Hali hii husababishwa na vitu vitatu ambavyo nataka
Paula Paul uangalie wewe utakua umedondokea kundi gani kati ya haya matatu nitakayoyachambua kulingana na upeo wangu
1.Makuzi yako utotoni
Wakati ukiwa mdogo ulikuwa na kulelewa katika aina gani ya mazingira,kuna wale wamezaliwa mtoto m1 tu kwenye familia then mama na baba wapo busy na mishe zao hivyo kupelekea huyu mtoto kukua ktk hali ya upeke ake peke ake na mwisho anazoea hii hali,na matokeo yake akikua Hawezi dumu na marafiki kamwe.
au mwingine kazaliwa kisha wazazi wake baba na mama wakaachana hivyo mzazi m1 kaamua kumchukua mtoto na kuondoka nae au kumpeleka kwa ndugu,huyu mtoto kwakua tyr kashaelewa haya sio mazingira yangu,lazima atajitenga tenga na mwisho ataanza kuwa pekeake na baadae atazoea maisha hayo,ila effect zinakuja onekana ukubwani,hatoweza dumu na marfiki,mifano ya kundi hili ipo mingi.
2.Waliotendwa/kuumizwa (na marafiki)
Hawa ni wale sio kwamba hawawezi kuwa na marafiki au kudumu nao,hawa ni wale kwanza wanapenda marafiki sana sana ila shida yao ni moja "yalishawakuta" walifanyiwa umafia,au jambo baya lolote kiasi kwamba sasa hivi muda wa kufatana fatana au kuwa intouch saaaana na mtu hawawezi,hujikuta wakikumbuka nyuma na mwisho hujisemea "sihitaji yanikute tena" matokeo yake hushindwa kudumu na marafiki.
ila kutokudumu kwao na marafiki haimaanishi wamewachukia hao wengine hapana,Upendo upo ila wanaishi maisha ya wasi wasi ya kutoamini tena mtu mwngine na effect zake ndio hizo kwenye thread yako
Paula Paul (kundi hili ndio lina watu wengi hata kwnye hi thread wengi wanatoka kundi hili.
3.Nature
Hawa ni wale waliozaliwa hivi,ki ufupi ni aina ya watu hat kama wamezaliwa kwenye familia yenye watoto 7,ila yeye ni mt wa kujitenga tenga mkimya mkimya mfata mambo yake,ndugu zake wakicheza game wakibadilishana Pad yeye Hana time na game muda huo,atasubiri wamalize kucheza wakiondoka wote yeye ataenda atashika Pad atacheza mwenyewe au atachagua mtu anaemtaka yeye acheze nae,akimaliza hapo HUYOOO anaondoka zake.
huyu yeye siku zote n mpole mpole,mkimya mkimya,sio kwamba anachuki na wengine Hapana huyu ndio alivyoumbwa,mfano wa huyu mtu ni kama jamaa anaitwa PROFESSOR kwenye season inaitwa MONEY HEIST huyu kiumbe ni mtu wa peke ake pake ake,lipo kama jinga jinga flani,ila Ana upendo wa hali ya Juu kwa wenzake sema ndio huwezi mgundua.(ana akili huyo acha kabisa)
watu wa aina hiii wakiwa watu wazima ndio effect zao huonekana kwasababu hatoweza dumu na rafiki na haoni shida kukaa bila rafik kwasababu ndivyo alivyoumbwa.
Tukirudi kwenye swali lako la Je Ni tatizo au si tatizo?
Jibu nadhani linategemea wewe upo kundi gani hapo juu.