Marwa ndiye aliyeinjinia mpango wa wao kunaswa na vyombo vya kielectroniki.

Jioni ya leo (jumanne) ka nzi ketu kanaruka ruka mikoani kamethibitisha pasipo shaka kuwa baadhi ya simu za wahusika wakuu zimekuwa ‘tapped’ ili kuweza kujua jinsi operesheni hii ilivyoendesha kikamilifu ikihusisha utaalamu na ujasiri wa hali ya juu kuliko uwezo wowote wa TISS kuwanyemelea mafisadi.

Msimamizi wa Operesheni hii ardhini ambaye alizungumza na KLHN kwa masharti yale yale mliyoyazoea amesema kuwa hawakuwa na mpango wa kuhusisha vyombo vya usalama kwani kwenye suala zima vyombo hivyo baadhi ya wahusika wake wa kuu wamo ndani mpango huu na hivyo njia pekee ilikuwa ni kuwadokeza tu watu kuwa mpango huo upo, unajulikana, na utakapoanza kutekelezwa Watanzania “wasishtuke”.

Hata hivyo wameahidi kuwa endapo Mwendesha Mashtaka Mkuu ataamua kuunda "Special Tribunal" ya kufuatilia suala hili ili kuona mashtaka yoyote kuletwa au uchunguzi ushirikiano unaweza kutolewa kwa kadiri ya kwamba vyanzo vyote vya habari hii vitabakia kuwa siri na havitalazimishwa kujitaja isipokuwa kuleta ushahidi kama ulivyo (raw evidence). Nje ya hapo amesema kuwa hawana "imani na Polisi wala Usalama wa taifa kwenye suala hili".

KLHN inaendelea kufuatilia kwa karibu mpango huu na kufichua njama yoyote ile ya kifadi yenye lengo la kuleta mgongano wa kidini au kikabila nchini. Baadhi ya habari zitasahihishwa kwa kadiri wingu linavyozidi kusafishika zaidi.

duh!I CANT BELIVE THIS!!!!!!!!!KWELI NCHI YA MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE IMEFIKA HAPA???
 
Hakuna chochote ni habari za kutengeneza na umafia tu unaofanywa na genge fulani kwa malengo wanayoyajua wenyewe!
 
hakuna kitu

kama video ingekuwepo tungeiona

hii dunia ya YOUTUBE its just a matter of kurekodi kisha kuiveka hewani

ushajiuliza mbona hakuna aliyeiweka online?

kwa sababu watu wana mambo muhimu zaidi kuliko udaku

Duh! hapo ndio huwa ninapochoka saa nyingine! Wengi tumeiona hii taarifa kupitia ITV,sasa kama kuna waliorekodi ili kuweka Youtube hio tena ni issue nyingine,maana huku bongo brother,habari kama hio ni ya kushtukiza tu,sio kwamba labda utakuwa na PVR ili urekodi..inabidi usubiri wakiitoa tena wenyewe.Sasa pia kwa wewe kutokuiamini hii habari kwa sababu haiko kwenye Youtube pia ni kichekesho
 
Sijui ni kwanini hata watu wakisikia milio ya risasi huwa wanakimbilia kwenye mlio badala ya kuangalia usalama wao.

Sijui ni kwanini ni wavivu wa kufikiri hivi
 
Mkuu, Kwa nini wewe unafikiria hivyo?

Unakumbuka mtiririko wa habari ya kifo cha Balali? Lilianzisha genge fulani kwa ushirikiano wakitumia gazeti fulani na mtandao, at last hakuna aliyeuona mwili wa 'marehemu'. Makundi hayo yapo na yanafanya kazi. Wengine ni wana JF. Subiri!
 
Duh! hapo ndio huwa ninapochoka saa nyingine! Wengi tumeiona hii taarifa kupitia ITV,sasa kama kuna waliorekodi ili kuweka Youtube hio tena ni issue nyingine,maana huku bongo brother,habari kama hio ni ya kushtukiza tu,sio kwamba labda utakuwa na PVR ili urekodi..inabidi usubiri wakiitoa tena wenyewe.Sasa pia kwa wewe kutokuiamini hii habari kwa sababu haiko kwenye Youtube pia ni kichekesho[/quote]

Imani ya kidini hupofusha kiasi cha kumuaminisha profesa 1 + 3 = 0
 
Jamani huu udaku typical Mengi style mara nataka kuuliwa na Shabbir Dewji mara Manji sasa mchaga hatakiwi kugombea urais halafu waislam wanatumwa Songea! sijui wapo waislam wangapi Songea.

Only JF
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom