CAG Prof. Mussa Assad amjibu Spika Ndugai, Asema Katiba ya JMT haina kifungu kinachomtaka ajieleze


A

africansongs

Member
Joined
Jan 5, 2018
Messages
39
Points
150
A

africansongs

Member
Joined Jan 5, 2018
39 150
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.

======

Mara baada ya mkutano huo wa Spika Ndugai, Mwananchi lilizungumza na Profesa Assad ambaye alijibu kwa ujumbe wa maandishi akisema, Katiba haina kifungu cha kujieleza.

“Soma Katiba 143 ina disciplinary arrangements (mpangilio wa hatua za nidhamu), kujieleza haimo,” alisema Profesa Assad.

Ibara ya 143 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inasema “Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza”.

Ibara ya 144(3) inasema “iwapo Rais anaona kwamba suala la kumuondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa” atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili.

Sehemu hiyo inasema mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni majaji au watu waliopata kuwa majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani.

Awali katika maelezo yake, Ndugai alimsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

Aliendelea kusema pia kuwa hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu.

“Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri
 
okiwira

okiwira

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Messages
651
Points
500
okiwira

okiwira

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2018
651 500
Mkuu mkakati uliopo ni wa Ndugai kujiudhuru.

Ili Ngosha aibuke mshindi midomoni mwa wapinzani
 
M

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2011
Messages
4,744
Points
2,000
M

Mkirindi

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2011
4,744 2,000
Habari ya ripoti ya CAG imefika vijijini. Watu wana mapenzi nae mno, akijiuzuru subirini maandamano ya nguvu kupinga kujiuzuru kwake.
Sasa haya ndiyo yatakuwa maandamano yenye tija, muhimu kwa taifa na unganishi, maandamano ambayo yatakuwa mali ya wananchi kwa ujumla tena yasiyo pendelea chama chochote.

Hata mie na wanangu tutajiunga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Messages
5,007
Points
2,000
thetallest

thetallest

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2017
5,007 2,000
Acha kukurupuka,hakulazisha,alishauri,kama alilazimisha weka proof hadharani,kwa kupitia clip.

Nyie kwa upumbavu wenu ndio mnaokuza huu mgogoro kwa vi thread vya kijinga
Badala ya Ngugai kusononeshwa na matumizi mabata ya fedha,yeye kaumizwa na neno dhaifu.

Badala ya kuhoja zilipo Bil 800 ambazo hazipo kwenye mahesabu,yeye kakazana na kuumizwa kuitwa dhaifu

Badala ya kuumizwa na Matumizi yasiyoidhinishwa na bunge eti kaumizwa na kuitwa dhaifu.

Wito kwa watanzania,ndugai ajiuzulu ili kulikomboa bunge letu.

Ndugai kwa sasa hana Moral Authority ya kuendelea kuwa Spika.

Rais anapinga ufusadi,na ndio maana kampuuza ndugai kwa kupeleka ripoti bungeni.

Rais hapendi wizi,ndio maana kila mara anatumbua,halafu mtu anaemsaidia Rais kuona panapovuja etu ndugai hamtaki.

Ndugai anataka CAG atakaekuwa na tabia kama ndugai,CAG atakaeficha ukweli ili kuwafurahisha wanaomlipa.

Ndugai anathubutu kumfananisha Prof aliebobobea na anaeamini na umoja wa mataifa,halafu anafananushwa na Mbwa?

Au ugonjwa wake umeanza kupanda?
Ndugai must go.
Tanzania tunaheshimika sana,ndugai apumzuke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waterloo

Waterloo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Messages
16,064
Points
2,000
Waterloo

Waterloo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2010
16,064 2,000
Na bunge linaweza kumfuta kazi rais kwahiyo rais hayuko juu ya bunge
Mihimili ya utawala iko mitatu lakini Rais wa Nchi ndo mkuu wa mihimili yote hiyo. Baada ya Uchaguzi Mkuu ni Rais anayelifungua Bunge rasmi,je kaka Rais siyo sehemu ya Bunge ni kwa nini alifungue? Majaji wa Mahakama Kuu huteuliwa na Rais, je Rais siyo sehemu ya Mahakama?
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
18,745
Points
2,000
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
18,745 2,000
Acha kukurupuka,hakulazisha,alishauri,kama alilazimisha weka proof hadharani,kwa kupitia clip.

Nyie kwa upumbavu wenu ndio mnaokuza huu mgogoro kwa vi thread vya kijinga
Mmefikia mahala mnashindwa kuchagua wa kumtetea.. JOBU, CAG au JIWE...? Maana kitendo cha kwamba wote wapo upande mmoja ndo kinawatoa jasho… INGEKUWA MMOJA WAPO YUPO CDM katika hao, zigo la ubaya wote mngemtwisha yeye… mnabaki kutukana na kulazimisha kwamba JOBU harumbani na CAG ila sisi tunaoandika ndo tunaona hivyo…!!!! AIBU... Mwenzenu mmoja keshawaambia, KAMA MMEJIPAKA MASIZI JIFUTENI
 
nasrimgambo

nasrimgambo

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2017
Messages
537
Points
500
nasrimgambo

nasrimgambo

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2017
537 500
Badala ya Ngugai kusononeshwa na matumizi mabata ya fedha,yeye kaumizwa na neno dhaifu.

Badala ya kuhoja zilipo Bil 800 ambazo hazipo kwenye mahesabu,yeye kakazana na kuumizwa kuitwa dhaifu

Badala ya kuumizwa na Matumizi yasiyoidhinishwa na bunge eti kaumizwa na kuitwa dhaifu.

Wito kwa watanzania,ndugai ajiuzulu ili kulikomboa bunge letu.

Ndugai kwa sasa hana Moral Authority ya kuendelea kuwa Spika.

Rais anapinga ufusadi,na ndio maana kampuuza ndugai kwa kupeleka ripoti bungeni.

Rais hapendi wizi,ndio maana kila mara anatumbua,halafu mtu anaemsaidia Rais kuona panapovuja etu ndugai hamtaki.

Ndugai anataka CAG atakaekuwa na tabia kama ndugai,CAG atakaeficha ukweli ili kuwafurahisha wanaomlipa.

Ndugai anathubutu kumfananisha Prof aliebobobea na anaeamini na umoja wa mataifa,halafu anafananushwa na Mbwa?

Au ugonjwa wake umeanza kupanda?
Ndugai must go.
Tanzania tunaheshimika sana,ndugai apumzuke

Sent using Jamii Forums mobile app
tena udhaifu wa hali ya juu maana inadhihirisha kwa kiwango gani hata spika mwenyewe muongoza bunge ana madhaifu ya kufahamu vyema sheria na kanuni na mipaka yake ya mahusiano ya kiofisi baina ya bunge na CAG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PRINCE CROWN

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Messages
4,653
Points
2,000
Age
43
PRINCE CROWN

PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2013
4,653 2,000
Tatizo hapa ni mwana siasa. Na mwana taaluma mbobezi.
 
M

mzee wa kismati

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2013
Messages
1,947
Points
1,500
M

mzee wa kismati

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2013
1,947 1,500
****** is the worst subufa we ever had
 
mwanadome

mwanadome

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
3,351
Points
2,000
mwanadome

mwanadome

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
3,351 2,000
Uko sahihii mkuu. na ndugai hayuko peke yake Katika vita hiii
Ndugai anataka kutotua kwenye reli tusijadili ripoti ya CAG kama alivyotutoa kwenye reli tusijadili ripoti maalum ya CAG kuhusu trilion 1.5 kwa kujifanya anamuita CAG bungeni ajieleze wakati majadala wa Trilion 1.5 ukikaribia
USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO
 
M

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Messages
5,266
Points
2,000
Age
43
M

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2013
5,266 2,000
Kiuhalisia na bila kificho, spika kuna jambo lililopo kwenye ile ripoti inamgusa na ndio maana kaweka nguvu nyingi kupambana na neno dhaifu badala ya ripoti yenyewe ili ripoti isijadiliwe kiufasaha!
Hebu aipishe ofisi ya umma na kuiruhusu ripoti ile ijadiliwe kwa kina! Anachosha na kubore sana hasa kwenye mambo ya msingi!
Asiwachukulie watanzania kama watu wajinga. Aondoke haraka ofisini ili ampe nafasi rais mzalendo apambane na ufisadi kikwelikweli!
 
Mzalendo2015

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Messages
3,462
Points
2,000
Mzalendo2015

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2012
3,462 2,000
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.
Ndugu yangu,
Usipate taabu ya kuuliza sijui mshindi ataibuka nani....Mbona mshindi katika hii vita anajulikana na si mwingine isipokuwa Prof. Mussa Asad.
Ndo maana unaweza kuona Spika Ndugai ni kama maeishiwa pumzi/hoja kwa sasa anahangaika na kutapatapa atokee wapi.
Prof. Assad ni ngima nzito mpaka Ikulu imepoteza mwelekeo. Ogopa sana mtu makini anayemtegmea Mungu halafu hana chembe ya ufisadi hata kidogo.
Kinachofanyika sasa ni Ndugai, Bunge, CCM na Magufuli kumpiga vita Prof. Assad kwa kuanika madudu wanayofatnya nyuma ya pazia huku wakijidai ni watu safi kumbe wamejaa unafiki mtupu.
 

Forum statistics

Threads 1,285,012
Members 494,369
Posts 30,847,295
Top