CAG ashitukia ulaji mil.775/- kila heka NSSF

CAG ashitukia ulaji mil.775/- kila heka NSSF

We acha Mkuu inauma na kusikitisha sana jinsi hawa wahuni na mafisadi wanaitafuna nchi yetu kila kukicha huku wakiendelea kukingiana kifua na kuonea vidagaa tu lakini yale mapapa na manyangumi ya ufisadi hayaguswi haya siku moja.

Mmmh mpaka mwili umenisismka
 
Inatia hasira sana hela zetu zinafujwa bila huruma,two weeks ago Nssf wametoa tangazo LA majengo yaliyo vacant yaani ni aibu,75% ya majengo hayana wapangaji na mategemeo kupata wapangaji hasa kwa usawa huu ni majaliwa,hebu fikiria ni kiasi gani cha pesa zilitumika kuyajenga,hii inaonyesha walioliongoza hili shirika walitumia elimu akhera maana huwezi kuwekeza ukiwa timamu bila kufanya study kujua uhitaji wa watu eneo husika,halafu mijingajinga unakuja humu kumtetea mpuuzi mmoja aliyetaka kuliangamiza shirika,dadadeki
Wewe una vita binafsi na Mh. DAU sio bure. Ushindwe na ulegee, pumbavu.Aliyekutuma mwambie akafie mbele.
 
CAG ashitukia ulaji mil.775/- kila eka NSSF

Comptroller General Mussa Assad hawezi kusemwa "kashtukia ulaji," kwa sababu na yeye alikuwepo kama mjumbe wa bodi ya NSSF, anayajua toka mwanzo na anakuwa implicated by default for green-lighting these massively corrupt deals.

IMG_4490.JPG

Mussa Assad akipewa zawadi na Director Dau kwa kazi nzuri aliyofanya kama board members wa NSSF

IMG_4420.JPG

Mussa Assad, wa nne kwenye mstari, akipakua ubwabwa kwenye tafrija ya N.S.S.F ambapo Director Dau aliwapongeza kwa kazi nzuri waliyofanya kusimamia shirika.

Second, Mussa Assad ameshawahi kutoa ka smokescreen report fulani kanasema amepitia hesabu za NSSF, kakuta hakuna ufisadi. Leo atatokaje aseme kashtukia ufisadi?

Third, Mussa Assad ni swahiba wa karibu wa Ramadhani Dau, hawezi kumvua nguo mwenzie wakati walikuwa wanacheka pamoja na kufunika kombe mwanaharamu wa auditing akipita.

C.A.G. amebanwa na mahesabu imebidi aya present kama yalivyo, lakini huwezi kusema kashtukia ufisadi. Waandishi wetu wanachemka kama kawaida. Wao wenyewe wamesema ni wabunge ndio wamefura wakisema "wananusa" ufisadi. Ingekuwa C.A.G. Assad "kashtukia" ufisadi wabunge "wasingenusa" ufisadi kwa sababu ungekuwa umeshaanikwa tayari na Mussa Assad.

C.A.G. Assad nae faili lake ni hati chafu, Rais anatakiwa am fire.
 
Hizi nyimbo zili flop, ma dj wanalazimisha zichezwe tu.

Hakuna jipya.
Tàtizo ni kuwa japo ufisadi ni wa dhahiri lakini wakubwa wamejitahidi kuufumbia macho nadhani kuna namna walifaidika na ufisadi huu! Haahlafu akina yahe kama fox wakaaminishwa kuwa jamaa anaandamwa kwa chuki za kidini hasa kwa sababu jamaa alikuwa anajifichia kwenye dini kwa kutoa futari!
Ukweli ni kamba wimbo huu haujawahi kutendewa haki ndio maana wimbo wenyewe (eka moja kwa sh. 777,000,000/=) unadai utendewe haki!
Inabidi MTU awe na uwezo mkubwa sana wa kujifanya hamnazo kama huyu niliyemnukuu Ambaye anaweza kusema hiyo ni bei halali ya ardhi miaka hiyo huko kigamboni (sh 775,000,000/= kwa eka) na hakuna ufisadi hapo!
Hiyo tisa, kumi ni kuwa jamaa aliyesimamia hilo mr. Uda ameonekana ndio mtu anayefaa kuiwakilisha Tanzania huko ughaibuni maana yeye ndio taswira nzuri ya Tanzania! Ukisha kumwona Uda kuwa ni Safi kiasi cha kuwa mwakillishi wetu ughaibuni unakosa uhalali wa kutumbua yeyote, maana kama Uda ni safi basi waliobaki wote ni malaika!
 
Have you any knowledge ever of what mega real estate development investments are?
 
CAG ashitukia ulaji mil.775/- kila eka NSSF

Kufuatia taarifa hiyo, wabunge kupitia Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) walikuja juu na kuubana uongozi wa NSSF, wakitaka maelezo ya kina kuhusiana na suala hilo walilodai lina harufu ya ufisadi.

Wakati ikipitia taarifa ya CAG, kamati hiyo, chini ya Mwenyekiti wake, Naghenjwa Kaboyoka, ilibaini kuwa katika mradi wa NSSF kuendeleza mji wa kisasa wa Kigamboni jijini Dar es Salaam ambao shirika hilo limeingia ubia na taasisi nyingine, thamani ya kiwanja kimoja iliyowekwa ni Sh. milioni 800 wakati thamani halisi ni Sh. milioni 25, hivyo kuwapo na malipo ya ziada ya Sh. milioni 775 kwa kila kiwanja.

PAC ilifichua ulaji huo wakati ikiibana NSSF kwa kutaka ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali za ukaguzi zilizoainishwa na CAG katika mwaka wa fedha 2014/15.

Mwenyekiti wa PAC, Kaboyoka, alisema kuwa watalieleza Bunge kuhusu harufu ya ufisadi katika mradi huo wa NSSF katika kuendeleza mji wa Kigamboni.

Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), alidai mradi huo umegubikwa na 'uchafu' kutokana na kile kilichofanyika .

Mbunge wa Magomeni, Jamal Kassim Ali (CCM), alisema kuna taarifa kwamba mbia, ambaye ni kampuni ya Azimio Housing Estates, kuwa anataka kukopa tena wakati kuna fedha za uwekezaji hazijaingizwa kwenye mradi.

Ali alidai pia kuwa, kuna mgongano wa maslahi kutokana na kampuni hiyo kuonekana ikipewa kazi nyingi na NSSF.

Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly, alisema taarifa zao zinaonyesha mbia huyo yupo tayari kuingiza fedha kwenye uwekezaji huo lakini anataka akope, hivyo kuna uwezekano wa NSSF kupoteza Sh. bilioni 270 ambazo zimeingizwa kwenye uwekezaji huo kama isipokuwa makini kuangalia namna ya kuzirudisha.

Katika ripoti ya CAG ya 2014/15, inaelezwa kuwa NSSF iliingia ubia na kampuni hiyo na kuanzisha kampuni maalumu kwa jina la Hifadhi Builders Limited.

Ilielezwa kuwa katika mkataba huo wa mradi wa Kigamboni, Azimio Housing Estates inatakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi zilizopo Kigamboni lakini baada ya tathmini, PAC imebaini zipo ekari 3,503 tu.

Katika ubia huo, NSSF inamiliki asilimia 45 ya hisa wakati Azimio Housing Estates inamiliki asilimia 55 ya hisa na jumla ya gharama za mradi ni dola za Marekani milioni 653.44.

Aidha, inaelezwa kuwa utaratibu wa uchangiaji mtaji ni NSSF kutoa fedha kwa asilimia 45 ya gharama za mradi na Azimio kutoa fedha zenye thamani ya asilimia 35 ya gharama za mradi pamoja na ardhi ambayo itathaminishwa kuwa asilimia 20 ya gharama za mradi.

Hata hivyo, wajumbe wa PAC walishangazwa na uthamini uliofanywa kwenye ardhi wakieleza kuwa gharama imeonekana ni kubwa kuliko gharama halisi.

Ripoti ya CAG inaeleza kuwa katika makubaliano ya usitishwaji, kiasi cha Sh. bilioni 43.9 ilicholipwa Azimio na shirika ni sehemu ya ada ya ushauri ambayo inabadilishwa kuwa mkopo utakaorejeshwa na kampuni kupitia sehemu ya mauzo ya nyumba katika mradi wa Dege ndani ya miaka mitatu, kwa riba ya asilimia tatu kwa mwaka.

Akijibu hoja za wabunge, Mkurugenzi wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, alisema utekelezaji wa mradi wa Dege ulisimama tangu Februari mwaka huu kutokana na mwekezaji kutokuwa na fedha huku NSSF tayari ikiwa imeshaingiza Sh. bilioni 270.

Hata hivyo, alisema kuna ukaguzi maalumu unafanyika kwenye miradi yote ya NSSF ukiwamo huo wa Kigamboni.

“Tukitoka kwenye ubia huu, tunaweza kupoteza fedha hizo… tupo makini kuhakikisha mwekezaji huyo (Azimio) anarejesha fedha hizo,” alisema Mkurugenzi huyo.

Prof. Kahyarara alikiri Azimio kupeleka barua kwa NSSF ikitaka kukopa na ilikataliwa kupewa mkopo huo kwa sababu inadaiwa na haiwezi kukopeshwa tena.

Alisema sehemu kubwa ya ardhi imenunuliwa na NSSF kwa bei kubwa tofauti na uhalisia na kuna uchunguzi unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato (TRA) huku akisema hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi wale wote waliohusika na mkataba wa mradi huo.

UTATA MIKOPO SACCOS
Katika hatua nyingine, PAC imemuagiza CAG kufanya ukaguzi maalumu wa mikopo yote iliyotolewa na NSSF baada ya kubaini kuwa Saccos ya Bumbuli Development Corporation imepatiwa mkopo usio wa kawaida wa Sh. bilioni 2.4 ndani ya mwaka mmoja.

Mwenyekiti wa PAC, Kaboyoka, alisema juzi kuwa kamati yake ilishtushwa na kumuagiza CAG kufanya ukaguzi maalumu wa fedha za Saccos ya Bumbuli.

Alisema suala la Saccos ya Bumbuli kupatiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha, limewashtua wajumbe wa kamati hiyo na kujiuliza imekuwaje ipate fedha nyingi katika kipindi hicho kifupi huku ikipewa tena fedha nyingine na kufanya deni kufikia Sh. bilioni 2.4 ndani ya mwaka mmoja.

“CAG afanye ukaguzi kwenye Saccos maana haijulikani kama fedha walizopewa awali zimerudishwa au la,” alisema Mwenyekiti huyo.

Kaboyoka aliongeza kuwa maelekezo mengine yatatolewa bungeni kwa mujibu wa Kanuni ya 117(10) katika kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016, inayoipa mamlaka kamati hiyo kuwasilisha taarifa bungeni kuhusu hesabu za serikali.

Awali, wakati wakichangia mapitio ya hesabu za NSSF, wajumbe wa kamati hiyo walionyesha kushtushwa na jinsi Saccos hiyo ilivyopewa mabilioni ya shilingi kwa zaidi ya mara moja ndani ya muda huo mfupi.

Mbunge wa Viti maalumu, Tunza Malapo (Chadema), alihoji kama NSSF imefanya uhakiki na kujiridhisha juu ya uwapo wa Saccos hiyo ya Bumbuli.

Mbunge wa Kilindi, Omar Kigua (CCM), alihoji vigezo vilivyotumika mpaka Saccos moja kupewa mkopo mara tatu ndani ya mwaka mmoja.

Alisema NSSF imetoa mikopo kwa Saccos tisa, kwa kiasi kinachozidi asilimia 50 ya thamani ya mali za Saccoss, husika kinyume cha sera ya kukopesha ya shirika na limeomba kiasi ambacho hakikustahili kutolewa.

Katika ripoti ya CAG, mbali na Bumbuli, Saccos zingine zilizopatiwa fedha nyingi kinyume cha utaratibu ni Korongo Amcos Saccos, UMMA Saccos, SBC Saccos Ltd, Hekima Saccos, Ukombozi Saccos Ltd, Uzinza Saccos Ltd, Harbour Saccos na Umoja Saccos.

Akizungumzia suala hilo la Saccos, Mkurugenzi wa NSSF, Prof. Kahyarara, alisema ukaguzi wa awali uliofanywa, umebaini ni kweli kuna Saccos zilikuwa hazionekani huku kwenye vitabu zikiorodheshwa kuwa zimekopeshwa.

Aidha, alisema kuna wadaiwa wengine wamejitokeza na kupeleka fedha wenyewe, na ambao awali walikuwa hawajulikani.

Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Prof. Samwel Wangwe, alisema hivi sasa bodi imesimamisha mikopo kwa Saccos hadi uchunguzi ukamilike na baada ya hapo utawekwa utaratibu mpya wa utoaji mikopo.

Ardhi hiyohiyo ikiwa chini ya umiliki wa jadi, wananchi, wanasema haina thamani ila minazi migomba na mihogo na mazao yake mengine kama yapo; na kwamba eti ardhi yote ni mali ya serikali! Wakishaichukua kwa fidia kiduchu ya mihogo na miembe nk., inayokadiriwa na 'professional valuers' ambao ni wa serikali hiyihiyo inayomyang'anya mwananchi ardhi yake; thamani ya ardhi hiyo hupanda ghafla na kuwa mamilioni/bilioni ya T. Shs.!

Hivi tuna wataalamu wa kweli wa masuala ya uthamini - valuers - wa ardhi? Au tuna watu wanaojikuna wenyewe na kucheka wenyewe kwa mujibu wa mpunga au pilau iliyopo?

Au je! hakuna empirical fomular ya ku-determine thamani ya ardhi au kitu chochote?
Na hili neno 'mwananchi' maana yake ni nini hasa! kama nchi/ardhi yenyewe ni mali ya serikali?
Sitaki kusikia eti wananchi wanamiliki ardhi kupitia serikali eti kwakuwa serikali ni ya wananchi!

Ardhi ni kitu kingine na serikali ni kitu kingine kwasababu ardhi inaonekana, ni kitu tangible. Kinashikika na kugawanyika. Ideally kila mwananchi anastahili kuwa na kipande chake cha ardhi. Lakini hatuwezi kugawana serikali ili kila mtu awe na kipande chake!

Kwahiyo jukumu la serikali ni kusimamia haki katika ugawanaji wa ardhi ili kila anayestahili, kama ni kwa jadi au kwa pesa yake halali, aweze kunufaika na thamani halisi ya ardhi yake.

Wazaramo wana nini cha kujivunia katika magorofa yaliyopo ndani ya ardhi yao ya asili, jiji la Dar ambako kila kukicha wanasogezwa mbali zaidi kupisha wenye nguvu? Ardhi waliyopokonywa kwa kulazimika kuwauzia matajiri/wenye mitaji, au kuchukuliwa na serikali kwa fidia kiduchu ndiyo hiyo inanadiwa sehemu kama Kigamboni kwa mabilioni ya shilingi!

Msiniambie naleta ukabila hapa, kwani kuna Mtanzania asiye na kabila? Hamuoni kwamba kuna makabila mengine yana uelewa mkubwa wa thamani ya ardhi mengine hayana? Na bila kulinda haki za ardhi za asili kwa wanyonge hamuoni kwamba sera zenu zinasaidia wanyonge kupoteza ardhi zao za asili ambazo zingekuwa mtaji wao kiuchumi?

Bila sera zinazolinda haki za ardhi za asili za jamii zisizo na mitaji; jamii hizo zitaendelea kupoteza ardhi ama kwa kulazimika kuuza kwa wenye nguvu au kwa kunyanganywa na serikali kupitia miradi kama Kigamboni na CDA kule Dodoma. Kwani ukoloni Berlin Conference na utumwa ulithamini ardhi ya wananchi?

Sasa; katika hali kama hii ya wananchi kuyang'anywa ardhi chini ya sera za Berlin conference, kutakuwa na usawa, haki, na amani mbele ya safari?
 
Kimahesabu ya wanaowekeza kwenye majengo, ukipata occupancy rate ya 50% kwa kodi uliyojipangia hiyo ni win win situation. 20% ni break even.

Kama uliyosema ni kweli basi wamefanya vizuri sana tena sana.
Well, sio kwa NSSF. Nafanya nao kazi na majengo yao msh na Arusha break even ni ndoto. Too unrealistic construction figures
 
Huyu mjinga alivyokuwa anafanya utafikiri alitumia ubongo wa marehemu maana anawekeza na hujui nani watahitaji,jengo LA moshi na kigoma miaka 20 hayatajaa,jpm funga hawa takataka
Mifuko yote uwekezaji wa kwenye majengo ilikua ni njia kupiga tu. Hilo la moshi nenda skyscrapercity.com uone ndani lilivyo vibaya.

Too much obstructions in way of ngazi, ramps, lifts, escalators, balustrades zinang'aa za kichina, mavyumba hayana formula basi ili mradi jengo lina mavioo watu wanavutiwa.
 
Well, sio kwa NSSF. Nafanya nao kazi na majengo yao msh na Arusha break even ni ndoto. Too unrealistic construction figures

Hapo ndipo unapoonyesha ufinyu wako wa "real estate investment". Kwa Tanzania, kuwa na hilo jengo tu ina maana tayari una faida.

20% ya break even ninayoiongelea ni ile ya running expenses na si ile ya gharama za kujengea. Upo hapo ulipo?
 
Have you any knowledge ever of what mega real estate development investments are?
Acha kukariri upuuzi upuuzi tu usio na kichwa wala mabega...umezielewa nondo alizokushushia jamaa hapo juu lkn???wapigaji siku zote huwa lzm watafute lugha tamu ili kuwaweka sawa maboya km nyie kina Faiza Focks mnaodandiaga train kwa mbele huku masaburi yote mkiyaacha nje...kushadadia lugha msizozijua kumbe mnaliwa naniliu
 
Ardhi hiyohiyo ikiwa chini ya umiliki wa jadi, wananchi, wanasema haina thamani ila minazi migomba na mihogo na mazao yake mengine kama yapo; na kwamba eti ardhi yote ni mali ya serikali! Wakishaichukua kwa fidia kiduchu ya mihogo na miembe nk., inayokadiriwa na 'professional valuers' ambao ni wa serikali hiyihiyo inayomyang'anya mwananchi ardhi yake; thamani ya ardhi hiyo hupanda ghafla na kuwa mamilioni/bilioni ya T. Shs.!

Hivi tuna wataalamu wa kweli wa masuala ya uthamini - valuers - wa ardhi? Au tuna watu wanaojikuna wenyewe na kucheka wenyewe kwa mujibu wa mpunga au pilau iliyopo?

Au je! hakuna empirical fomular ya ku-determine thamani ya ardhi au kitu chochote?
Na hili neno 'mwananchi' maana yake ni nini hasa! kama nchi/ardhi yenyewe ni mali ya serikali?
Sitaki kusikia eti wananchi wanamiliki ardhi kupitia serikali eti kwakuwa serikali ni ya wananchi!

Ardhi ni kitu kingine na serikali ni kitu kingine kwasababu ardhi inaonekana, ni kitu tangible. Kinashikika na kugawanyika. Ideally kila mwananchi anastahili kuwa na kipande chake cha ardhi. Lakini hatuwezi kugawana serikali ili kila mtu awe na kipande chake!

Kwahiyo jukumu la serikali ni kusimamia haki katika ugawanaji wa ardhi ili kila anayestahili, kama ni kwa jadi au kwa pesa yake halali, aweze kunufaika na thamani halisi ya ardhi yake.

Wazaramo wana nini cha kujivunia katika magorofa yaliyopo ndani ya ardhi yao ya asili, jiji la Dar ambako kila kukicha wanasogezwa mbali zaidi kupisha wenye nguvu? Ardhi waliyopokonywa kwa kulazimika kuwauzia matajiri/wenye mitaji, au kuchukuliwa na serikali kwa fidia kiduchu ndiyo hiyo inanadiwa sehemu kama Kigamboni kwa mabilioni ya shilingi!

Msiniambie naleta ukabila hapa, kwani kuna Mtanzania asiye na kabila? Hamuoni kwamba kuna makabila mengine yana uelewa mkubwa wa thamani ya ardhi mengine hayana? Na bila kulinda haki za ardhi za asili kwa wanyonge hamuoni kwamba sera zenu zinasaidia wanyonge kupoteza ardhi zao za asili ambazo zingekuwa mtaji wao kiuchumi?

Bila sera zinazolinda haki za ardhi za asili za jamii zisizo na mitaji; jamii hizo zitaendelea kupoteza ardhi ama kwa kulazimika kuuza kwa wenye nguvu au kwa kunyanganywa na serikali kupitia miradi kama Kigamboni na CDA kule Dodoma. Kwani ukoloni Berlin Conference na utumwa ulithamini ardhi ya wananchi?

Sasa; katika hali kama hii ya wananchi kuyang'anywa ardhi chini ya sera za Berlin conference, kutakuwa na usawa, haki, na amani mbele ya safari?
Faiza Fuxy upo
 
Hapo ndipo unapoonyesha ufinyu wako wa "real estate investment". Kwa Tanzania, kuwa na hilo jengo tu ina maana tayari una faida.

20% ya break even ninayoiongelea ni ile ya running expenses na si ile ya gharama za kujengea. Upo hapo ulipo?
Unadhani gharama za ujenzi hazihusiani na ukadiriaji wa pango?
 
Unadhani gharama za ujenzi hazihusiani na ukadiriaji wa pango?

Tukiongelea 20% kuwa ni breakeven kutokana na kodi ya jengo jipya tunaongelea running expenses na si total construction costs.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Have you any knowledge ever of what mega real estate development investments are?
There is absolutely no justification ever for a piece of land at kigamboni which can be bought at a sky price of 775,000,000/= per acre! Usituletee na upuuzi wa mega real estate hapa! Huu ni ufisadi wa kiwango cha ibilisi! Niambie nani kigamboni alishauza kwa bei hata ya 30,000,000/= tu kwa eka? Huwezi kuamini kuna ibilisi nchi hii anayeweza kuthubutu kusema amenunua ardhi kwa bei ya milioni mia saba sabini na tano! (775,000,000) wakati wenye mfuko wanachama wa nssf wanakufa maskini! Huwezi kuamini pia kuwa nchi hii kuna mtoto wa ibilisi anayeweza kuona manunuzi hayo ni halali! Sema hadharani basi kuwa bei ya eka moja kigamboni miaka ile ilikuwa sh 775,000,000/=, naona unaogopa hata kuzitamka na kujificha kwenye lugha ya malkia ili wasikuelewe wote!
 
Pata darsa la bure bilash:

Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni

Jana Magazeti mengi yameandika kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Hasa Mradi wa Dege Beach Huko Kigamboni ambapo imeelezwa Kuwa Katika Kila Kiwanja Kimoja kati ya Viwanja 300 vilivyoko Katika hatua ya kwanza ya Mradi thamani ya Kiwanja imezidishwa Kwa zaidi ya Shilingi Milioni 775. Ikielezwa Kuwa thamani ya Kila Kiwanja Ni Shilingi Milioni 25 Tofauti na Milioni 800 ambazo NSSF imenunua Kwa Kila Kiwanja Kimoja Kwa Mujibu wa Mkataba kati yake Na Kampuni ya Azimio.

Taarifa Hizi ni za Uongo. Ukweli ni Kuwa NSSF haikununua Ardhi eneo la Dege Beach, Kigamboni Kwa thamani ya Milioni 800 Kwa Kiwanja, imepewa Ardhi Bure Ili iwekeze Kwa kuingia Ushirika wa Mradi Katika Ardhi ya Mtu Binafsi (Kampuni ya Azimio).

Aina hiyo ya Ushirika hujulikana Kwa wataalam wa Sekta ya Majengo (Real Estate) Kama Utaratibu wa "Land for Equity" (Yaani Ardhi Kwa Hisa). Ambapo Katika Makubaliano ya Mradi, Mbia Mmoja wa Mradi anatoa Ardhi Na Mbia mwengine anatoa Fedha za Uwekezaji. Na kisha Hisa za Mradi hugawanywa kulingana Na mtaji wa Kila Mmoja (Ardhi Kwa Mbia wa kwanza, Na Fedha Kwa Mbia mwengine).

Na hili si Jambo jipya nchini. Uchunguzi unathibitisha kuwa kilichofanywa na NSSF (Katika Mradi wa Dege Beach Kigamboni) ndicho kinachofanywa na taasisi mbalimbali nchini (wakiwemo NSSF wenyewe), katika Miradi mbalimbali ya Uwekezaji wa Ushirikiano kati sekta ya Majengo.

Baadhi ya mifano ya Miradi ya namna hiyo ni kama ifuatavyo:

• Miaka ya 90 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliingia makubaliano na Shirika la Mafuta la Taifa (TPDC) kujenga Jengo la Mafuta House kwenye ardhi inayomilikiwa na NHC katika eneo ambalo sasa pamejengwa Jengo la Banjamin Mkapa Towers. Katika Ujenzi Huo NHC walipewa asilimia 25 ya thamani ya mradi kwa kutoa ardhi (Land for Equity) ambayo mwaka 1995 ilikuwa ni Shilingi bilioni 19 bilioni. Kwa mujibu wa mkataba huo thamani ya ardhi ile mwaka huo ilikuwa shs 4.75 bilioni.

Mwaka 1995 thamani ya ardhi katikati ya jiji la Dar es salaam ilikuwa ni shilingi 62,500 kwa kila mita ya mraba na kiwanja kile kina mita za mraba 6,221 sawa na ekari moja na nusu. Kwa kutumia mahesabu ya kawaida thamani ya ardhi ya NHC ingekuwa shilingi 388 milioni Na si hiyo 4.75 Bilioni ambayo inaonyesha bei kukuzwa Kwa nyongeza ya shilingi 4.35 bilioni.

• NSSF ni mfaidika wa Utaratibu wa "Land for Equity" Katika mradi Mpya wa Umeme Mkuranga. Mwaka 2014 NSSF ilinunua ardhi kwa thamani ya shilingi 100 milioni, ardhi hiyo ilikuwa Ni jumla ya ekari 100.

Mwaka 2015 Wawekezaji waliingia ubia na Shirika la NSSF Ili kujenga Mtambo wa Umeme Katika ardhi Husika. Mchango wa NSSF Katika Mradi Huo ulikuwa ni ardhi yake ya Ekari 100 ambayo iliinunua Kwa Shilingi Milioni 100 Tu Mwaka Mmoja nyuma. Lakini Katika Mkataba wa Mradi Huo NSSF imepata asilimia 10 ya thamani ya Mradi Mzima wa Uwekezaji ambayo ni Dola za Kimarekani 450 Milioni Sawa na zaidi ya Shilingi 900 Bilioni.

Katika Mradi huu wa Mkuranga NSSF ndani ya mwaka mmoja iliweza kupandisha thamani ya ardhi ile kutoka shilingi 100 milioni mpaka shilingi 90 Bilioni ambayo ni Asilimia 10 ya thamani ya Mradi Wote. Kama zingetumika Hesabu Za kawaida Tu thamani ya Uwekezaji wa NSSF kwenye Mradi Husika ilipaswa Kuwa Asilia 0.06 Tu Na Sio Asilimia 10 walizopewa.

• Mradi mwengine uliofuata Utaratibu wa "Land for Equity" (Ardhi Kwa Hisa) ni Taarifa Juu ya makubaliano kati ya NHC na PPF Katika Ujenzi wa Jengo la PPF Tower Mwanza, ambapo NHC walitoa ardhi na kupewa Aslimia 25 ya hisa za mradi husika. Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni 258, Lakini Ukubwa wa ardhi waliyotoa NHC ni Kiwanja cha ekari moja tu.

Kamwe huwezi kusikia ikisemwa kuwa PPF wamenunua Kiwanja Cha Ekari Moja Kwa thamani ya Shilingi Bilioni 64 Kwa Kuwa Ni Ushirika wa Pamoja.

• NSSF imejenga jengo RITA, eneo la Posta jirani Kabisa na Jengo la Klabu ya Billicanas Jijini Dar es salaam. Katika Mradi Huo RITA iliyojengewa Jengo Husika, Na Kwa Kutoa ardhi hiyo wamepata hisa Asilimia 25 ya thamani ya mradi mzima wa Jengo Hilo, ambayo ni hilingi Bilioni 198.

Lakini Ukubwa wa Kiwanja cha RITA ni nusu ekari tu. Kamwe huwezi kusikia NSSF wamenunua nusu ekari kwa Shilingi bilioni 49 Katika Mradi wa Jengo la RITA.

• Miradi mengine iliyofuata Utaratibu huu wa "Land for Equity"
* Mradi kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Fida-Hussein Katika Jengo lililoko Maeneo ya Jirani Na Hospitali ya Ocean Road.
* Mradi wa Jengo la UVCCM eneo la Fire Jijini Dar es salaam.
* Mradi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation eneo la Posta.
* Mradi wa Jengo la UWT (Makao makuu ya Airtel) eneo la Morocco nk.

• Hitimisho:

NSSF iliingia ubia na kampuni ya Azimio Kwaajili ya Uendelezwaji wa Ardhi Katika Mradi wa Dege Beach Kule Kigamboni. Kampuni ya Azimio Kwa Kutoa Ardhi ya Mradi Husika ilipewa asilimia 20 ya thamani ya mradi wa Dege Eco Village.

Lakini Pia kwenye Mkataba wa Mradi Azimio wanapaswa Kutoa 35% ya Fedha za thamani ya Mradi, Hivyo kuwafanya wawe na 55% ya Mradi Husika Huku NSSF wakiwa na 45 ya Mradi Kwa Fedha watakazotoa.

La kushangaza this time wameenda kwenye kamati ya bunge juzi . CAG presented his report na amesema amewapa NSSF clean report and everything is ok.

NSSF wenyewe wanasema hapaana things are not ok. Past management imeharibu mambo.

Kamati ikaamua kuwa the report is ADOPTED na Mradi wa Dege uendelee. Management Ikae na the JV partner waangalie modalities za kuendelea na mradi.

Out of desperation Huyu Mkurugenzi mpya wa NSSF fed the reporters with all lies (Tariff za uwongo). Na maya zaidi hakuna gazeti hata moja ambalo lilifanya investigative journalism na kuuliza basic questions kama vile:

1. Kama kuna ufisadi wa mabilioni why did CAG give clean report?

2. Kama kilichofanyika Dege ni ufisadi then why PPF NHC TBA TPDC etc are not taken to task? Why NSSF?

I'm sure wenye vichwa vilivyotulia Hapa Jamiiforums wataweza kulitazama hili kuala kwa jicho la tatu

Hii inanifanya niacin kuwa huko NSSF kuna CIVIL WAR au VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE. Theory yangu ni kuwa wale wanaokaimu wanawafanyia fitna wakiosimamishwa ili wafukuzwe then wao wawe confirmed. Hiyo ndio vita inayoendelea kwa sasa na maya zaidi huyu mkurugenzi mpya naye amejiingiza kwenye hiii michezo michafu na kutoa taarifa za uwongo kwa vyombo vya habari

Pia tussah kuwa huyu Mkurugenzi mpya aliwahi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa Mradi wa Daraja la Kigamboni ni mradi wa anasa na haunt tija kwa shirika. Lakini wiki tatu zilizopita huyu huyu Mkurugenzi anawaambia waandishi wa habari kuwa Mradi wa Daraja la kigamboni ni mzuri sana kwa taifa na unaingizia Shirika Mabilioni

Nasubiri kwa ham kusoma Jinsi Paskal Mayala atakavyokuja kumjibia na kumtetea huyu Mkurugezi mpya

Chanzo: https://www.jamiiforums.com/threads/ukweli-kuhusu-mradi-wa-nssf-wa-dege-beach-kigamboni.1139716/
 
Back
Top Bottom