Hahaa. Mtu anayeweza kukaa na wa kishua, halafu akakaa uswazi.Akakaa na mabaharia, halafu akakaa na walokole. Akakaa na wabongo, halafu akakaa na wanyamwezi.
Akawa mpenzi wa kujiendeleza kielimu, akajua changamoto za maisha na namna mbalimbali za kuzikabili...
Nafikiri anaweza kusema amepata maksi za kiasi fulani katika kile Wafaransa wanachokiita "savoir faire", uwezo wa kuwa na maadili na ujuzi wa kufanya kitu sahihi, kwa muda sahihi, pahali sahihi.
Sasa hapo ndipo unapokuta mtu kaleta mchango JF kitu ambacho watu washapitia, kinajulikana, mara nyingine hata kumueleza kwamba hilo jambo watu wengi wanalo na ni kawaida inakuwa faraja kubwa. Kwa sababu pengine mtu anaweza kujiona yeye ni wa ajabu, wakati hata nusu ya robo ya ajabu hajafikia.
Kiranga
Umenifurahisha na comment zako na imenikumbusha msemo ukitaka kupata marafiki wa kweli ishi maisha kama ya kinyonga zaidi ni kijifunza kuangalia mazuri ya mwenzako ikiwezekana mpongeze kwa jambo zuli alilanalo na kuwa mwepesi wa kuomba msamaha pale unapokwaza wenzako . Kumbuka Mungu ndiye aliyeumba watu wote mshua, wa uswazi, msomi , baharia , lofa , mdini , mdhambi . Mimi nimejifunza kumfurahia mtu kama alivyo , kila binadamu ana jisikia faraja kuona anathaminiwa .
Urafiki hujengwa au uja wenyewe au waweza amua maisha yako hutaki rafiki labda kwa kujiona unajitosheleza kwa kila kitu , wazungu wa western countries wengi wao kutokana na utoshelevu kimaisha wananiona kinachobaki ni kazi na kutaradadi dunia kukutana na watu wapya maisha mapya maisha yao ya kitajiri , afrika matajiri hasa ni wachache na utamaduni wa afrika kama ndoa na harusi, misiba , maisha kwa ujumla umekaa kirafiki/ kijamaa zaidi.
Mbinu unazoweza kutumia kujenga urafiki imara;
1.Penda na jali watu , misemo kama impressing people endup poor ipotezee
2.Endeleza na furahia career, vipawa, karama zako on the way ukikutana na mtu anatabia kama zako au unavutiwa na maendeleo yake mfurahie usimuonee wivu mtajikuta automatically mnakuwa marafiki .
3.watu unaojisikia furaha kuwa nao waonyeshe hivyo hata kama hamuonani ama kuwasiliana mara kwa mara.
4.Jenga mazoea ya kujichunguza weakness zako mara kwa mara ambazo zinaweza kuudhi watu mfano kama unajiona ni mbinafsi, hasira, chuki, roho mbaya, ugomvi nk tafuta namna ya kuachana na rabia hizo ama kwa kusali na kuombewa au tafuta psychologist au unayemwamini akusaidie ubadilike.
4.Jijengee tabia ya kuwa mtu wa kutoa msaada , kufariji kimawazo, pesa, ujuzi , muda nk usiangalie sana maslai utalipwaje as urafiki sio ajira au fursa kwani changamoto za urafiki ni tofauti na changamoto za ajira / fursa tanguliza sana utu.
5.Jali na wafurahie wenzio zaidi unavyojipenda wewe .
Wale wanaosema wanaona shida kuimarisha urafiki wajaribu mbinu hizi ni uzoefu niliouona kwangu ambao nimeuchunguza kutokana marafiki wengi niilio nao ambao wengi nimedumu nao zaidi ya miaka 30.
Sent from my iPhone using JamiiForums