CAG Prof. Mussa Assad amjibu Spika Ndugai, Asema Katiba ya JMT haina kifungu kinachomtaka ajieleze


A

africansongs

Member
Joined
Jan 5, 2018
Messages
39
Points
150
A

africansongs

Member
Joined Jan 5, 2018
39 150
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.

======

Mara baada ya mkutano huo wa Spika Ndugai, Mwananchi lilizungumza na Profesa Assad ambaye alijibu kwa ujumbe wa maandishi akisema, Katiba haina kifungu cha kujieleza.

“Soma Katiba 143 ina disciplinary arrangements (mpangilio wa hatua za nidhamu), kujieleza haimo,” alisema Profesa Assad.

Ibara ya 143 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, inasema “Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu hatalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu mwingine yeyote au idara yoyote ya Serikali, lakini maelezo hayo ya ibara hii ndogo hayataizuia Mahakama nayo kutumia madaraka yake kwa ajili ya kuchunguza kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu ametekeleza”.

Ibara ya 144(3) inasema “iwapo Rais anaona kwamba suala la kumuondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kwa mujibu wa masharti ya ibara hii lahitaji kuchunguzwa” atateua Tume Maalum ambayo itakuwa na mwenyekiti na Wajumbe wengine wasiopungua wawili.

Sehemu hiyo inasema mwenyekiti na angalau nusu ya wajumbe wengine wa tume hiyo itabidi wawe watu ambao ni majaji au watu waliopata kuwa majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani.

Awali katika maelezo yake, Ndugai alimsifu Profesa Assad kwa ujasiri wake huku akiufananisha na ujasiri wa mbwa kumtukana mtu anayemlisha.

Aliendelea kusema pia kuwa hana chuki binafsi na Assad bali tatizo ni lugha tu.

“Unatukana hadi mkono unaokulisha, inahitaji ujasiri
 
U

Umkonto

Senior Member
Joined
Dec 27, 2018
Messages
167
Points
250
U

Umkonto

Senior Member
Joined Dec 27, 2018
167 250
Akili za kuambiwa changanya na zako;
Yani mwanasiasa mkongwe unatumwa ukamwambie mwenzako akajieleze na ajiuzulu.

Basi na wew unasema kama ulivyoagizwa wakati unajua kabisa katiba haisemi hivyo. Unafanya hivyo kumfurahisha aliyekutuma, lakini mwisho wa siku wew ndiyo unaonekana mjinga, mwenzako yupo nyuma anasikilizia.

Na wew ndiyo kiongozi wa chombo cha kutunga sheria halafu unahamasisha viongozi wavunje sheria. Du!

Nilitegemea ungesema labda; "Tunakushukuru CAG umetupa changamoto, tunakuahidi tutazifanyia kazi"

Kazi mojawapo ya bunge, ni kuisimamia serikali, sasa CAG kawarahisishia njia za kuisimamia serikali, nyie mnataka akajieleze kwa jiwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa, CAG aende kwa jiwe kufanya nini? Watanzania siyo wajinga kihivyo.Sent using Jamii Forums mobile app
 
E

emalau

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Messages
2,285
Points
2,000
E

emalau

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2009
2,285 2,000
Kwa jicho pana Rais yupo nyuma ya Spika.


Magufuli hapendi kukosolewa wote mnajua ya Lissu, wote mnajua ya Wapinzani leo, wote mnajua kilichompata msajili wa hazina alipotoa maoni ya wazi clouds 360 kuwa kuweka fedha za umma bank kuu kutapunguza mzunguko wa fedha na si kosa kisheria kuweka katika mabenki ya kawaida, aliliwa kichwa.
Dumelang
Nakumbuka hii interview niliiangalia live, jamaa alikuwa 100% correct, namba tunaoisoma sasa
 
ichumu lya

ichumu lya

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2016
Messages
1,213
Points
2,000
Age
49
ichumu lya

ichumu lya

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2016
1,213 2,000
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.
Ndugai sio mwanasiasa ni kiraza tu. Mimi nijuavyo mwanasiasa ujibu hoja kwa sio vitisho na kujificha kwenye Dora.

Ata ivyo sishangai kuona Mwenyekiti wa ccm kujificha kwenye jeshi maana ata yeye sio mwanasiasa so..Wanaaiasa wanasoma namba sio wa Upinzani tu ata wa ccm wanajutia maamuzi yao ya kipumbavu. Hakuna aliye salama wote ni vilio na kusaga meno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
46,414
Points
2,000
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
46,414 2,000
Kiufupi Ndungai hajitambui.
Na elimu yake haijamsaidia sana. Au labda anajitoa ufahamu ili kiutetea serikali
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
18,745
Points
2,000
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
18,745 2,000
Kama hadi sasa hivi Magufuli amenyamazia jambo hili basi ujue kuna kitu behind the scene. Si bure anyamaze
Kama ambavyo MSUKUMA alisema bungeni kuhusu mshahara wa LISU, la CAG nalo linakwenda kuingizwa kwenye mjadala kama lile… INGAWA WANAKOSEAGA KUJUA KAMA WANARUHUSIWA KISHERIA AU LA.... Maana nikiangalia la mshahara wa LISU, waliacha kumlipa, akawapa 14 days, wakasalimu amri… Tukamwona tu SPIKA akisema washamlipa, labda kuchelewa kutokane na mifumo ya ulipaji… UTADHANI SI YULE ALOIYESEMA KINYUME KABLA...!!!

Ukiangalia majibu ya CAG tangu mwanzo, utagundua kuwa anafanya REFERENCE kwenye katiba kwa kiasi kikubwa sana… NASHANGAA HUYU MSIMAMIZI WA WATUMGA SHERIA ANASHINDWA KULIONA HILO....
 
sengobad

sengobad

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2017
Messages
1,625
Points
2,000
sengobad

sengobad

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2017
1,625 2,000
Ndio maana katika taaluma mbali mbali kuna kamusi zao.
Utasikia dictionary of medicine, dictionary of geography na kadhalika.
Sasa shida nchi hii kila kituni siasa kuanzia mpira mpaka mahesabu.
Ni shida kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Najiuliza huo ushauri alioutoa jana kwann hakuutoa toka mwanzo, hiv spika kama naogopa hivyo rais eti ameguswa je ataweza kumsimamia serikali yake rais,na kwann rais mwenyewe asimtake cag ajieleze kwake.
 
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
11,397
Points
2,000
Mystery

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
11,397 2,000
Kuna kitu tunachokiita check and balance, ambapo uwepo wao mihimili yote mitatu ni muhimu katika kuleta "good governance"

Hata hivyo kila mhimili unafanya kitu tunachokiita "watchdog" kwa wenziwe

Inaonekana kwenye nchi hii chini ya utawala wa awamu ya 5, mhimili. wa serikali "umegoma" kufanyiwa watchdog na hiyo mihimili mingine 2, na mhimili huo wa Executive unajifanya kuwa ndiyo Superior wa mhimili yote hiyo na hapo ndipo penye kiini cha tatizo lenyewe.

Mpaka hapo huo mhimili wa Executive utakapojishusha na kujiona upo sawasawa na hiyo mihimili mingine miwili, ndipo tutakapokuwa,tume-solve tatizo
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
18,745
Points
2,000
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
18,745 2,000
Ok, Rais ni sehemu ya bunge….. kwa hiyo bunge likionyesha udhaifu kwenye jambo Fulani, lisiambiwe kwamba ni dhaifu kwa vile raisi nisehemu ya bunge?

Nisichoelewa ni kwamba, uwepo wa raisi kama sehemu ya bunge, kunafuta bunge kuitwa dhaifu endapo watakuwa na udhaifu kwenye jambo fulani?
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
18,745
Points
2,000
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
18,745 2,000
Kuna kitu tunachokiita check and balance, ambapo uwepo wao mihimili yote mitatu ni muhimu katika kuleta "good governance"

Hata hivyo kila mhimili unafanya kitu tunachokiita "watchdog" kwa wenziwe

Inaonekana kwenye nchi hii chini ya utawala wa awamu ya 5, mhimili. wa serikali "umegoma" kufanyiwa watchdog na hiyo mihimili mingine 2, na mhimili huo wa Executive unajifanya kuwa ndiyo Superior wa mhimili yote hiyo na hapo ndipo penye kiini cha tatizo lenyewe.

Mpaka hapo huo mhimili wa Executive utakapojishusha na kujiona upo sawasawa na hiyo mihimili mingine miwili, ndipo tutakapokuwa,tume-solve tatizo
Na jiwe alishasema… mhimili wake una miziz mirefu … Na JOBU kasema, ukiwa unalishwa hutakiwi kumsema anayekulisha...
 
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
12,556
Points
2,000
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
12,556 2,000
Hii mechi bado mbichi, mm naenda kukojoa narudi sasa hv...!! So that means CAG is a boss of his own, untouchable.. yaani yeye ngangariiiiiiiii, alafu Bunge dhaifuuu, ndio mnataka kusema hivyo sio?
 
K

Kasegela

Member
Joined
Mar 24, 2019
Messages
33
Points
125
K

Kasegela

Member
Joined Mar 24, 2019
33 125
Badala ya Ngugai kusononeshwa na matumizi mabata ya fedha,yeye kaumizwa na neno dhaifu.

Badala ya kuhoja zilipo Bil 800 ambazo hazipo kwenye mahesabu,yeye kakazana na kuumizwa kuitwa dhaifu

Badala ya kuumizwa na Matumizi yasiyoidhinishwa na bunge eti kaumizwa na kuitwa dhaifu.

Wito kwa watanzania,ndugai ajiuzulu ili kulikomboa bunge letu.

Ndugai kwa sasa hana Moral Authority ya kuendelea kuwa Spika.

Rais anapinga ufusadi,na ndio maana kampuuza ndugai kwa kupeleka ripoti bungeni.

Rais hapendi wizi,ndio maana kila mara anatumbua,halafu mtu anaemsaidia Rais kuona panapovuja etu ndugai hamtaki.

Ndugai anataka CAG atakaekuwa na tabia kama ndugai,CAG atakaeficha ukweli ili kuwafurahisha wanaomlipa.

Ndugai anathubutu kumfananisha Prof aliebobobea na anaeamini na umoja wa mataifa,halafu anafananushwa na Mbwa?

Au ugonjwa wake umeanza kupanda?
Ndugai must go.
Tanzania tunaheshimika sana,ndugai apumzuke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M

Msengapavi

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2008
Messages
7,124
Points
2,000
M

Msengapavi

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2008
7,124 2,000
Ndugai ni mouthpiece ya Jiwe, wanachofanya ni harassment kwa CAG ili ajiuzulu.
Jiwe ni mwizi wa fedha za umma na CAG ni mlinzi, sasa anataka mlinzi aondolewe.
Duh! umetumia maneno makali lakini kaama ni ukweli ni poa sana! wacha wanaoumia waumie!
 

Forum statistics

Threads 1,285,009
Members 494,369
Posts 30,847,189
Top