Mimi nimelelewa kijijini kabisa na poor woman but responsible, caring, teacher, hardworking, inspirational and tough. Mamangu aliniambia, kuwa uwe mwanaume unayejali familia yako hasa mkeo na watoto wako. Jifunze maisha anayoishi mamako yasije yakatokea kwa mkeo na watoto wako. Alinifundisha kufanyakazi sana na kujitegemea. Kila week end ni jembe sana. Mwanzoni nilidhani ananionea nilipokuwa naanza kupata akili nilianza kumuelewa na kumuonea huruma kuwa mama anahitaji msaada wangu sana. Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa niuza ndizi za kuchoma na kachumbari some of the week end sokoni. Siku za kawaida nilikuwa nikitengeneza ufuta nauviringisha na sukari nauza kwa wenzangu shule. Nakili ni kwamba I was a brilliant and intelligent kid, nilipokua sekondari one to six, kwetu tunalima sana mpunga, nilikuwa nikirudi shule navuna mpunga, nakoboa napeleka Dar kwaajili ya kuuza kwa kina mamantilie kisha nanunua mahitaji yangu ya shule kama begi, madaftari, nguo, sabuni na kuweka akiba ya kutumia shuleni. Haya yote. mamangu ndivyo alivyokuwa akinifundisha. Leo hii. siwezi kumpiga jiwe Mungu, I am successful man and I will be more than who I am today bila kusahau foundation yake kuwa ni mama tu. Hivyo inawezekana kabisa mama kuwa mwalimu bora kama mamangu alivyokuwa. Katika utu uzima wangu siku moja nilikuwa namshukuru mama kwa yote aliyonifanyia na kunifanya kuwa nilivyo leo, akaniambia sio mimi peke yangu na wewe pia umechangia kuwa hivyo kwakuwa nilichokuwa nakuambia kifanye ulikifanya na nilichokukataza ulikiacha kwahiyo mchango wangu na wako umekufanya wewe kuwa ulivyo leo.