Kikwete: Membe alinitesa alivyohamia ACT-Wazalendo

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,889
Reaction score
8,486
Rondo. Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema kuwa uamuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, kuhamia ACT-Wazalendo kutoka CCM mwaka 2020 na kuwania urais ulimpa wakati mgumu.

Amesema hajui kama ni Zitto Kabwe (Kiongozi wa ACT-Wazalendo) ndiye aliyemfuata Membe ajiunge na kukiimarisha chama chake au Membe ndiye aliyemfuata ili akuze demokrasia na aendeleze siasa.

Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 16, 2023 alipokuwa akitoa hotuba wakati wa misa ya kumuaga Membe aliyefariki Mei 12, 2023 katika hospitali ya Kairuki alikokuwa akipatiwa matibabu mpaka umauti ulipomkuta.

Amesema Membe alikuwa jasiri na hakuogopa jambo lolote pale anapoona haliendi sawa hivyo alipoamua kuhama chama ulikuwa uamuzi wake, ingawa yeye (Kikwete) ulimpa wakati mgumu.

Kikwete amesema hata hivyo uamuzi huo haukuathiri ujamaa wao kwa kuwa aliamini kwenye familia kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama anachokiona kinafaa.

"Ukweli uamuzi ule wa Membe ulinipa wakati mgumu wa kushirikiana naye lakini nashukuru baadae tulikuwa vizuri maana hasira zake ziliisha," amesema.

Amesema hata hivyo anajua familia moja inaweza kuwa na wanachama wa Chadema, ACT-Wazalendo, CUF, CCM lakini bado wanaendelea kushirikiana hivyo uamuzi wa Membe aliuchukulia wa aina hiyo.

Kikwete amesema hata hivyo mara kadhaa alifanya jitihada za kutatua changanoto zilizomfanya Membe aondoke CCM.

Bila ya kutaja kama alifanikiwa au la lakini kauli yake na kile kilichotokea mwaka jana baada ya Membe kurejea CCM kinaonyesha mafanikio ya jitihada zake.
 
Lakini tukubali tusikubali,kuingia kwa Magufuli kwenye urais bila kutegemewa kulitokana na makosa ya mikakati ya Kikwete mwenyewe na mtandao wake.

Kikwete na mtandao wake wali mind sana lango kuu asipite mtu asiye wa kwao na kuacha mlango wa uani wazi kabisa.

Tulipopitia miaka mitano ya Awamu ya Tano iwe fundisho, maana Taifa lilngeweza kuingia machafuko yasiyotarajiwa.

CCM yenyewe ilishaingia migawanyiko ambayo hadi leo itachukua muda kuifuta.
 
Lakini tukubali tusikubali,kuingia kwa Magufuli kwenye urais bila kutegemewa kulitokana na makosa ya mikakati ya Kikwete mwenyewe na mtandao wake.

Kikwete na mtandao wake wali mind sana lango kuu asipite mtu asiye wa kwao na kuacha mlango wa uani wazi kabisa.

Tulipopitia miaka mitano ya Awamu ya Tano iwe fundisho, maana Taifa lilngeweza kuingia machafuko yasiyotarajiwa.

CCM yenyewe ilishIngia migawanyiko ambayo hadi leo itachukua muda kuifuta.
Bila Magufuli nyinyiem isingekuwepo
 
Lakini tukubali tusikubali,kuingia kwa Magufuli kwenye urais bila kutegemewa kulitokana na makosa ya mikakati ya Kikwete mwenyewe na mtandao wake...
Hakuna mtu aliyewahi ingia ikulu ya magogoni kwa bahati mbaya ndugu yangu,rais wa nchi hii wenyewe hukaa na kukubaliana 'fulani awe rais'.

Miongoni mwa wenyewe ni Marais wastaafu, wakuu wa idara ya usalama, wakuu jeshini nk.

Unadhani ilikua bahati mbaya magu kuingia tatu Bora na akina migiro!?
 
Lakini tukubali tusikubali,kuingia kwa Magufuli kwenye urais bila kutegemewa kulitokana na makosa ya mikakati ya Kikwete mwenyewe na mtandao wake.

Kikwete na mtandao wake wali mind sana lango kuu asipite mtu asiye wa kwao na kuacha mlango wa uani wazi kabisa.

Tulipopitia miaka mitano ya Awamu ya Tano iwe fundisho, maana Taifa lilngeweza kuingia machafuko yasiyotarajiwa.

CCM yenyewe ilishIngia migawanyiko ambayo hadi leo itachukua muda kuifuta.
Sasa unataka Urais uwe wa Kikwete na Watu wake pekee? Au mimi sijaelewa?

Kuingia kwa Magufuli ulikuwa nimpango wa Mungu.
 
Na bado kuna surprise nyingi sana Tanzania. Anayedhani amesimama, aangalie asianguke.
Watakuja marais wa aina zote ili mradi akili zetu zirudi ndani ya fuvu la kichwa. Kuna mambo yanazalisha watu radicals bila sababu. Mojawapo ni rushwa na udhalimu
 
Rondo. Rais mstaafu Jakaya Kikwete amesema kuwa uamuzi wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, kuhamia ACT-Wazalendo kutoka CCM mwaka 2020 na kuwania urais ulimpa wakati mgumu.

Amesema hajui kama ni Zitto Kabwe (Kiongozi wa ACT-Wazalendo) ndiye aliyemfuata Membe ajiunge na kukiimarisha chama chake au Membe ndiye aliyemfuata ili akuze demokrasia na aendeleze siasa.

Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 16, 2023 alipokuwa akitoa hotuba wakati wa misa ya kumuaga Membe aliyefariki Mei 12, 2023 katika hospitali ya Kairuki alikokuwa akipatiwa matibabu mpaka umauti ulipomkuta.

Amesema Membe alikuwa jasiri na hakuogopa jambo lolote pale anapoona haliendi sawa hivyo alipoamua kuhama chama ulikuwa uamuzi wake, ingawa yeye (Kikwete) ulimpa wakati mgumu.

Kikwete amesema hata hivyo uamuzi huo haukuathiri ujamaa wao kwa kuwa aliamini kwenye familia kila mtu ana uhuru wa kujiunga na chama anachokiona kinafaa.

"Ukweli uamuzi ule wa Membe ulinipa wakati mgumu wa kushirikiana naye lakini nashukuru baadae tulikuwa vizuri maana hasira zake ziliisha," amesema.

Amesema hata hivyo anajua familia moja inaweza kuwa na wanachama wa Chadema, ACT-Wazalendo, CUF, CCM lakini bado wanaendelea kushirikiana hivyo uamuzi wa Membe aliuchukulia wa aina hiyo.

Kikwete amesema hata hivyo mara kadhaa alifanya jitihada za kutatua changanoto zilizomfanya Membe aondoke CCM.

Bila ya kutaja kama alifanikiwa au la lakini kauli yake na kile kilichotokea mwaka jana baada ya Membe kurejea CCM kinaonyesha mafanikio ya jitihada zake.
Kilichofanya Membe aondoke CCM ni wendawazimu wa yule dhalim. Kifo cha yule mwovu ndiyo kilimrudisha Membe CCM.
 
Lakini tukubali tusikubali,kuingia kwa Magufuli kwenye urais bila kutegemewa kulitokana na makosa ya mikakati ya Kikwete mwenyewe na mtandao wake.

Kikwete na mtandao wake wali mind sana lango kuu asipite mtu asiye wa kwao na kuacha mlango wa uani wazi kabisa.

Tulipopitia miaka mitano ya Awamu ya Tano iwe fundisho, maana Taifa lilngeweza kuingia machafuko yasiyotarajiwa.

CCM yenyewe ilishIngia migawanyiko ambayo hadi leo itachukua muda kuifuta.
Fundisho gani wakati tulipita miaka mitano ya bata na gharama za vyakula na vifaa vya ujenzi vikiwa bei inayoeleweka.Kikwete alifanya vizuri sana kumpitisha Marehemu Jiwe.
 
Sasa unataka Urais uwe wa Kikwete na Watu wake pekee? Au mimi sijaelewa?

Kuingia kwa Magufuli ulikuwa nimpango wa Mungu.
Yah. Mungu ni wa ajabu. Anakuweka ktk majaribu makubwa kwa kumleta shetani kwako. Kisha tena Mungu huyohuyo kwa wakati wake atamponda shetani, nawe utakiri kuwa Mungu ni mkuu.
 
Back
Top Bottom