Captain George Mazula wa Air Tanzania afariki dunia

mwanaizaya

Senior Member
Apr 26, 2008
133
1
Ndugu wapendwa,

02F44907-D205-485C-8611-5A4DECAB03A2.jpeg


KAPTENI Mkuu wa Ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATC), George Mazula (59) (PICHANI) amefariki dunia nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa pumu.

Msemaji wa familia ya Mazula, Dk. Charles Lugora aliliambia HabariLeo jana msibani hapo kuwa Kapteni Mazula alifariki jana saa nne asubuhi baada ya kubanwa ghafla na ugonjwa unaodhaniwa kuwa ni pumu.Kwa mujibu wa msemaji huyo utaratibu wa mazishi ya rubani huyo utafahamika leo baada ya kikao cha familia kilichotazamiwa kufanyika jana saa moja usiku nyumbani kwake namba SGX 4617 K.

Marehemu ameacha mjane mmoja na watoto wawili walioko Marekani wanaotarajiwa kuja wakati wowote kuanzia leo ambao ni (Brian na George). Mtoto mwingine wa Mazula alifariki kwa kupigwa risasi yeye na mpenzi wake miaka miwili iliyopita nchini Marekani.

Mungu amlaze mahali pema peponi

R.I.P GEORGE
 
Last edited by a moderator:
Wanandugu Member Wa Jf
Rafiki Yetu Kaka Yetu Mpendwa Baba Yetu Capt George Mazula Amefariki Hivi Punde Huko Tanzania Habari Kamili
Tuwe Pamoja!!!!!mungu Amlaze Mahali Pema Peponi
!!!!!poleni Sana Wanafamilia!!!!
 
Yeah!!!!so Sad Ni Baba Wa Mtoto Alieuwawa Kule Marekani Detroit
Hali Ningumu Kuamini Wana Jf Tuwaombee Sana Familia Yote Mungu Awatie Nguvu...
 


:(

R.I.P George.

Poleni sana Mazula family, pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote.
 
Ohhhhhhhhhhhhh Ma God!!!!!!!!!!!!!!! Eeeeeeeeeee Mungu

Wazuri Wote Unawachukua!!!!!

George Mwanae Yuko Njian Kuja Kumwona Babayake Akitoka Kwenye Operashen India Ya Mgongo Anakuta Maiti Mungu Weeeeeee!!!!!!!!!!!!

Msalimie Walter Uko Alipo

R.i.p

Mazula
 
Capt. Mazula si ndiye yule aliyekataa kurusha ndege akishinikiza kushushwa kwa tajiri mmoja wa Arusha ambaye ni Swahiba wa Mafisadi. RIP
 
Capt MAzula ni miongozni mwa Wazalendo halisi wa Nchi hii na atakumbukwa kwa ujasiri wake pale alipoirusha ndege ya E.A Airways na kuishusha Tanzania wakati Jumuiya ya A. Mashariki inavunjika. Tumempoteza Shujaa na Mzalendo halisi.

BWANA alitoa na BWANA ametwaa, Jina lake lihimidiwe!
 
Rest in Peace Captain Mazula

Utakumbukwa kwa mchango wako katika ATC na taifa kwa ujumla. salamu za pole kwa familia.
 
Ctaki kuamini kama kweli Mazula Katutoka. The best Rubani we ever Had in TZ. I was so comfortable with his flight
RIP George
 
Oh...Maskini..! nimemkumbuka yule dogo aliyeuawa kule marekani .... its very sad now the dad has also gone..... May the almighty god rest his soul in eternal Peace... Pole nyingi kwa familia kwa kutoneshwa tena kidonda....so sad.!!
 
ndugu wapendwa
poleni wote na msiba mkubwa uliotokea mpendwa wetu rafiki ndugu kaka yetu
captain george mazula wa airtanzania amefariki muda mchache uliopita mengine zaidi tutawaletea amefariki tanzania
mungu amlaze mahali pema peponi
R.I.P GEORGE

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un

Rest in Peace brother George
 
naomba ziwe habari za kweli na uhakika kwa kuwa mtindo wa kusingiziana vifo umezidi siku hizi. amekufa kwa ajali? au nini
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom