Bungeni: Serikali yakiri kudhulumu watu

Bungeni: Serikali yakiri kudhulumu watu

Jee, UKAWA ikitokea bahati mbaya mkachukuwa nchi mtaendeleza hili la kurudishia watu mali zao walizodhulumiwa?

Ndio....Tutaanza Na CCM iliyodhulumu mali za wananchi.

Mfano maeneo ya wazi na viwanja vingi vya mpira wa miguu mikoani ambavyo vilikua vya wananchi wote lakini CCM imedhulumu
 
Hilo nalo neno, tunataka nchi isiyodhulumu raia wake, na ikiwa leo wamekiri hili nililoandika nadhani na hayo uyaletayo ukiyawakilisha kwa mbunge wako kwa ushahidi kama alivyofanya huyo aliyetetewa na mbunge wake leo bungeni utakuwa umefanya la maana sana katika kupigania haki.

KUONDOA HILI FUTILIA MBALI HII KITU CCM:confused2:
 
Kwa serikali hii unaweza kuambiwa hayo ni maneno ya waziri ni si ya serikali ukapoteza time yako bure ya kufuatilia madai mfu
 
Jee, UKAWA ikitokea bahati mbaya mkachukuwa nchi mtaendeleza hili la kurudishia watu mali zao walizodhulumiwa?

UKAWA wanapigania usawa na haki za watanzania. Hapo ni kama unauliza makofi polisi.usiwe na shaka.dhulma zote zilizofanywa na serikali dhalimu ya ccm zitalipwa.na sheria itachukuwa mkondo wake.
 
Hawa wananchi ndiyo walioteseka.

Nionyeshe picha moja tu ya "mwarabu koko" au mhindi "amekomeshwa" na Nyerere na anaishi maisha ya dhiki kama haya.

Mali zipi zilizodhulumiwa zilifika hapa kuwakomboa?

View attachment 258643

Duuuuuh camera mega pixel 16,wakati huo zilikuwepo?Acha fix
 
Aliyekomeshwa na Nyerere ni mlalahoi siyo aliyedhulumiwa.

Nani aliyekufa na njaa kijijini?

Nani aliyekula ugali wa njano wa misaada?

Nani alikula mlo mmoja kwa siku?

Nani aliyetembea na matambara mabovu kama nguo?

Umeshawahi kusoma wahindi waliofukuzwa na Idi Amin wanateseka London? Google usome biashara zao leo.
Museveni mwenyewe kawarudishia mali zao na leo wana viwanda vingi na ni wakulima wakubwa Uganda.

Angalia matajiri wa Tanzania leo.
Nani mtoaji mkubwa wa ajira na mlipa kodi?

Kuwa mkweli. Acha chuki binafsi na ubaguzi.

Mlalahoi alikomeshwaje na Nyerere? kupewa heshima katika nchi yake ni kukomeshwa? Mawazo yako ni yaleyale ya Kibepari. Kutegemea kuajiriwa, why watanzania hawawazi kujitegemea lakini? Nyie waarabu mnaajiri au mnanyonya nguvu za walalahoi? Na safari hii tunarudi kwenye usoshalist mtakoma!
Kwa taarifa yako leo watanzania ndio wanakula mlo moja si enzi za Nyerere, kama unaongelea njaa ya 74 that was catastrophy
 
Hawa wananchi ndiyo walioteseka.

Nionyeshe picha moja tu ya "mwarabu koko" au mhindi "amekomeshwa" na Nyerere na anaishi maisha ya dhiki kama haya.

Mali zipi zilizodhulumiwa zilifika hapa kuwakomboa?

View attachment 258643

Toa ujinga wako hapa, miaka ile hapakuwa na picha za rangi, unamlaghai nani?
Ebu muulize baba yako Tz ilikuwa ya ngapi kufuta ujinga duniani miaka ile?
 
Leo nimeona "live" katika bunge wakati wa majumuisho ya bajeti ya Wizara ya fedha, kuna mbunge (sikumbuki jina) alisimama kumtetea mtu wa jimboni kwake kuwa alidhulumiwa wakati wa "uhujumu uchumi" na amekuwa anahangaishwa kulipwa madai yake na mwisho akaambiwa amechelewa. Mbunge huyo alisema kama kuchelewa alikuwa hajachelewa kwani anadai siku zote na ushahidi upo. Ndipo aliposimama Naibu Waziri wa Fedha na kumtaka huyo mbunge kuwa awasilishe madai yake yote kwake na karatasi zake zote na anaahidi kushughulikia hilo na kuhakikisha haki inapatikana kwani ni kweli wengi walidhulumiwa wakati wa (operesheni) ya Uhujumu Uchumi.

Ikumbukwe kuwa hii operesheni ilifanyika wakati marehemu Nyerere akiwa Rais na marehemu Sokoine akiwa Waziri Mkuu.

Huyo mbunge alisema kuwa wapo pia waliolipwa kwa kuonekana kweli walidhulumiwa.

Sasa nnajiuliza, na tusichangie hili kwa jazba, Ikiwa serikali inakiri tena bungeni, watu walidhulumiwa, jee ni hatua gani wale waliodhulumiwa wazee ambao wameshakufa ili kudai haki zao, si kurudishiwa tu mali zao na hukumu ipi "posthumous" inayoweza kutolewa kwa waliodhulumu?

Tukumbuke watu walidhulumiwa si katika uhujumu uchumi tu, kama Serikali ilivyokiri leo bungeni bali pia kuna watu waliodhulumiwa wakati wa Azimio la Arusha. Nao wakati wa Mwinyi waliambiwa wakadai lakini kwa kuwa haikutangazwa sana wengine walipoenda wakaambiwa wamechelewa, hivi haki ya mtu kweli ina kuchelewa katika kuidai?

Kwanza nnaisifu sana Serikali ya awamu hii kwa kukiri hilo bungeni "live" kuwa kweli kuna dhuluma ilitendeka. Kwa hakika Serikali kukiri hilo kosa ni ujasiri mkubwa sana na ni njia nzuri sana ya wananchi waliodhulumiwa kuweza kurudisha imani kwa Serikali yao na sasa wapokelewe na kurudishiwa mali zao na kusiwe na hili suala la kuchelewa.

Naipongeza Serikali kwa hilo, na lisiishie hapo watutangazie tuanzie wapi? Kwani nnaamini si wengi waliosikia hilo bungeni kwani si wengi wanaotazama bunge.

Nawaomba na waandishi wa habari walitangaze hili, kwani ni jambo la kheri kubwa sana, hakuna dua inayopokelewa haraka kama ya mwenye kudhulumiwa, pengine haya majanga yote yanayotupata Tanzania ni kwa hizo dhuluma zilizofanywa na viongozi wetu huko nyuma, ni wakati muafaka Serikali kukiri hilo na kuanza kufanya toba na kurudisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.

Hansard zitakuwa zipo kwa wanaotaka kuelewa zaidi.

Ahsante Serikali kwa kuliweka wazi hilo.
Muongo akishazoeleka kwa kusema uwongo, basi siku akisema ukweli kuna watu wanadhani anatakiwa kupongezwa.. Kupongezwa atapongezwa endapo tu ... Atalipa waliodhurumiwa kwenye kila nyanja
- Uhujumu uchumi,
- Mabomu ya mbagala na gongolamboto
- Waliofukiwa na kutolipwa fidia kwenye uanzishwaji wa mgidi wa Bulyanhulu
- Walionyang'anywa haki ya ardhi sehemu mbalimbali hapa TZ

Jee, UKAWA ikitokea bahati mbaya mkachukuwa nchi mtaendeleza hili la kurudishia watu mali zao walizodhulumiwa?

Sio tu waliodhulumiwa mali watarudishia, lakini pia watu kama Dr. Ulimboka aliyeteswa na Ramadhani Ighondi kwa maelekezo ya Ikulu naye atapewa fidia kwa mateso aliyoyapata na wale wote waluiohusika kuagiza, au kushiriki moja kwa moja katika utesaji watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
FaizaFoxy hata dhuluma ya idadi ya kura alizopata Padre Slaa nayo itangazwe ili fidia iwekwe wazi..maana marupurupu ya wabunge wa kuteuliwa kwa miaka mitano ingeweza kujenga upinzani imara zaidi...kuliko huu. Serikali iseme
 
Last edited by a moderator:
Ukimwuuliza Nyerere huko aliko kwa nini alinyanganya watu mali zao, kwa nini aliprlrka watu maporini wakaliwa na wanyama wakali, uhujumu uchumi ulikuwa ni nini hasa bila shaka atalia machozi ya damu. Ulikuwa ni upuuzi mtupu.
 
Leo nimeona "live" katika bunge wakati wa majumuisho ya bajeti ya Wizara ya fedha, kuna mbunge (sikumbuki jina) alisimama kumtetea mtu wa jimboni kwake kuwa alidhulumiwa wakati wa "uhujumu uchumi" na amekuwa anahangaishwa kulipwa madai yake na mwisho akaambiwa amechelewa. Mbunge huyo alisema kama kuchelewa alikuwa hajachelewa kwani anadai siku zote na ushahidi upo. Ndipo aliposimama Naibu Waziri wa Fedha na kumtaka huyo mbunge kuwa awasilishe madai yake yote kwake na karatasi zake zote na anaahidi kushughulikia hilo na kuhakikisha haki inapatikana kwani ni kweli wengi walidhulumiwa wakati wa (operesheni) ya Uhujumu Uchumi.

Ikumbukwe kuwa hii operesheni ilifanyika wakati marehemu Nyerere akiwa Rais na marehemu Sokoine akiwa Waziri Mkuu.

Huyo mbunge alisema kuwa wapo pia waliolipwa kwa kuonekana kweli walidhulumiwa.

Sasa nnajiuliza, na tusichangie hili kwa jazba, Ikiwa serikali inakiri tena bungeni, watu walidhulumiwa, jee ni hatua gani wale waliodhulumiwa wazee ambao wameshakufa ili kudai haki zao, si kurudishiwa tu mali zao na hukumu ipi "posthumous" inayoweza kutolewa kwa waliodhulumu?

Tukumbuke watu walidhulumiwa si katika uhujumu uchumi tu, kama Serikali ilivyokiri leo bungeni bali pia kuna watu waliodhulumiwa wakati wa Azimio la Arusha. Nao wakati wa Mwinyi waliambiwa wakadai lakini kwa kuwa haikutangazwa sana wengine walipoenda wakaambiwa wamechelewa, hivi haki ya mtu kweli ina kuchelewa katika kuidai?

Kwanza nnaisifu sana Serikali ya awamu hii kwa kukiri hilo bungeni "live" kuwa kweli kuna dhuluma ilitendeka. Kwa hakika Serikali kukiri hilo kosa ni ujasiri mkubwa sana na ni njia nzuri sana ya wananchi waliodhulumiwa kuweza kurudisha imani kwa Serikali yao na sasa wapokelewe na kurudishiwa mali zao na kusiwe na hili suala la kuchelewa.

Naipongeza Serikali kwa hilo, na lisiishie hapo watutangazie tuanzie wapi? Kwani nnaamini si wengi waliosikia hilo bungeni kwani si wengi wanaotazama bunge.

Nawaomba na waandishi wa habari walitangaze hili, kwani ni jambo la kheri kubwa sana, hakuna dua inayopokelewa haraka kama ya mwenye kudhulumiwa, pengine haya majanga yote yanayotupata Tanzania ni kwa hizo dhuluma zilizofanywa na viongozi wetu huko nyuma, ni wakati muafaka Serikali kukiri hilo na kuanza kufanya toba na kurudisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.

Hansard zitakuwa zipo kwa wanaotaka kuelewa zaidi.

Ahsante Serikali kwa kuliweka wazi hilo.

Kwa muktadha wa kichwa cha habari na kilichomo ndani ya bandiko lako na ukisoma pale nilipoweka wino mzito, bandiko lako linajikanganya sana, kimantiki na kisheria pia.

1. Operesheni hiyo ilifanywa na Serikali = hivyo hakutakuwa na "posthumous judgment" dhidi ya Serikali kwni Serikali haijafa na ni nadra sana kwa Serikali kufa. Na hata inapotokea mapinduzi au nchi mpya kuzaliwa kutoka nchi ya zamani na Seikali mpya kuingia/kuzaliwa, madeni na madai huendelea kuwapo na kudaiwa, "subject to the statute of limitation".

2. Kama ulimaanisha watu/watendaji waliofanya dhuluma hiyo, itakuwa ngumu kuwadai kwani walifanya wakiwa kazini, i.e in the course of emplyoment.

Kwa hiyo hoja yako inakosa msingi kwa mantiki ya mkanganyiko huo wa kisheria. Na kama ulimlenga Nyerere hapo ndio ngumu kabisa kwani ana kinga ya kikatiba.
 
Wewe umezaliwa lini?

Vijijini kulikuwa hamna njaa na dhiki?

Na vyakula vya ration ni fix pia?

Kweli mmerogwa!

Njaa na dhiki vimeisha vijijini?
Hebu usiwe mzigo na badala yake Fikirisha akili yako kidogo,mlalahoi utamdhulumu nini?
 
Serikali hii ya awamu ya nne ndiyo hasa imeweka dhuluma kupitia kodi za kero na zisizolipika kama kipaumbele chake. Nitatoa mifano michache:
1.Kupandisha Motor vehicle licence kutoka elfu 20 hadi laki 3 kwa mwaka
2.kuongeza gharama za fire tingisha kutoka elfu 5 hadi elfu 50 bila sababu yoyote
3. Land rent imeongezwa hadi 300% bila sababu yoyote ya msingi
4. Kunyanganya watu ardhi yao na kuwapa wawekezaji bila fidia au kwa fidia mbuzi
5. kutowalipa wafanyakazi salaries increaments au pesa za likizo
7. kuwabambika wafanya biashara kodi kubwa zaidi ya ile wangetakiwa kulipa kwa kiwango cha mitaji yao
8.kuwauzia wafanya biashara EFDs za elfu 30 kwa laki 8
9. kulipa wafanyakazi mishahara mbuzi
10. Kudhulumu haki ya watu kuandamana, kuchagua wanayempenda
11. etc

Hapo penye red
11. kudhulumu maisha ya wanaotetea haki mfano:Mwangosi na kuiacha familia yake inateseka.
12. Kutishia wafanya kazi wasidai haki zao mfano:Kumtesa dr.Ulimboka na kumtupa porini
13. Kuwafumba vinywa waandishi wa habarimfano: kumteka na kumn'goa jicho yule mhariri wa gazeti...
na kufungia gazeti la mwanahalisi lililotoa tetesi za aliyemtesa ulimboka.
14.etc
 
Duuuuuh camera mega pixel 16,wakati huo zilikuwepo?Acha fix
Kuu hii picha ni ya kipindi
hiki cha maisha bora kwa kila mtanzania,
enzi za mwalimu usingemkuta mtanzania
anayeteswa kihivi kwenye jamuhuri ya muungano wa tz.
 
Back
Top Bottom