Captain George Mazula wa Air Tanzania afariki dunia

Watanzania Tuonyeshe Mapezi Yetu Na Mshikamano Kwa Kutoa Michang Yetu Kwa Madogo Kama Mnavyofanya Sikuzote
 
Captain umetutoka? Ni vigumu kuamini.

Poleni sana ndugu na wanafamilia.

Mungu amlaze pema peponi.


Ameni.
 
We Will B Misin U Much .....

The Great Has Gone Ooooh Ma God Help Us The Rest!!!!!

Jamani Wwenye Taarifa Watoto Wanaingia Lini Bongo Maana Nakumbuka Kuna Mmoja Alikuwa Na Prbl Za Paper Natumaini Kama Bado Aje Tu Jamani Kumzika Mzee Mungu Atampa Sehemu Nzuri Zaiidi Ya Marekani


Oooohhhhhhhh George

Club Tutacheka Na Nani Jo!!!!!!!!!!!!!!

Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Hata Kutuaga Nduguzo Jamani Wiiiiiiiiiiiiiii
 
Last edited by a moderator:
Kapten George Mazula afariki Dunia
Saturday, 02 August 2008
Rubani mkuu wa atc kepteni george mazula amefariki dunia nyumbani kwake mtaa wa nyumbu, mikocheni, dar leo asubuhi baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kupumua.

Msemaji wa familia, dk. charles lugora, amesema kwamba marehemu kepteni mazula alikuwa nchini india kiasi cha wiki tatu zilizopita alikokwenda kupatiwa matibabu ya athma na ali;porejea alikuwa anaendelea vyema hadi hali ilipobadilika ghafla asubuhi ya leo ambapo alifariki dunia milango ya saa nne unusu asubuhi.

Dr. Lugora amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake na ratiba kamili itatolewa kesho. marehemu mazula aliyefariki akiwa na umri wa miaka 59, ameacha mke na watoto wawili (brian na george).

Mtoto wake wa tatu, walter, aliuwawa huko marekani septemba 2006, ambapo yeye na mchumba wake vonetha nkya waliuwawa kikatili na watu wasiojulikana.

mola aiweke roho ya marehemu pahala pema peponi.
 
Kapten George Mazula afariki Dunia
Saturday, 02 August 2008
Rubani mkuu wa atc kepteni george mazula amefariki dunia nyumbani kwake mtaa wa nyumbu, mikocheni, dar leo asubuhi baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kupumua.

Msemaji wa familia, dk. charles lugora, amesema kwamba marehemu kepteni mazula alikuwa nchini india kiasi cha wiki tatu zilizopita alikokwenda kupatiwa matibabu ya athma na ali;porejea alikuwa anaendelea vyema hadi hali ilipobadilika ghafla asubuhi ya leo ambapo alifariki dunia milango ya saa nne unusu asubuhi.

Dr. Lugora amesema mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake na ratiba kamili itatolewa kesho. marehemu mazula aliyefariki akiwa na umri wa miaka 59, ameacha mke na watoto wawili (brian na george).

Mtoto wake wa tatu, walter, aliuwawa huko marekani septemba 2006, ambapo yeye na mchumba wake vonetha nkya waliuwawa kikatili na watu wasiojulikana.

mola aiweke roho ya marehemu pahala pema peponi.

Nilifahamiana sana na George Mazula karibu ya miaka arobaini tangu mwaka 1969 tulipoanza kusoma shule pamoja pale Tambaza High School na kumaliza masomo yetu mwaka 1970. Pia tuliishi pamoja katika hosteli ya wanafunzi wa Kihindi na wachache wa Kiafrika, H. H. The Aga Khan Hostel, Upanga.

Miongoni mwa wanafunzi wengine waliosoma na George Mazula pale Tambaza High School na ambao pia waliishi naye katika H.H. The Aga Khan Hostel (1969 - 1970), Upanga, ni Andrew Nyerere, mtoto wa kwanza wa Baba wa Taifa; High Court Judge Mohammed Chande Othman; kiongozi serikalini na katika usalama wa taifa Omari Mangosongo; mwanasheria James Maugo; news editor, Daily News, Abdallah Yakuti; mwandishi wa habari na sub-editor, Daily News, Balinagwe Mwambungu; mwana siasa Dodo Dafi; mwandishi wa habari, Daily News, na sasa mwandishi wa vitabu, Godfrey Mwakikagile, ambaye pia ni binamu wa rubani Oscar Mwamwaja (marehemu) na Major-General Rhodfrey Owen Mwambapa aliyekuwa mkuu wa chuo cha maofisa wa jeshi, Monduli, na ambaye pia ni marehemu.

Marehemu Oscar Mwamwaja, aliyekuwa na George Mazula kaitka Air Tanzania, ndiye yule rubani aliyepigwa risasi miaka mingi iliyopita wakati ndege ya taifa letu ilipotekwa Mwanza na kulazimishwa kwenda Uingereza. Ndege ile iliendeshwa na Deo Mazula, kaka ya George Mazula, na Oscar Mwamwaja alikuwa ni co-pilot wa ndege hiyo.

Wengine waliosoma na George Mazula pale Tambaza High School na walioishi naye katika H.H. The Aga Khan Hostel ni wanasheria Obeid Mwasha (District Executive Officer, Lushoto), Rashid Hemedi, Simon Shirima na wengineo; madakari Rwiza na Msaki; engineer kwa miaka mingi USA na Tanzania, Walter Mallya; Rodgers Nsekela, Geoffrey Mbogo, Suleiman Kazema, Hamisi Kasanga na wengi wengineo.

Wote hao walimaliza Form VI na George Mazula pale Tambaza High School na waliendelea na elimu yao katika vyuo vikuu mbali mbali nchini Tanzania na ng'ambo.

Walio hai kati ya hao niliowataja wanamkumbuka sana George Mazula kama nami pia ninavyomkumbuka. Karibu wote hao niliowataja walikuwa darasani pamoja na George Mazula pale Tambaza High School.

Poleni sana familia yake, ndugu zake na marafiki zake.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
 
R.I.P Captain Mazula, tumepoteza Rafiki na ndugu wa kweli mwenye kuipenda nchi yake kwa dhati.Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi
 
R.I.P Captain Mazula, tumepoteza Rafiki na ndugu wa kweli mwenye kuipenda nchi yake kwa dhati. Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi

Alipokuwa mwanafunzi pale Tambaza, nakumbuka wanafunzi wengi walijua mara moja kwamba George Mazula aliipenda nchi yetu kwa dhati na alikuwa tayari kufanya chochote kulitumikia taifa letu. Alikuwa jasiri, shupavu, lakini pia mnyenyekevu.

Alichaguliwa na headmaster wetu, Mr. Lila, kuwa head prefect mwaka 1970. Kabla ya hapo mwaka 1969, alichaguliwa kuwa mmoja wa ma prefect wa shule yetu Tambaza High School. Na sisi sote tulijua kwamba alistahili kuwa kiongozi.

Na licha ya madaraka aliyokuwa nayo, alijulikana kuwa ni mtetezi wa wanyonge. Wengi wetu tulisema kwamba angefaa kuwa kiongozi miaka ijayo na tulifikiri kwamba labda angesomea masomo mengine - na si ya kisayansi - ili apate kazi serikalini na kuendelea huko mpaka atakapokuwa kiongozi wa taifa. Alikuwa katika Form V na Form VI Science (1969 - 1970).

Na katika mazungumzo yetu, alisema mara nyingi kwamba anataka kuwa rubani - na atakuwa rubani! Hakuwa na mashaka hata kidogo. Na alifanikiwa.

Alikuwa ni kiongozi. Hata headmaster wetu, Lila, alijua mara moja alipomchagua kuwa prefect mwaka 1969 na head prefect mwaka 1970 kwamba ni kiongozi na anastahili kuwa kiongozi wa wanafunzi wenzake.

Nakumbuka pale H.H. The Aga Khan Hostel, Upanga, kulikuwa na wanafunzi wa Kihindi tulioishi nao walioonyesha kwamba wanatudharau sisi wanafunzi weusi. George Mazula aliwanyosha mara moja mbele ya wanafunzi wengine, na kwa sauti nzito, na walikuwa wanamwogopa sana; si kwa sababu alikuwa anawakandamiza - walimwogopa kwa sababu alikuwa anasema ukweli mbele ya watu.

Alijulikana katika shule yetu kama Msema Ukweli. Hakumwogopa mtu. Lakini kuliko kitu chochote kama prefect pale Tambaza High School, aliheshimiwa na alipendwa sana na wanafunzi wenzake kwa sababu alikuwa ni mtetezi wa wanyonge.

Na angekuwa jeshini, sisi sote tuliomfahamu tungemwona askari shupavu, na General, anayeongoza jeshi letu vitani kuilinda nchi yetu.

A true patriot! A gem! Tangu alipokuwa kijana hadi alipotuondoka.

Ametuacha, lakini bado yuko nasi mioyoni. And the ideals he cherished and upheld will always inspire us. Daima!

Kwaheri, Ndugu Mazula, and rest in peace until we meet again where you are. There's a better place than the world you left behind. Umetutangulia, tutakufwata. As always, tuko nyuma yako.

Rest in peace, Ndugu! Mzalendo halisi!
 
Alichaguliwa na headmaster wetu, Mr. Lila, kuwa head prefect mwaka 1970. Kabla ya hapo mwaka 1969, alichaguliwa kuwa mmoja wa ma prefect wa shule yetu Tambaza High School. Na sisi sote tulijua kwamba alistahili kuwa kiongozi.

...Historia hiyo, ahsante sana.

(Marehemu) Mzee Bori Lilla naye alikuwa Headmaster wa kwanza mwafrika, pale Tambaza Sekondari.

Mwenyezi Mungu awarehemu, na wote waliotutangulia.
 
Poleni familia na Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.. amina
 
Poleni wanafamilia na marafiki wa marehemu na Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Captain Mazula.
 
Alikuwa mtu mzuri sana, mola ailaze roho yake pema peponi.

Alikuwa ananifurahisha jinsi alivyokuwa anavyotuisha ndege yake, huskii ikogota kama mzigo ulioanguka kutoka ghorofani.

Aliwahi kuni-upgrade free of charge kwenda first class wakati natoka Mwanza hadi Dar kwa vile makarani wa Mwanza walifanya uzembe wakapitisha abiria wengi zaidi ya nafasi za economy class. Sasa kwa vile mimi nilichelewa kuingia kwenye ndege ile kutokana urabu niliokuwa nao pale uwanjani akasema mzee mwenzagu wewe kaa first class ya bure, na kama kawa pale tena nikapata urabu mwingine tena wa bure.

Kapteni Mazula ni jina lililotukukua sana katika nyanya ya aviation nchini mwetu tangu enzi za EAA; kwa kweli tutamkosa sana. Mungu apumzishe roho yake kwa amani hadi sote tutakapoungana naye siku yetu ikifika kwa vile ndiyo njia yetu.
 
Dear All,



The following are the funeral and burial arrangements time table for the
late Capt. George Mazula on Wednesday the 6th of August 2008.





1. From 11.00 to 12.00 hours Lunch at the late Capt Mazula's residence

2. From 12 .30 to 13.45 Requiem mass at St. Martha Catholic Church close to
the late Capt Mazula's residence

3. From 14.30 to 16.30 Last respects at Leaders Club, Kinondoni; and

4. Followed by burial at Kinondoni 2nd World War Memorial Graves

R.I.P G.MAZULA

Regards,

WAFIWA
 
mkuu ni yale WAZITO MKUU KULE CHINI/!!!KABISA UKIWA UNAENDA POSTA

NI MARACHACHE KAJAMBANANI KUZIKWA KULE UNLESS ULIKUWA UNAMBEBEA

MABEGI LOWASSA!!!KWA HUYU BWANA AKI YAKE KABISA KWA UPENDO ALIOKUWA NAO.....

KAMA NI UWEZO HATA IKULU UNAMLAZA HUYU ULALE PEMA PEPONI KAKA
 
Poleni wafiwa wote. Hata hivyo nina kaswali kadogo tu kwa wataalamu wa Urubani na mambo ya Anga: Kwa magonjwa kama PUMU, yanayomkamata mtu ghafla na wakati wowote, bado mtu huyo anaruhusiwa kurusha ndege?
 
mimi pumu inanishangaza,huku duniani,hata siku mmoja sijaona mtu kabanwa pumu,lakini mtu atakwambia ana pumu.lakini nyumbani,watu hushindwa hata kupumua na hupata matatizo sana,au sijui ni hali ya hewa.would someone please make my day and explain this anomaly.
 
Back
Top Bottom