lovebitelol
JF-Expert Member
- Mar 2, 2014
- 964
- 972
- Thread starter
- #81
Kwann uishi single? Akati Mungu alimuumba adam na hawa
100% tena haswa haswaSwali ni je, baba hana umuhimu katika malezi ya mtoto?
Dadavua.100% tena haswa haswa
Japo sikufaham ila kama umelelewa na baba tu bas una adab sana kulko waliolelewa na mama tu,Sasa mmoja anapokuwa hayupo mwingine ni dhahiri hawezi kukamilisha ambacho ambaye hayupo angeweza kukiongeza kwa mtoto.
Mimi mwenyewe nimekua na Baba karibia maisha yangu yote.
Mzee, ukibisha au kukataa, ukatae kwa facts na usiwe dogma tu huna ushahidi na bado unabisha hata kama umepewa ushahidi.Hapana Big No
Wahenga walisema hvyo sababu ktk ile age ya mtoto kuanza kujifunza anajifunza zaid kwa mama sbu ya udogo wake,so anapofikisha miaka nane utaanza kuona anaanza kujifunza kutoka kwa baba maana ndio msimamiz wa sheria zote za nyumban kwa kias kikubwaNi vizuri mtoto apate malezi ya wazazi wake wote wawili , lakini katika uhalisia mwanamke anahusika sana katika maisha ya kila siku ya familia husika , kuanzia mume hadi watoto. Ndiyo sababu wahenga walisema " Asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu" na siyo asiyefunzwa na Baba. Wapo watoto chungu nzima wamepata malezi ya mama pekee na wakawa na mafanikio maishani
Huo ndio uthibitisho tunaoutaka hapa sio wengine wanaleta siasa. Ila kwa mtazamo wako ungependa hilo suala lijitokee kwa mtoto wako ambaye huishi nae.
Adabu kweli ninayo... since nipo STD 5 mzee tu.Japo sikufaham ila kama umelelewa na baba tu bas una adab sana kulko waliolelewa na mama tu,
KabisaaaaaaExactly.
Ndiyo maana ukimchukua kijana aliyekulia Kijenge na wa Sinza mori watu wawili tofauti kabisa [emoji3][emoji3]
God bless you.....Kwakweli mtu anahitaji malezi na mapezni sana toka kwa wazazi wote wawili. Najifunza mengi sana juu ya malezi ya watoto wangu. Ninapokuwa napumzika let say kitandani huwa nawaangalia watoto wanavyecheza na mimi kisha wanakimbia kwa mama yao inanipa funzo kubwa sana ninavyoona raha na faraja wanayopata toka kwa wazazi inanifanya nione mapungufu niliyokuwanayo nilipolelewa na mama tu. Sitathubutu kilichotokea kwangu kitokee kwa watoto wangu, Nimegundua kuwa ukitaka watoto wako wawe na raha na furaha ni kuhakikisha mama yao ana raha na furaha na hiyo inanifanya nifanye kila liwalo kuhakikisha my wife mwenye fyraha na raha wakati wote kwa ajili ya mapenzi yangu kwake na watoto wangu. Wanaume tunachangia kwa kiasi kikubwa sana kuwafanya watoto wetu waishi maisha ya ajabu kwa kuwabughudhi mamazao, tujitahidi juu ya hili. Naelewa mapenzi makubwa niliyonayo kwa mama yangu ndio yaleyale waliyonayo watoto wangu kwa mama yao na kama ambavyo siwezi kumpa nafasi mtu yeyote amnyanyase mamangu najua pia watoto wangu wanawaza hivyo. Mapenzi ya mtoto kwa mama ni naturally ila sisi wa baba tunatakiwa kufanya kazi ya ziada kuvutia mapenzi ya watoto kwetu, tuwe responsible, lovely and caring fathers.
Mwanzo nilisema mtoto anakua vzr akiwa na mama ila anakua vzr zaid akiwa na baba,ktk familia mama ndio muangaliz sana sbu muda mwng yupo nyumban tofaut na baba bt baba anasimamia sheria zte za home vzr kulko mama,thats why,mtoto akikua na baba sio rahis sana kufanya ujinga ujinga sbu ya ile hofu ambayo anayo.Dadavua.
[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]Adabu kweli ninayo... since nipo STD 5 nipo na mzee tu.
Wewe ni mwanaume wa dar..?Fikiria kwa makini nimetumia fumbo kusema chips
Wa ndio ila nimetokea villageWewe ni mwanaume wa dar..?
post using my macbook air using jamiiforums app
Mimi nimelelewa kijijini kabisa na poor woman but responsible, caring, teacher, hardworking, inspirational and tough. Mamangu aliniambia, kuwa uwe mwanaume unayejali familia yako hasa mkeo na watoto wako. Jifunze maisha anayoishi mamako yasije yakatokea kwa mkeo na watoto wako. Alinifundisha kufanyakazi sana na kujitegemea. Kila week end ni jembe sana. Mwanzoni nilidhani ananionea nilipokuwa naanza kupata akili nilianza kumuelewa na kumuonea huruma kuwa mama anahitaji msaada wangu sana. Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa niuza ndizi za kuchoma na kachumbari some of the week end sokoni. Siku za kawaida nilikuwa nikitengeneza ufuta nauviringisha na sukari nauza kwa wenzangu shule. Nakili ni kwamba I was a brilliant and intelligent kid, nilipokua sekondari one to six, kwetu tunalima sana mpunga, nilikuwa nikirudi shule navuna mpunga, nakoboa napeleka Dar kwaajili ya kuuza kwa kina mamantilie kisha nanunua mahitaji yangu ya shule kama begi, madaftari, nguo, sabuni na kuweka akiba ya kutumia shuleni. Haya yote. mamangu ndivyo alivyokuwa akinifundisha. Leo hii. siwezi kumpiga jiwe Mungu, I am successful man and I will be more than who I am today bila kusahau foundation yake kuwa ni mama tu. Hivyo inawezekana kabisa mama kuwa mwalimu bora kama mamangu alivyokuwa. Katika utu uzima wangu siku moja nilikuwa namshukuru mama kwa yote aliyonifanyia na kunifanya kuwa nilivyo leo, akaniambia sio mimi peke yangu na wewe pia umechangia kuwa hivyo kwakuwa nilichokuwa nakuambia kifanye ulikifanya na nilichokukataza ulikiacha kwahiyo mchango wangu na wako umekufanya wewe kuwa ulivyo leo.Suala la malezi ya baba na mama ni mada nyingine tofauti yenye uwanja mpana wa kujadili. Lakini hii ya kwetu inauliza. " INAWEZEKANA SINGLE MOM AKAWEZA KUMFUNDISHA MTOTO WAKE WA KIUME JINSI YA KUWA MWANAUME?