CAG Prof. Mussa Assad amjibu Spika Ndugai, Asema Katiba ya JMT haina kifungu kinachomtaka ajieleze

A

africansongs

Member
Joined
Jan 5, 2018
Messages
39
Points
150
A

africansongs

Member
Joined Jan 5, 2018
39 150
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.

======

Mara baada ya mkutano huo wa Spika Ndugai, Mwananchi lilizungumza na Profesa Assad ambaye alijibu kwa ujumbe wa maandishi akisema, Katiba haina kifungu cha kujieleza.

“Soma Katiba 143 ina disciplinary arrangements (mpangilio wa hatua za nidhamu), kujieleza haimo,” alisema Profesa Assad.

Ibara ya 143 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inasema “Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza”.

Ibara ya 144(3) inasema “iwapo Rais anaona kwamba suala la kumuondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa” atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili.

Sehemu hiyo inasema mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni majaji au watu waliopata kuwa majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani.

Awali katika maelezo yake, Ndugai alimsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

Aliendelea kusema pia kuwa hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu.

“Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri
 
Bill

Bill

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
5,176
Points
2,000
Bill

Bill

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
5,176 2,000
neno hkili ni sawa na wanasiasa aanavyotuita wananchi wanyonge kwani sisi tunape da kuitwa wanyonge WAO DHAIFU SISI WANYONGE
Pia wao wanavyopenda kuitwa MHESHIMIWA, hivi walishatuuliza sisi wananchi ikiwa tunapenda kuwaita hilo jina. Kinyume cha MHESHIMIWA kuna MDHARAULIWA.

Wote tuitane ndugu, Ndugu Spika Job Ndugau, Ndugu Rais nk.
 
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
17,059
Points
2,000
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
17,059 2,000
CAG ni mwenyekiti wa chama gani cha kisiasa ?? kwa Maana yupo busy kweli kupambana na hoja za kisiasa Badala ya kutekeleza majukumu yake kitaalam.
 
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
3,849
Points
2,000
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
3,849 2,000
Hii ni intellectual fight haihitaji muscles elongated. Sasa sijui kama hao wapiganaji wanazo weapon za kutosha kusimama kwenye battle hii. Naona wanapigana Watu ambao hawapo katika level moja
 
Njopino

Njopino

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2014
Messages
1,146
Points
2,000
Njopino

Njopino

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2014
1,146 2,000
Hii ni intellectual fight haihitaji muscles elongated. Sasa sijui kama hao wapiganaji wanazo weapon za kutosha kusimama kwenye battle hii. Naona wanapigana Watu ambao hawapo katika level moja
Ndio shida ya wanasiasa wanaamini wana ushawishi mahali popote pale hata pasipo stahiki kuweka kauli wanaweka kauli pasipo stahali mapambano wanaweka mapambano hata kama sio field yao, hii ni asymmetrical fighting, Kwa akili ya kawaida kwanza Ngugai kuanzisha fight na Prof. Ni kumdharirisha Prof. kulikuwa na njia nyingine ya kufanya argument kama ana concern na Prof. Kwa mtu mwenye akili asingeweza kusimama open field na Asaad. Na hilo ndio tatizo la nchi yetu, tunachukulia elimu ni jambo dogo sana.
 
K

Kifoi

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2007
Messages
941
Points
500
K

Kifoi

JF-Expert Member
Joined May 12, 2007
941 500
Serikali na Bunge ni vitu viwili tofauti...hivyo Ndugai aache uongo. Rais hawezi kuwa sehemu ya Bunge hata kama anasaini yanayopitishwa na Bunge.

Mihimili ipo mitatu. Spika Ndugai aache chuki binafsi na CAG, kwanza CAG hakusema bunge ni dhaifu ila alisema "kama mapendekezo ya CAG kuhusu upotevu wa pesa hatua hazitachukulia haitakuwa suala lake bali litakuwa ni udhaifu wa bunge" hapo amejibu swali kutokana na jinsi alivyoulizwa.

Hapa linaloendelea kutokea ni kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana wa fedha za umma kwa hiyo wanaona jinsi ya kulificha hili tatizo ni kumtibua CAG na kumsemea uongo ili afukuzwe.

Hakuna asiyejua nia ya ndugai na Magufuli....kumfukuza CAG na kumuweka mtu wa aina ya Doto James ili waendelee kuchukua fedha zisizo idhinishwa.
tatizo hasa hapa ni dini ya asad
 
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
9,323
Points
2,000
Age
27
Detective J

Detective J

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
9,323 2,000
CAG ni mwenyekiti wa chama gani cha kisiasa ?? kwa Maana yupo busy kweli kupambana na hoja za kisiasa Badala ya kutekeleza majukumu yake kitaalam.
Hoja gani za kisiasa ana pambana nazo? Cheocha CAG sio cha kisiasa bali kikatiba.
Na analindwa na katiba.
Labda umwambie ndugai aache kuweka siasa kwenye common sense

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyox official

Nyox official

Senior Member
Joined
Feb 12, 2019
Messages
141
Points
225
Nyox official

Nyox official

Senior Member
Joined Feb 12, 2019
141 225
A
Usimuhusishe mpendwa wetu katika hili, hawezi kuingilia jambo dogo kama hili hawezi kuingia mtego wa kubishania neno dhaifu tena katika nchi ya watu maskini na wanyonge. Yuko busy tuletea maendeleo wananchi.
Tukutane 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akil z Kilumumba hizi,yaan suala la kujadil kodi za wananchi zinazoliwa na wachache c maendeleo ila kuzunguka mikoan ya tz kuonyesha kua kafanya maendeo kwa kuwadangany watz ndo ww unaona n maendeleo
 
Gidbang

Gidbang

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2014
Messages
1,576
Points
2,000
Age
43
Gidbang

Gidbang

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2014
1,576 2,000
Mkuu hakika umenena,eti sisi wanyonge wao kuitwa dhaifu nongwa,inabidi watufafanulie mwananchi ni nani,nahuyo mwananchi mnyonge ni yupi.Kumbe wao so wananchi na si wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu ni mtu mmoja tu Ndugai nadhani tua ze kuweka petition ya kumtoa kwenye kiti chake yule P.... aliyewahi kusoma gazeti la Sani anajua Jina la P
 
Mwalupii

Mwalupii

Member
Joined
Feb 9, 2013
Messages
21
Points
45
Mwalupii

Mwalupii

Member
Joined Feb 9, 2013
21 45
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.

======

Mara baada ya mkutano huo wa Spika Ndugai, Mwananchi lilizungumza na Profesa Assad ambaye alijibu kwa ujumbe wa maandishi akisema, Katiba haina kifungu cha kujieleza.

“Soma Katiba 143 ina disciplinary arrangements (mpangilio wa hatua za nidhamu), kujieleza haimo,” alisema Profesa Assad.

Ibara ya 143 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inasema “Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza”.

Ibara ya 144(3) inasema “iwapo Rais anaona kwamba suala la kumuondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa” atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili.

Sehemu hiyo inasema mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni majaji au watu waliopata kuwa majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani.

Awali katika maelezo yake, Ndugai alimsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

Aliendelea kusema pia kuwa hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu.

“Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri
Hii ni ngoma nzito mwenye ngoma anasubiri ya kama ya Lisu.
 
M

Mzinza wa town

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2018
Messages
237
Points
250
M

Mzinza wa town

JF-Expert Member
Joined Mar 15, 2018
237 250
Hii isomwe in Maguvanga voice...
Msema kweri ni mpenzi wa Mungu na CAG amesema ukweri tatizo watanzania tulizoea kusifiana tuuu hata vitu vya uongo,kama sikumfukuza bashite na kelele za wengi mnadhani nitamtumbua huyu siieigii.badala wafanyizie kazi ripoti wanazurura mara Doha,mara naskia yuko swideni tena kwenye limerii eti anafungua mkutano,mara anakimbilia waandishi dar tumepoteza milionzi ofu mane wewe unanguvu za kusafiri hovyohovyo. mimi nimekataa mikutano mingapi kwaajili ya kazi za watanzania ifike mahali viongozi tumtangulize Mungu mbere na tuwe na uzalendo! Mimi nimewahi kuita watu vilaza mbona sijajiuzulu,niliwaambia viongozi wastaafu wanawashwa-washwa kwahiyo nijiuzulu,nimesema hata sisiemu kuna majizi hilo neno ni gumu lakini ndiyo ukweri wenyewe. Wakaangalie kwenye kamusi udhaifu na majizi lipi neno laini nalipi zito. Mmezoea maneno malainii mimi kipindi changu nataka maneno magumu tena sieijii akitoa ripoti yake mwakani awe amevuta kabangi kake polepoooole ili awatandike vizuri!! tunawalipa mamilioni wanakaa vikao kurushiana vijembe huo ni uzaifu jamani au tuuite uzinifu? Haya tuchape kazi tuache maneno.hapa kazi tuu,natumbua watu wezi na wasioweza kazi siyo walioongea sijui nini mtu akachukia!! Siunywe maji utatulia au ulivyoenda uko katari ungekunywa kawaini kidogo ukasahau.
😂😂😂😂😂😂😂
 
J

jaranono

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Messages
642
Points
1,000
J

jaranono

JF-Expert Member
Joined Jun 24, 2015
642 1,000
Hayo ya maandamano ndio maana lile jeshi lisiloshindwa kitu kilitoa ujumbe wa AMANI! na wa UDOM akatoa tamko la kuchakaza Prof asijaribu kujiuzulu maana ataleta shida kwa wapenda haki nchini.
 
Forum statistics

Threads 1,284,202
Members 493,978
Posts 30,817,083
Top