Asante. Naam.
Kuna rafiki zangu wazuri sana tumejuana zaidi ya miaka 20, wengine 30.
Wengine tulikuwa tunachukua likizo pamoja tunazunguka kuangalia scene ya miji kama Nairobi, Kampala etc. Miaka hiyo.
Sasa tumetenganishwa na jiografia, wao wako Tanzania, mimi niko Marekani.
Na inaweza kupita miezi hatujawasiliana, lakini tukiwasiliana moto wa urafiki uko pale pale.
Tunashirikiana kwenye misiba, harusi, watoto wanazaliwa, urafiki haujapungua kwa sababu ya umbali au kutowasiliana kila siku.
Mimi rafiki anayetaka kuwasiliana extensively kila siku sitamuweza.
Imagine una marafiki 10 halafu wote wanataka kuwasiliana extensively, one on one, kila siku. Huo utakuwa utumwa.
Kuna mambo yangu mengine mengi, maelfu ya vitabu, movies, documentaries, kaka mkubwa kwenye family mimi, mambo ya kazi manyota nategemewa mimi etc.
Uzuri au ubaya ni kwamba nilishakuwa "life of the party", literally. Yani watu walikuwa wanatangaza party kwa jina langu, kwamba Kiranga atakuwepo, watu wakisikia hivyo wanakuja kwa wingi.
Maisha ya marafiki wengi sana.
Halafu nikareject maisha yale.
Nikataka kwenda kuwa Buddhist Monk.
Nikawa na uchaguzi wa mawili, kwenda kuwa Buddhist Monk au kwenda kufanya kazi Wall St.
Nikaona kwenda kuwa Buddhist Monk itakuwa extreme isolation. Nikaamua kupunguza contact na kwenda Wall St.
Lakini baadhi ya rafiki zangu wa zamani nawasiliana nao mpaka leo.
Wengine wanachukua likizo wanafunga safari kunitembelea kutoka Tanzania.
Na mimi nikirudi Tanzania tunaendeleza parties pamoja pale tulipoziacha.
Sent using
Jamii Forums mobile app