Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Caught on Tape: Mkakati wa Mamluki wafichuliwa!

Status
Not open for further replies.
😕😕😕🙁🙂😱😀😉

chinks

ndio katika ya hao wanafiki mnaopanga mambo halafu mkaa kuangalia upepo unaelekea wapi, mpo humu humu mnajidai kati yao wapinga ufisadi. Na bado.....
 
Nahofia usalama wa nchi yangu...hii habari imenifanya "very uncomfortable" hasa kuhusishwa kwa Albert Marwa.
 
Nahofia usalama wa nchi yangu...hii habari imenifanya "very uncomfortable" hasa kuhusishwa kwa Albert Marwa.

tunasema kikulacho kinguoni mwako. Uanamtandao name de plume unafiki si mnao hata huko ughaibuni, sasa haya ndio madhara yake. Mtajiju....
 
Wakuu mnaweza kufirikia "aloud" na kusema huenda lisemwalo lipo...ukiona kuwa miaka ya 1990 kulikuwa na "tetesi" kuwa Albert alikuwa anafanya biashara ya silaha nchi za jirani na hii taarifa ya leo yenye "uhakika" kuwa kuna mkono wake kwenye mikakati ya kuleta furugu za kidini na kikabila Tanzania. Natumai mmenipata...just trying to think aloud...!!

Analysis nzuri sana Mkuu.Nami nimewahi kusikia kuwa Albert alikuwa akijihusisha na biashara ya sialaha kupitia kwa connections alizopewa na baba yake wa kufikia.Niliposoma habari hii mara ya kwanza nilijiuliza WHY ALBERT MARWA?Nafahamu kuwa mtu aliye tayari kubadili dini kuoa mwanamke ili awe karibu na kiongozi flani anaweza kujihusisha na lolote lile.Lakini sikudhani kuwa hiyo ni sababu pekee ya Albert kujihusisha na kundi hili.Inawezekana kabisa kwamba role yake katika kundi hilo ni upatikanaji wa nyenzo pindi zitapohitajika....pengine nami na-think aloud too lakini inaweza kuwa na substance
 
MkJJ tunashukuru kwa habari,

Inawezekkana huo mpango uliokuwa unapangwa ni tofauti kabisa kwa maana
walikua wanatumia lugha ya kinteligensia so ikawa interpreted hivyo. Kwa haraka haraka
jinsi mpangilio wa vikao vyao ulivyokuwa unaendeshwa ni watu atleast wanao ujuzi walao
mdogo wa kupangilia mambo kukwepa kuwa suspected.

Je sauti zimechunguzwa vya kutosha kujua kweli huo mpango ni kama ulivyo na sio coding ilitumika????

Je hao watu wa Ikulu waliingia kuratibu hiyo kazi ama waliingia kwa nyazifa zao?????? ama kujua kuhusu hiyo njama na kureport???????

Maana aliyerecord sauti lazima ni insider wa hiyo terror group, Je

kundi la hawa jamaa hawakuwa na tahadhari ya kuwafanya washuku lolote..
 
Nahofia usalama wa nchi yangu...hii habari imenifanya "very uncomfortable" hasa kuhusishwa kwa Albert Marwa.

Everything is under control, ndio maana hawa wameshikwa binafsi nimeamua kuingia huko ku-deal na hii ishu kichwa kichwa, nitarudi tena hapa siku ya mkutano wa NEC mwisho wa wiki, maana hili ni taifa letu ni lazima tulilinde sisi wenyewe wananchi wake.

Heshima mbele kwa wakuu wote JF, haya mambo mengine ni muhmu mno kuwaachia wengine, ni lazima tuingie wenyewe huko mpaka kieleweke, muwe na mijadala iliyo na amani, lakini wengine ni lazima tuingie huko kulinda taifa letu, maana hapa kuna wananchi wenzetu ambao wamekamatwa pabaya hapa..

Respect and Out!
 
Duh!

sasa huyo TAOE iko wapi? maana nimetazama kule YOU TUBE hakuna kitu au ndio kama kawaida yetu tunajadili HEWA TUPU?

BTW

Bonafsi namjua ana albert na ni mtu wangu lakini ukweli ni kuwa mindhali kuna mtu alitaka sana kujua habari za albert nashangaa kaja ziulizia humu wakati watu wa albert wanajulika na its an OPEN SECRET

sasa basi, info ulizoziweka hapo Yebo yebo nyingi ni Uzuushi lakini kwa sababu thread haimzungumzii albert binafsi basi ntakaa pembeni

ila as far as i can see ni kuwa mtashangaa jinsi gani hii thread itakavyokuwa na CONFLICT OF INTEREST na wahusika wetu watatu humu ambao so far najua hawajaguswa lakini wakiguswa watarudi na nguvu zote au lakini sijui ni kwa style gani

lakini kwanza leteni hiyo so called TAPE kisha tutamove on from there...in the meantime narudi kwenye LERKER MODE
 
Nahofia usalama wa nchi yangu...hii habari imenifanya "very uncomfortable" hasa kuhusishwa kwa Albert Marwa.

acha uzushi

2ue3cpx.gif
 
mawili matatu ya kuongeza kuhusu wasifu wa kijana Albert Marwa

... kati ya mwaka 1997 - 1998 aliponunua nyumba 2 (za serikali) Oysterbay

... (alinunua nyumba za serikali Oysterbay kabla hata ya kifo cha JKN..!!).

Zilikuwa zimeshaanza kuuzwa ?

Walikuwa wanauza mbili mbili ?

Alikuwa anaishi humo kabla ya kuuziwa ?

Kama mtumishi wa Serikali ?
 
Zilikuwa zimeshaanza kuuzwa ?

Walikuwa wanauza mbili mbili ?

Alikuwa anaishi humo kabla ya kuuziwa ?

Kama mtumishi wa Serikali ?

Kuhani

Yes, zilishaanza kuuzwa. Binafsi ndio mara ya kwanza nilisikia nyumba zimeuzwa Oysterbay. Nimesema Albert yuko "connected" ni kwa sababu hana makeke kama wakina Kinje ndio maana Watanzania wengi hawajamsikia/ kumfahamu. Hakuwa anaishi kwenye hizo nyumba na wala sijawahi kumfahamu Albert kama muajiriwa popote pale Serikalini au Uraiani ila alizinunua na mpaka leo anazimiliki. Hii sio siri na wala siwezi kuita ni data..!!
 
Yebo Yebo,

Kuna Mawaziri, Majaji, Mabalozi wamenyang'anywa nyumba baada ya kuuziwa ovyo ovyo, Bakari Mwapachu, Jaji Stephen Ihema, Balozi Adam Marwa (nyumba za Serikali za Mitaa), Balozi Ben Moses (za Serikali Kuu lakini kajinunulisha zaidi ya moja na mkewe).

Sasa huyu mtu ambae hata hakuwa mtumishi, achilia mbali Waziri, watu si wangeshamfanyia unoko kama hata Waziri ananyang'anywa ?

Na pia, nyumba zilianza kuuzwa 2001. Huyu aliuziwaje in the nineties, tena mbili, na hata sio mtumishi?

Umeongelea connection, lakini hata hawa Mawaziri na Mabalozi wamenyang'anywa, Mkuu. Huyu character ana clout kuliko Head of Ethics Secretariat, Ofisi ya Rais, Jaji Ihema, ex-Minister Mwapachu na Mabalozi ?
 
Kuhani unajaribu kutafuta "sense" where there is "senseless". Unajaribu kureason kwa kuangalia what should have been or what ought to be. Bahati mbaya (kama bahati has anything to do with it) kuna mambo yanafanyika nchini mwetu that are beyond the realm of sense and sensibility!
 
Mwankijiji,
Na Mwandishi Maalum

KLHN yaweza kuripoti kwa uhakika kabisa kuwa mpango wa kuanzisha uchafuzi wenye mlengo wa kidini na kikabila nchi umeundwa na sasa umefichuliwa. Mpango huo ambao unawahusisha watu mbalimbali wenye majina makubwa umedhihirika kuanzia siku ya Ijumaa iliyopita.

Mpango huo ulianza kusukwa wiki chache zilizopita na hatimaye kuanza kutekelezwa siku ya Ijumaa iliyopita. Kwa wanaokumbuka siku ile (ya Ijumaa) kulikuwa na mkutano wa Waislamu kuelezea masuala mbalimbali ya maslahi yao na hasa suala la OIC. Baadhi ya viongozi wa Waislamu toka mikoani walikuwa jijini pia.

Ilikuwa ni katika nafasi hii timu iliyokuwa imeanza kukusanywa iliweza kuwakutanisha viongozi mbalimbali hao wa Waislamu kwa kuandaa mkakati kamambe ambao kwa madai yao mipango yake inatoka ndani na juu kwenye serikali. Katika kufanya hivyo viongozi kama 9 hivi wa Kiislamu waliweza kupatikana na kukutanishwa katika hoteli ya Regency siku ya Ijumaa.

Miongoni mwao ni mashehe na viongozi wengine wa kidini; baadhi yao ni pamoja na Shekhe Mazinge, Mwaipopo, Said Liko, Chifu Msokwa, Ustaadh Twaha, Dr. Salehe, Abubakar Bonde, Sheikh Amour Jongo, Rajabu Jazba, na Ustaadh Ramadhani. Waliokuwemo kwenye mkutano huo pia ni pamoja na Albert Marwa (inadaiwa ni mtoto wa kulelewa wa Generali Marwa) pamoja na mtu mmoja aitwaye Mtawa (huyu yasemekana ni mtumishi wa ngazi ya Juu ikulu). Walikuwepo baadhi ya watu wengine ambao wanadaiwa kuwa ni maafisa wa Usalama wa Taifa ambao kutokana na sheria hatuwezi kuwataja majina yao.

Mpango huo ambao "vijidudu" vya uchunguzi viliweza kuunasa kwa picha na kwa sauti kimsingi una malengo yafuatayo.

a. Kuwaonesha waislamu kuwa Bw. Reginald Mengi na Freeman Mbowe ndio maadui wakubwa wa maslahi ya Waislamu nchini.
b. Kwamba Mengi na Mbowe wana mkakati wa kuhakikisha kiongozi anayekuja ni kutoka kabila la Wachagga. Katika hili la dhidi ya "Uchagga" wanamkakati walikuwa wana uhakika wa kutobughudhiwa na polisi kwenye mikutano ambayo waliipanga kuifanya hasa wakiamini kuwa IGP Said Mwema yuko upande wao. Hata hivyo mmoja wao aliapa kuwa aliwahi kuambiwa na Dr. Nchimbi kuwa Mwema ni Mchagga (sijui kwa upande wa mama) na hivyo wasitarajie sana.
c. Walioleta mpango huo wamemhusisha kiongozi wa juu serikalini kuwa ndiye aliyewatuma kutekeleza mpango huo hasa kuonesha kuwa vyombo vya IPP vinatumika kueneza Ukristu, kukandamiza Waislamu, na kuinua Wachagga. Hili litaelezwa ili Waislamu waanze kuvisusisa vyombo vya habari vya IPP.
d. Kuendelea kuwahusisha Mengi na Mbowe katika vifo vya Chacha Wangwe na Gavana Ballali.

Katika kutekeleza mpango huo timu hiyo ilikuwa ijipange na kuandaa bajeti ya kiasi kisichopungua shilingi milioni 100 ambazo zitagawanywa kati yao na kwa wale ambao watakuwa tayari kutekeleza mpango huo. Kiasi ambacho cha awali ambacho kila mmoja alikuwa agawiwe ni kama milioni tatu tatu huko mmoja wa wanamkakati huo akiahidi uwezekano wa kupata fedha zaidi kutoka kwa Bakhresa. Kiasi cha awali kinadaiwa kutolewa na mfanyabiashara Yusuph Manji wa Quality Group.

Siku ya Jumamosi kundi hilo la wanamkakati lilikutana kwenye hoteli ya Golden Tulip kuendelea na mipango yao ambayo ka nzi ka KLHN kalikuwa kanafuatilia kila hatua tena kwa ukaribu kabisa.

Wakiwa na magari yenye namba za usajili za T267 ABT na T87 ABG wanamkakati wakiongozwa na Mazinge Mwipopo (spelling yaweza isiwe sahihi) na Chifu Msokwa walihamisha kikao chao kingine kutoka Golden Tulip kuelekea Msikiti wa Mtambani ambapo waliamua kubadilisha na kuelekea Msikiti wa kwa Mtoro. Ka nzi kaliweza kunasa habari za kutosha.

Siku ya Jumapili kikao chao kiliendelea huko Kinondoni mtaa wa Kazina nyumba (censored) ambapo kuanzia saa tisa hadi majira ya Magharibi waliendelea na mipango yao na maazimio yao ikiwemo la kuhakikisha kuwa viongozi watakaoshiriki katika mkakati huo wa kuitisha mikutano mbalimbali mikoani wahakikishe na wao wanapata watu angalau 20 chini yao.

Kutoka kwenye vikao hivyo iliazimiwa uitishwe mkutano wa waandishi wa habari ili kuweza kufafanua madai yao dhidi ya Mengi na Mbowe na hivyo kuanzisha mchakato huo wa kueneza propaganda hii ya udini na ukabila. Baadhi ya wajumbe walikuwa wameshaondoka siku ya Jumatatu kuelekea mikoani kuanza kazi hiyo na hilo ndilo lililosababisha vyombo vya ITV kurusha hivyo walivyonavyo.

KLHN imepata nafasi ya kusikiliza masaa ya kutosha ya mazungumzo ya kundi hili na jambo moja ambalo tunaweza kusema kwa uhakika ni kuwa linatia hofu na kuuliza tumefikaje hapa.

Hata hivyo mpango huo haujaenda vizuri kama ulivyotarajiwa hasa baada ya kutokea mabishano ya kiasi cha fedha huko baadhi ya wajumbe wakiamini kuwa Bw. Albert Marwa amepewa fedha zaidi kuliko alizowapatia wajumbe hao. Wengine wameanza kudai kuwa Bw. Marwa ndiye aliyeinjinia mpango wa wao kunaswa na vyombo vya kielectroniki.

Jioni ya leo (jumanne) ka nzi ketu kanaruka ruka mikoani kamethibitisha pasipo shaka kuwa baadhi ya simu za wahusika wakuu zimekuwa ‘tapped' ili kuweza kujua jinsi operesheni hii ilivyoendesha kikamilifu ikihusisha utaalamu na ujasiri wa hali ya juu kuliko uwezo wowote wa TISS kuwanyemelea mafisadi.

Msimamizi wa Operesheni hii ardhini ambaye alizungumza na KLHN kwa masharti yale yale mliyoyazoea amesema kuwa hawakuwa na mpango wa kuhusisha vyombo vya usalama kwani kwenye suala zima vyombo hivyo baadhi ya wahusika wake wa kuu wamo ndani mpango huu na hivyo njia pekee ilikuwa ni kuwadokeza tu watu kuwa mpango huo upo, unajulikana, na utakapoanza kutekelezwa Watanzania "wasishtuke".

Hata hivyo wameahidi kuwa endapo Mwendesha Mashtaka Mkuu ataamua kuunda "Special Tribunal" ya kufuatilia suala hili ili kuona mashtaka yoyote kuletwa au uchunguzi ushirikiano unaweza kutolewa kwa kadiri ya kwamba vyanzo vyote vya habari hii vitabakia kuwa siri na havitalazimishwa kujitaja isipokuwa kuleta ushahidi kama ulivyo (raw evidence). Nje ya hapo amesema kuwa hawana "imani na Polisi wala Usalama wa taifa kwenye suala hili".

KLHN inaendelea kufuatilia kwa karibu mpango huu na kufichua njama yoyote ile ya kifadi yenye lengo la kuleta mgongano wa kidini au kikabila nchini. Baadhi ya habari zitasahihishwa kwa kadiri wingu linavyozidi kusafishika zaidi.

Mkuu utanisamehe lakini habari yako ni artt ya kipekee, yaani sinema nzito ya James Bond! haina ukweli zaidi ya mtu fulani anataka kupandikiza chuki...
Habari nilizozipata mimi kulikuwepo na mkutano wa masheikh ktk maswala ya Bakwata kama wanavyofanya miaka yote.. iweje leo waonekane watu Hotelini wakizungumza habari iwe OIC wakati ni kawaida yetu sisi Wadanganyika kuzungumzia WATU kama kikolezi cha maengezi..
Mbowe na Mengi wanahusika vipi na OIC, ikiwa kweli IPP wanahusika kwa njia fulani na ukandamizaji wa Uislaam wasizungumziwe? mbona makanisani mnazungumzia maswala ya OIC na hakuna mwandishi wa habari anaye wafuata Mapadre majumbani mwao..Sisi wenyewe tumewahi kukutana kuzungumzia Mustakabali wa nchi yetu ilikuwa na maana tulikuwa na mpango gani?.. acheni uchinvi!
jamani nyie msianze haya tena... nilisema maswala haya yatatupeleka kubaya sana na hasa pale mnapokuwa mkitumia nafasi zenu za Uandishi kupandikiza mbegu mbaya..Mbowe na Chadema wana Uhusiano mzuri sana na CUF chama ambacho mimi ningeweza kusema kingekuwa cha kwanza kuondoa mahusiano yake na Mbowe kwa sababu Ansar Sunni wamejaa telee!
Acheni udini wenu jamani acheni asionekane mtu kavaa kanzu Hotel kubwa basi kuna jambo... yale yale ya - A nigger kaonekana kwenye neighborhood!
 
Mkandara, don't doubt me on this one brother.. some details are still sketchy but the substance I'll defend with my life.
 
Yebo Yebo,

Kuna Mawaziri, Majaji, Mabalozi wamenyang'anywa nyumba baada ya kuuziwa ovyo ovyo, Bakari Mwapachu, Jaji Stephen Ihema, Balozi Adam Marwa (nyumba za Serikali za Mitaa), Balozi Ben Moses (za Serikali Kuu lakini kajinunulisha zaidi ya moja na mkewe).

Sasa huyu mtu ambae hata hakuwa mtumishi, achilia mbali Waziri, watu si wangeshamfanyia unoko kama hata Waziri ananyang'anywa ?

Na pia, nyumba zilianza kuuzwa 2001. Huyu aliuziwaje in the nineties, tena mbili, na hata sio mtumishi?

Umeongelea connection, lakini hata hawa Mawaziri na Mabalozi wamenyang'anywa, Mkuu. Huyu character ana clout kuliko Head of Ethics Secretariat, Ofisi ya Rais, Jaji Ihema, ex-Minister Mwapachu na Mabalozi ?

Kuhani

Hao wote uliowataja zaidi ya "vyeo vyao vya sasa au zamani" siwezi kusema connections zao zina nguvu kiasi gani kwa sababu sijui walichonacho nilichokiona. Albert kwa upande mwingine nimeona alichofanya na alivyojikusanyia kwa kutumia "connections" na uwezo alionao wa kujituma (legal or illigal) kupata anachotaka.

Sidhani kama kuna mtu ninayemjua na ninayejua anamfahamu Albert ambaye hajui kama ana hizo nyumba Oysterbay. Magazeti yameanza kuandika kuandika 2001, wakati huo Albert alishamaliza ukarabati wa nyumba zake.

Amejichanganya kwa kuingia mambo ya imani na udini; atakuwa kwenye vyombo vya habari sasa, haya yote yatakuwa public domain soon.
 
Mwankijiji,
Mbowe na Chadema wana Uhusiano mzuri sana na CUF chama ambacho mimi ningeweza kusema kingekuwa cha kwanza kuondoa mahusiano yake na Mbowe kwa sababu Ansar Sunni wamejaa telee!!

Kaka hata mimi naichukulia hii habari kwa machale sana. Hata hivyo kwa list ya mashehe waliotajwa hapo naamini ni rahisi kwao kuingizwa mtegoni. Sitashangaa kama kuona mkono wa UWT katika kukarabati hilo na hata huo mkanda unaodaiwa kuwepo. Ni bahati mbaya sana ukitoa athari za UFISADI na UKADA, tatizo lingine kubwa katika asasi hii nyeti ni suala la allegiance to national interest Vs religious groups interests.....

Lakini kuhusu huu uhusiano mzuri wa Mbowe/CHADEMA na CUF kwa kweli sina uhakika. Nijuavyo mimi uhusiano wao ni wa shingo upande na umegubikwa na hali ya kutokuaminiana, kuoneana wivu na hata prejudices.....Wapo ambao wanajitahidi kubadili hali hiyo kutoka kila upande lakini hali bado sio nzuri....

Tanzanianjema
 
Tanzania bwana yangu macho na masikio,Mungu atusaidie tu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom