Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
MMILIKI wa baa ya Tale mjini Njombe, Jackson Mgeni (35), mkazi wa Mji Mwema mjini hapa, amefariki dunia kutokana na kuchomwa kisu tumboni na anayedaiwa mteja wake, Emmanuel Shiwa (32).
Mfanyabiashara wa madini na mkazi wa eneo la Uwanja wa Ndege mjini Njombe, anadaiwa kutenda ukatili huo baada ya kutokea ugomvi kati yao alipomwita Mgeni, akitumia neno 'mhudumu'.
Ni tukio hilo lilitokea Novemba jana saa nane usiku katika baa hiyo ya mjini Njombe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi Mahamoud Banga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema mtuhumiwa ni mteja mzoefu katika baa hiyo.
"Katika hali ya kupata huduma, mtuhumiwa alimwita Mgeni kwa jina la mhudumu. Sasa kile kitendo cha kuitwa mhudumu, ninafikiri kilimuudhi.
"Akaanza kugombana na yule mteja na yule mteja ninafikiri aliona hatoweza kupigana naye kawaida. Hivyo alitoka nje," alisema Kamanda Banga.
Aliendelea kusimulia, akisema: "Mtuhumiwa huyo baada ya kutoka nje alipanda gari lake, akaenda nyumbani kwake.
"Mashuhuda wanasema ni maeneo ya Uwanja wa Ndege, lakini baada ya muda alirudi na kisu na kumvizia yule jamaa na kumchoma nacho tumboni."
Kamanda Banga alisema kuwa baada ya kufanya tukio hilo, wananchi ambao ni wateja wa baa hiyo walikuwapo eneo la tukio, walimdhibiti mtuhumiwa na kutoa taarifa kituo cha polisi.
"Polisi walifika na kumkamata, majeruhi alikimbizwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Njombe (Kibena), lakini kabla ya kuanza kupatiwa matibabu alifariki (dunia)," alisema Kamanda Banga.
Njombe ni miongoni mwa mikoa yenye matukio mengi ya mauaji nchini. Hata hivyo, matukio mengi yanahusishwa na imani za kishirikiana na wivu wa mapenzi.