CAG Mstaafu Utouh Asema Fedha Za Escrow Zirudishwe

CAG Mstaafu Utouh Asema Fedha Za Escrow Zirudishwe

Siwezi kuipitia hotuba ya mnafiki na muongo ambaye anawapinga hata wataalamu ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewateua kisha wanampa ripoti naye anaipinga ili tu afiche dhambi zake kubwa za ufisadi na wale wanaomhusu kwa karibu.

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha fedha zake zilizokuwepo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zinarudi kama ilivyokuwa kwa zile za EPA. - See more at: Raia Mwema - Utouh: Za EPA zilirudi, za Escrow zirudi

Ukiwa muongo unatakiwa uwe na kumbukumbu, ulijuwaje kama "anawapinga wataalam wake" kama hujapitia hotuba yake? au umezuwa tu kichwani kwako kama kawaida yako?

Halafu umerudia kuutia uongo wako (huo uliojiwekea nyekundu) kinywani mwa Utuoh! unasikitisha sana, kwanini huuweki ukweli ambao ni huu hapa:

"Ushauri wangu ni kwamba uchunguzi unatakiwa ufanyike na wale watakaobainika kufanya wizi basi warudishe fedha walizoiba na halafu wapelekwe mahakamani".


Hivi uongo unakusaidia nini? kumwangusha Kikwete? kwi kwi kwi teh teh teh. Too late.
 
Kumbe hata kusoma hujui!? pole zako nyingi. Nimekuwekea tena hapa, acha kubwata kama mbwa koko.
kupitia kundi la mafisadi wenzake wenyewe walijiita wana mtandao wakakusanya pesa chungu nzima kwa mafisadi nchini

Naona wewe kusoma ndiyo hujuwi, si nimekwambia hapo juu naona na wewe sifa hizo unazo, au wewe si mwanamtandao?

Walikubwaga nini, ndiyo hasira zako unazimalizia hapa kwa kuzuwa uongo wa kila aina kuhusu Kikwete?
 
hahahahaha lol!!!! sasa naona unabwabwaja ajuza. Kwa taarifa yako huwa sikurupuki ninachoandika hapa kama ufanyavyo wewe. Ukishapewa ubwabwa na bahasha iliyotuna basi huandika pumba tupu ambazo hazina uthibitisho wowote. Unazidi kujidhalilisha katika kumtetea Kikwete mtu ambaye credibility yake nchini ni SIFURI imefika hata anashinikizwa na watendaji wake wa chini wa chama chenu cha wahuni kwamba Mawaziri fulani na fulani ni mizigo waondoe naye anawaondoa na kuweka wengine, lakini utendaji bado uko pale pale sifuri, cha kushangaza wakati Nape na Kinana wakiona mawaziri mizigo yeye Kikwete na washauri wake hawalioni hili!!! Ni aibu kubwa kwa nchi yetu kuwa na kiongozi kama huyu.

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha fedha zake zilizokuwepo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zinarudi kama ilivyokuwa kwa zile za EPA. - See more at: Raia Mwema - Utouh: Za EPA zilirudi, za Escrow zirudi

Ukiwa muongo unatakiwa uwe na kumbukumbu, ulijuwaje kama "anawapinga wataalam wake" kama hujapitia hotuba yake? au umezuwa tu kichwani kwako kama kawaida yako?

Halafu umerudia kuutia uongo wako (huo uliojiwekea nyekundu) kinywani mwa Utuoh! unasikitisha sana, kwanini huuweki ukweli ambao ni huu hapa:

"Ushauri wangu ni kwamba uchunguzi unatakiwa ufanyike na wale watakaobainika kufanya wizi basi warudishe fedha walizoiba na halafu wapelekwe mahakamani".


Hivi uongo unakusaidia nini? kumwangusha Kikwete? kwi kwi kwi teh teh teh. Too late.
 
hahahahahaha lol!!! Usione niko kwenye jukwaa hili ukadhani nataka kugombea nafasi yoyote ile ya uanasiasa la hasha. Nachukizwa tu na huyu mnafiki na chama chenu cha wahuni mnavyoiangamiza nchi kwa ufisadi wa kutisha miaka nenda miaka rudi huku mkitumia mabavu kuendelea kubaki madarakani.

Naona wewe kusoma ndiyo hujuwi, si nimekwambia hapo juu naona na wewe sifa hizo unazo, au wewe si mwanamtandao?

Walikubwaga nini, ndiyo hasira zako unazimalizia hapa kwa kuzuwa uongo wa kila aina kuhusu Kikwete?
 
Khe khe khe khe CAG anasema pesa zirudishwe ina maana ni pesa za umma, fisadi Kikwete anadai pesa ni za IPTL!!!! Sasa nani wa kuaminiwa kati ya hawa wawili? Yule aliyefanya uchunguzi wa documents husika kwa zaidi ya miezi sita au yule aliyeandikiwa email toka kwa mmoja wa wezi wa pesa hizo kwamba pesa ni za IPTL na si za umma!? Hii ngoma bado mbichi sana.
BAK you Kikwete very well kuendelea kuumiza kichwa kwa ajili yake tunajiongezea stress za bure unakumbuka habari za katiba? Kikwete ndivyo alivyo haiba yake ndio hiyo, lakini kibaya zaidi na ambacho hakiwezi kuvumilika kwa jinsi yoyote ile yeye binafsi, familia yake na chama chake ni wanufaikaji wa pesa za escrow! Watabisha leo, watakana kesho lakini ipo siku ukweli huu utawekwa wazi!! Nasema IPO siku
Kwahiyo anapotumia nguvu nyingi kutetea uchotwaji wa zile pesa he knows exactly what he is doing! La sivyo kama kiongozi mkuu wa kaya mwenye uchungu wa kweli na wananchi wake asingesita kuchukua hatua tena kali kwa watuhumiwa wote
After all alikuwa keshatafuniwa kila kitu na mamlaka zinazotambulika kama bunge/PAC, PCCB na CAG, sasa kujiumauma kote kule kwenye kutoa maamuzi stahiki kulikuwa kwanini????
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hahahaha ndio kazi ya kidumu sarakasi nyingi kweli kweli delete futa ccm
 
hahahahahaha lol!!! Usione niko kwenye jukwaa hili ukadhani nataka kugombea nafasi yoyote ile ya uanasiasa la hasha. Nachukizwa tu na huyu mnafiki na chama chenu cha wahuni mnavyoiangamiza nchi kwa ufisadi wa kutisha miaka nenda miaka rudi huku mkitumia mabavu kuendelea kubaki madarakani.
FaizaFoxy ni die hard wa kikwete ana mapenzi yaliyopitiliza kwake mpaka kuna wakati nikamuuliza kama ana vinasaba na huyu ndugu! Hakuwahi kunijibu
 
Last edited by a moderator:
Mpumbavu ni wewe uliyekuja na uongo wa kumzulia Utuoh, nimeandika hapo ukweli wa alichokisema, kimekukera unakuja na huku povu linakutoka.

PCCB kesi moja watachunguza hata mara mia, si kitu cha papo kwa papo. Wewe kama unasema wamemaliza uchunguzi tueleze huo uchunguzi wa PCCB uko wapi?

Unatuletea habari za siku 20 nyuma? Kikwete juzi kasema alipoondoka kapewa ripoti ya CAG akaamuru wapewe PCCB waichunguze. Sasa unafikiri PCCB na kesi kama hiyo wanachunguza siku 4 tu?

Hebu kuweni wakweli wa nafsi zenu hizi chuki zenu kwa Kikwete zisiwafikishe mpaka mkausahau utu, mnaanza kudanganyana, kuzuwa. Yote kwanini? kwa sababu kawafungia mianya yenu ya uchotaji?

Uongo hausaidii kitu na nchi haziendeshwi kwa uongo.
Hebu tuondolee janaba hapa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Unapomtaja Dr Mgimwa unanikumbusha ile kauli ya naibu wake ambaye ndiye waziri wa fedha wa sasa Saada Mkuya. Wakati wa msiba ule kwa uchungu na kwa vile watu wanasema akina mama hawana "vifua" alijikuta akitamka maneno haya kwa uchungu "wamemuondoa Mgimwa kweli! Namuachia MUNGU". Bahati mbaya sana maneno yale yalidakwa na kamera za TV.
Ndio maana Mnyika majuzi alipolianzisha Bungeni kuwa iundwe tume kuchunguza kuna watu walitoa macho kama mijusi iliyobanwa na mlango.

Damu ya mgimwa RIP itakua juu yao majnuni hawa
 
Wacha kuzuwa wewe, hiyo miradi ulimpa wewe?

Hao Watanzania wengi ni wewe na ukawa? hivi huu uongo wenu unawasaidia nini? Tanzania haiendeshwi kwa uongo uongo.

Kikwete mnamchukia kawazibia mengi sana. Kikwete ndiye Rais pekee wa Tanzania aliyethubutu kuwssweka ndani mpaka mawaziri wenye nguvi kabisa. Kikwete ndiye Rais pekee aliweza kuwasweka ndani mpaka ma god father waliozitisha serikali zote za kabala yake. Msofe yuko wapi? Alex Masawe yuko wapi?

Kikwete huyo huyo ndiyo aliyewea kufanya mpaka leo manijuwa EPA ni nini na leo hii mnaijuwa escrow ni nini?

Juzi kawapa vijembe vyenu pale kidiplomasia, kawauliza isingekuwa CCM mngeyaona haya> CCM wangetaka au wangekuwa wanafaidika na haya hata kwenye kamati yasingefika, kwani kwenye hiyo kamati CCM ni wengi kuliko UKAWA, umesahau?

Ile alikuwa anawapasha kuwa ni kazi yake ile kama Mwenyekiti wa CCM. Kumbuka hilo.

Siyo mnakuja hapa na kumzulia Utuoh, Utuoh anasema uchunguzi ufanyike kama kuna wizi warudishe fedha na halafu wafikishwe mahakamani, sasa sema kauli hiyo ya Utuoh na kauli za Kikwete jusi kwenye hotuba yake zinatofautiana nini?

Mbona hamsemi Utuoh alipowashushuwa mnapoongelea ya EPA? kuwa ooh Kikwete kawasamehe! Utuoh kaweka wazi kuwa huo ulikuwa ushauri wake na hakuna aliyesamehewa nyie bado mmekaa mnadanganya wa watu.

Ni wapi aliposema hakubalini na bunge? wacha ujing huo. Maazimio yote manane ya bunge kayafanyia kazi na kaainisha alichokifanya na hatua zilizochukuliwa na zitazochukuliwa.

Ulitaka nini zaidi? afukuze watu hovyo hata wasio na hatia? Ulitaka ataifishe mtambo wa PAP azidi kuitia nchi hasara za makesi na kuwekewa vikwazo kama alivyofanyiwa Nyerere? akaiacha hii nchi kuwa masikini wa mwisho duniani baada ya blunder yake ya kutaifisha?

Kikwete hakurupuki hata kidogo.

Safari hii mmeshikwa pabaya nyimbo zenu za kudandia zime-flop. Hamna jipya.

Ni kweli kabisa bila CCM haya yote tusingeyajua na yasingetokea lkn kwa sababu hii ni Tanzania chini ya JK ndiyo maana yametokea.
Only in Tanzania.
 
Msomeni vizuri wacheni uongo! Utuoh kasema "Ushauri wangu ni kwamba uchunguzi unatakiwa ufanyike na wale watakaobainika kufanya wizi basi warudishe fedha walizoiba na halafu wapelekwe mahakamani".

Ina maana ipi hapo? kwanza, uchunguzi haujakamilika. Pili, hakuna aliyebainika mpaka sasa kafanya wizi.
kwa mujibu wa jk kasema pesa za escrow hazikuwa za umma! Utafanyaje uchunguzi kwenye pesa ambazo si za umma? Jk amewasaliti watanzania, badala ya kutetea mali za umma anatetea iptl.
 
Jk ameusaliti umma wa watanzania, badala ya kutetea rasilimali za umma yeye ameungana na mafisadi.
 
Kweli Kumtetea mwizi kunahitaji ujasiri uso mfano...ama uwe mwenza au mshikaji. Leo ajuza FaizaFoxy habanduki; kula, kunya na kulala humu humu jamvini hata kama jua linachomoza.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Msomeni vizuri wacheni uongo! Utuoh kasema "Ushauri wangu ni kwamba uchunguzi unatakiwa ufanyike na wale watakaobainika kufanya wizi basi warudishe fedha walizoiba na halafu wapelekwe mahakamani".

Ina maana ipi hapo? kwanza, uchunguzi haujakamilika. Pili, hakuna aliyebainika mpaka sasa kafanya wizi.
lf that is the case,hakukua na sababu ya kusema pesa si za umma mpaka uchunguz uishe,hakukua na sababu ya kumwacha mwongo ofsin,alipaswa asimamishwe kwanza,
 
Inasikitisha sana, mpaka wahisani (wadau wa maendeleo) wanasitisha misaada yao kushinikiza !
 
Watu msokuwa na ajira za maana mna shida sana, tangu asubuhi ni porojo tu za siasa

wewe ndo huna kaz,ni kwel kwanin cag astaafu hajamalza kaz? Mbona said mwema na askari wengne waliongezewa muda?
 
Faiza Fox

Wacha uongo watu wamchukie Kikwete kwa lipi? Yeye muda wake wa urais unakwisha sasa kwa nini wamchukie. Kikwete alipoingia madarakani kama rais hakuwa na utajiri wowote ule sasa hivi ana miradi binafsi mingapi? Ana shares kibao kwa kampuni inayochimba dhahabu kule Mwanza, Je, alinunua kihalali au alihongwa tu? Amewapa ndugu zake pesa za escrow kwa ubadhirifu, Je, hayo yote unaona ni sawa? Kweli JK ni ndugu yako wa karibu sana lakini unapokuwa rais huwi rais wa ndugu zako unakuwa rais wa Watanzania. Hivi sasa Watanzania wengi wanapenda aitishe uchaguzi hata kesho, si hakubaliani na Bunge alivunje basi kwa Mujibu wa Katiba. Mbona anapata kigugumizi kuilinda katiba iliyomuweka pale kama yeye yuko msafi? Hatuwezi kuwa na chuki na kiongozi aliyejipaka mavi usoni na yeye anachekelea anafikiri hayo ni manukato.
rais msanii siyo kiongozi.....analeta mambo ya kujuana tu mpaka ikulu inapigwa vidole vys mat.....k
bora jk aondoke tu tumemchoka
wewe endelea kutetea ujinga ila weee ukiwa na shida hupaswi kusaidiwa kabisa
 
Hio makala ilitoka kabla ya hutuba ya profesa dokta jk kwa wazee wa daslama
 
Wacheni uongo kucheza na maneno, Utuoh kasema "Ushauri wangu ni kwamba uchunguzi unatakiwa ufanyike na wale watakaobainika kufanya wizi basi warudishe fedha walizoiba na halafu wapelekwe mahakamani".

Ina maana ipi hapo? kwanza, uchunguzi haujakamilika. Pili, hakuna aliyebainika mpaka sasa kafanya wizi.

Watu waongo sana, ndiyo maana hawakubandika na wameweka link tu, wanajua wengi hawatoenda kuisoma.

Wacheni uongo. Hauwasaidii kitu, tuko macho.

384_utouh.jpg


Utouh: Za EPA zilirudi, za Escrow zirudi
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovick Utouh, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha fedha zake zilizokuwepo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zinarudi kama ilivyokuwa kwa zile za EPA.

Katika mahojiano yake na Raia Mwema yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii, Utouh alisema kama angepewa fursa ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuhusu nini cha kufanya na suala la Escrow bila shaka angemwambia ahakikishe anapata kwanza fedha zilizopotea.


"Kwanza niseme kwamba aliyetoa pendekezo kwa serikali kwamba iwabane walioiba fedha za EPA wazirudishe kwanza kabla ya kufuata mikondo ya kisheria ni mimi. Hela kurudi ni jambo la muhimu sana.

"Ushauri wangu ni kwamba uchunguzi unatakiwa ufanyike na wale watakaobainika kufanya wizi basi warudishe fedha walizoiba na halafu wapelekwe mahakamani.

"Watu wanaolalamika kuhusu wezi wa EPA wanafanya hivyo kana kwamba watu walirudisha fedha na wakaachiwa jambo ambalo si la kweli. Hela zilirudi na bado kesi zikaendelea mahakamani na zinaendelea hadi hivi leo tunavyozungumza.


"Hivi kuna tatizo gani kama mtu atarejesha fedha aliyochukua? Huyu mtu unaweza kumkuta na hatia na ukampeleka jela lakini akifika kule atakula na kulala bure kwa gharama za walipa kodi. Kama atalipa fedha alizoiba, ndizo fedha hizohizo zitatumika kumhudumia.


"Ninachosema hapa, kitu kizuri ni kipi? Kuendelea na kesi kwa miaka mingi na huku ukitumia fedha za umma kuzihudumia au angalau kushinikiza kwanza hela zilizochukuliwa zirudishwe na kesi zikaendelea kama kawaida?


"Kutaka hela zirudishwe haina maana hata kidogo ya kusamehe watuhumiwa bali maana yake ni kuhakikisha kile kilichochukuliwa kinapatikana kwanza," alisema Utouh.


Katika mahojiano hayo ambayo yamechapishwa katika ukurasa wa 12 na 13 wa gazeti hili, Utouh alisema ni sahihi kwa ripoti ya CAG kuhusu suala la Escrow kusema fedha zilizokuwepo katika akaunti ya Escrow ni za umma na pia si umma kwa vile huo ndiyo ukweli.


"Kama ulifuatilia mjadala ule wa bungeni, kitu cha kwanza ambacho kilisemwa na kipo kweli ni suala la kodi. Ndani ya fedha zilizokuwepo kwenye akaunti ya Escrow kulikuwa na kodi. Kodi ni mali ya umma. Hivyo kwenye eneo hilo la kodi, fedha za umma zipo.


"Jambo la pili lipo kwenye historia ya kuanzishwa kwa akaunti hiyo. IPTL na Tanesco walikuwa na mzozo kuhusu malipo ya capacity charge. Mgogoro ulikuwa mkubwa na wakaamua kuweka fedha za malipo hayo kwenye akaunti ya Escrow huku wakisubiri shauri lao kutoka katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro.


"Sasa, nizungumze kama mfano tu, hypothetical, kwamba IPTL walikuwa wanaichaji Tanesco shilingi 30 kwa siku. Tanesco wakaona kwamba wanalaliwa kwa gharama hizo. Wanalipa zaidi ya wanavyotakiwa kulipa.

"Wakaenda mahakamani kushitaki. Uamuzi uliotoka ni kwamba, ni kweli Tanesco wamebambikiwa hizo gharama. Inabidi gharama za capacity charge zikokotolewe upya. Sasa ofisi ya CAG haina mamlaka ya kufanya ukokotoaji huo.

"Kwa hiyo, kama ukokotoaji ungefanyika, labda tuseme IPTL ingetakiwa kutoza shilingi 20 kwa siku, maana yake ile tofauti ya shilingi 30 inayotozwa na shilingi 20 inayotakiwa kutozwa, yaani shilingi 10, ingekuwa ya Tanesco.


"Hii maana yake ni kwamba, katika kila shilingi 30 iliyokuwepo katika Escrow, ukiondoa zile za kodi, shilingi 20 zilikuwa za IPTL kwa sababu ya umeme wake iliyouza na shilingi kumi zilikuwa za Tanesco ambayo ni taasisi ya umma," alisema.
 
Back
Top Bottom