Bungeni: Serikali yakiri kudhulumu watu

Bungeni: Serikali yakiri kudhulumu watu

Serikali ya Tanzania kama zilivyo serikali nyingi za kiafrika zimejaa dhulma. Ni aheri hata hapo zamani utasema kuwa haki za binadamu karibu Dunia nzima zilikuwa zimefifshwa na watawala. Angalia Waarabu walivyowadhulmu waafrika kwenye biashara ya utumwa, Wamarekani dhidi ya Waafrika, Makaburu dhidi ya watu weusi, Urusi, China, Yugoslavia, Romania dhidi ya wananchi wao, n.k.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba wenzetu katika mataifa mengine, dhulma hizo za kale zimefutika lakini kwetu zimeendelezwa na kuoteshwa mizizi. Angalia utawala wa Kikwete ulivyowadhulmu watu haki ya kuishi, rejea mauaji ya Mwangosi, kutolewa watu kucha na meno, miswada ya kugandamiza haki za habari, kukataa mamlaka ya wananchi kwa kupitia katiba ya CCM dhidi ya ile ya wananchi, n.k.

Nadhani wakati tunakiri dhulma zilizofanyika zamani, tuangalie kwa umakini juu ya hizi za sasa ambazo kuna wapumbavu wachache mpaka sasa wanazishabikia kisa tu zinafanywa na wapendwa wao dhidi ya mahasimu wao.

Safi sana kwa kukubali kuwa uhujumu uchumi wa wakati wa Nyerere na Sokoine kuna dhulma ilifanyika.

Wewe ni kati ya wachache sana, kuna watu hawaamini kabisa kama wakati wa utawala Nyerere kungeweza kuwa kumefanyika dhulma na serikali ikaja kukiri bungeni.

Ni ajabu kubwa sana.
 
Leo nimeona "live" katika bunge wakati wa majumuisho ya bajeti ya Wizara ya fedha, kuna mbunge (sikumbuki jina) alisimama kumtetea mtu wa jimboni kwake kuwa alidhulumiwa wakati wa "uhujumu uchumi" na amekuwa anahangaishwa kulipwa madai yake na mwisho akaambiwa amechelewa. Mbunge huyo alisema kama kuchelewa alikuwa hajachelewa kwani anadai siku zote na ushahidi upo. Ndipo aliposimama Naibu Waziri wa Fedha na kumtaka huyo mbunge kuwa awasilishe madai yake yote kwake na karatasi zake zote na anaahidi kushughulikia hilo na kuhakikisha haki inapatikana kwani ni kweli wengi walidhulumiwa wakati wa (operesheni) ya Uhujumu Uchumi.

Ikumbukwe kuwa hii operesheni ilifanyika wakati marehemu Nyerere akiwa Rais na marehemu Sokoine akiwa Waziri Mkuu.

Huyo mbunge alisema kuwa wapo pia waliolipwa kwa kuonekana kweli walidhulumiwa.

Sasa nnajiuliza, na tusichangie hili kwa jazba, Ikiwa serikali inakiri tena bungeni, watu walidhulumiwa, jee ni hatua gani wale waliodhulumiwa wazee ambao wameshakufa ili kudai haki zao, si kurudishiwa tu mali zao na hukumu ipi "posthumous" inayoweza kutolewa kwa waliodhulumu?

Tukumbuke watu walidhulumiwa si katika uhujumu uchumi tu, kama Serikali ilivyokiri leo bungeni bali pia kuna watu waliodhulumiwa wakati wa Azimio la Arusha. Nao wakati wa Mwinyi waliambiwa wakadai lakini kwa kuwa haikutangazwa sana wengine walipoenda wakaambiwa wamechelewa, hivi haki ya mtu kweli ina kuchelewa katika kuidai?

Kwanza nnaisifu sana Serikali ya awamu hii kwa kukiri hilo bungeni "live" kuwa kweli kuna dhuluma ilitendeka. Kwa hakika Serikali kukiri hilo kosa ni ujasiri mkubwa sana na ni njia nzuri sana ya wananchi waliodhulumiwa kuweza kurudisha imani kwa Serikali yao na sasa wapokelewe na kurudishiwa mali zao na kusiwe na hili suala la kuchelewa.

Naipongeza Serikali kwa hilo, na lisiishie hapo watutangazie tuanzie wapi? Kwani nnaamini si wengi waliosikia hilo bungeni kwani si wengi wanaotazama bunge.

Nawaomba na waandishi wa habari walitangaze hili, kwani ni jambo la kheri kubwa sana, hakuna dua inayopokelewa haraka kama ya mwenye kudhulumiwa, pengine haya majanga yote yanayotupata Tanzania ni kwa hizo dhuluma zilizofanywa na viongozi wetu huko nyuma, ni wakati muafaka Serikali kukiri hilo na kuanza kufanya toba na kurudisha imani ya wananchi kwa Serikali yao.

Hansard zitakuwa zipo kwa wanaotaka kuelewa zaidi.

Ahsante Serikali kwa kuliweka wazi hilo.
ndugu unataka nani ahadhibiwe kwa dhuluma hizo, waliosimamia sera hiyo, wameishakufa wote, duniani kote, masuala kama haya, serikali hutoa pole tu, wahindi wekundu, wa america, wa aborigini wa australia, jamii zote hizi zilidhurumiwa, ni hv karibu serikali za nchi hizo, zilikili wazi kwamba dhuluma ilitendeka, watendewa wakaombwa radhi mbele ya tume ya maridhiano, na maisha ya naendelea, hamna Kesi wala fidia.
 
Kafungulie nyuzi hayo yako tutakuja kujadili, hapa mada ni waliodhulumiwa wakati wa "uhujumu uchumi" na kilichoongewa bungeni kuhusu hilo, hebu soma mada.
FF mada yako umedadavua karibu kila kitu umemaliza sasa sio vema wachangiaji wakawa limited bila kuongeza mambo mengine yanayohusiana na dhuluma.Maana tunapojadili mambo ya zamani tunafanya.hivyo si kwa faida ya wafu bali kwa faida ya walio hai.kuhusu nini tuwafanye watawala waliofanya dhulma kwa kweli sijui niseme nini maana walishakufa almost.cha kuwafanya hakipo.Hapo ndo unapokuja umuhimu katika mada yako wa kuchomekea na dhulma zinazoendelea au zilizofanyika baada ya Nyerere.
 
ndugu unataka nani ahadhibiwe kwa dhuluma hizo, waliosimamia sera hiyo, wameishakufa wote, duniani kote, masuala kama haya, serikali hutoa pole tu, wahindi wekundu, wa america, wa aborigini wa australia, jamii zote hizi zilidhurumiwa, ni hv karibu serikali za nchi hizo, zilikili wazi kwamba dhuluma ilitendeka, watendewa wakaombwa radhi mbele ya tume ya maridhiano, na maisha ya naendelea, hamna Kesi wala fidia.
Nakubaliana na wewe.Nadhani.cha msingi kwa sasa ni.kuangalia dhulma za sasa zisijitokeze,kusubiri watu wafe ndo tudai fidia wala haisaidiii.Tujifunze kutoka dhulma za zamani kwa kuzuia au kupigia kelele dhulma zinazoendelea sasa.Hii kidogo italeta sense.
 
Mbona kawaida serikali hii ya CCM uchaguzi ukikaribia kila kitu ni chema.......ole wapewe nchi 2016 Januari utaona upande wao wa pili
 
ndugu unataka nani ahadhibiwe kwa dhuluma hizo, waliosimamia sera hiyo, wameishakufa wote, duniani kote, masuala kama haya, serikali hutoa pole tu, wahindi wekundu, wa america, wa aborigini wa australia, jamii zote hizi zilidhurumiwa, ni hv karibu serikali za nchi hizo, zilikili wazi kwamba dhuluma ilitendeka, watendewa wakaombwa radhi mbele ya tume ya maridhiano, na maisha ya naendelea, hamna Kesi wala fidia.

= zilidhulumiwa

Kwa hiyo unashauri na Watanzania waliodhulumiwa waombwe radhi maisha yaendelee. Na hilo alilosema huyu waziri sasa hivi za kusikiliza kilio chao na walipwe unaona halifai?
 
Hilo nalo neno, tunataka nchi isiyodhulumu raia wake, na ikiwa leo wamekiri hili nililoandika nadhani na hayo uyaletayo ukiyawakilisha kwa mbunge wako kwa ushahidi kama alivyofanya huyo aliyetetewa na mbunge wake leo bungeni utakuwa umefanya la maana sana katika kupigania haki.

nimeipenda mada yako inavyoonyesha serikali ya ccm inavyodhulumu, hata hivyo serikali hii ilidhulumu sana wananchi wa kagera babu yangu roli lake lilipelekwa vitani halikurudi yalikuwa yanakamatwa na kupaka rangi ya jeshi
 
Serikali ya Tanzania kama zilivyo serikali nyingi za kiafrika zimejaa dhulma. Ni aheri hata hapo zamani utasema kuwa haki za binadamu karibu Dunia nzima zilikuwa zimefifshwa na watawala. Angalia Waarabu walivyowadhulmu waafrika kwenye biashara ya utumwa, Wamarekani dhidi ya Waafrika, Makaburu dhidi ya watu weusi, Urusi, China, Yugoslavia, Romania dhidi ya wananchi wao, n.k.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba wenzetu katika mataifa mengine, dhulma hizo za kale zimefutika lakini kwetu zimeendelezwa na kuoteshwa mizizi. Angalia utawala wa Kikwete ulivyowadhulmu watu haki ya kuishi, rejea mauaji ya Mwangosi, kutolewa watu kucha na meno, miswada ya kugandamiza haki za habari, kukataa mamlaka ya wananchi kwa kupitia katiba ya CCM dhidi ya ile ya wananchi, n.k.

Nadhani wakati tunakiri dhulma zilizofanyika zamani, tuangalie kwa umakini juu ya hizi za sasa ambazo kuna wapumbavu wachache mpaka sasa wanazishabikia kisa tu zinafanywa na wapendwa wao dhidi ya mahasimu wao.

Hiyo hotuba uliyotowa labda yapo yenye ukweli labda hayapo yenye ukweli. Yanhitaji mjadala na ni mada nyingi tofauti ulioziongea.

Hili nililoliongea ni la sasa, au hujaona nilivyoandika "leo nimeona "live"", rudia post namba moja. Hilo ni la sasa bungeni limejadiliwa bunge hili ambalo linaendelea tena ni juzi tu, tarehe 7-06-2015. Na huyo aliyetajwa bungeni kudhulumiwa yupo hai anaishi na wengi wapo kama yeye.

Ni nini kilichokufanya uone kuwa hili ni la zamani? Hatuongelei historia hapa tunaongelea mambo yaliyojadiliwa na bunge hili linaloendelea - Kumbuka hilo.
 
Kwa sababu Nyerere alishakufa, mimi nashauri adhabu wapewe watoto zake, Hao Akina Makongoro si wapo badala ya kuwa rais apewe adhabu kwa niaba ya baba yake.

Nafikiri faiza utakuwa umefurahi.

Mtu alishakufa hawezi kubadilisha chochote wala kujibu chochote.
Huyu mwenzenu anayeshindwa kudhibiti ufisadi Hana tatizo kwa sababu ni ndugu Katika Imani.

maamuzi hayo hayakufanyika kifamilia ili uwahukumu watoto bali yalikua ya kiserikali. hivyo ni wajibu wa serikali na si familia ya aliyekua madarakani
 
= dhuluma / dhulma
= dhuluma / dhulma
= dhuluma / dhulma

Hebu waambie wakubwa wako wa ukawa waliweke kwenye sera zao au japo waliongelee kama walivyoliongelea mbunge na waziri wa CCM.

religious political masquarads zitakuua wewe. Endelea na ccm
 
nimeipenda mada yako inavyoonyesha serikali ya ccm inavyodhulumu, hata hivyo serikali hii ilidhulumu sana wananchi wa kagera babu yangu roli lake lilipelekwa vitani halikurudi yalikuwa yanakamatwa na kupaka rangi ya jeshi

Kadai, walilipwa. Mimi magari yetu matatu yalikamatwa lakini tulilipwa tena tulilipwa vizuri sana kuliko yangefanya kazi na yote yalirudi mazima kabisa hayana ubovu hata kidogo, na moja lilitiwa engine mpya kabisa.
 
= dhuluma / dhulma
= dhuluma / dhulma
= dhuluma / dhulma

Hebu waambie wakubwa wako wa ukawa waliweke kwenye sera zao au japo waliongelee kama walivyoliongelea mbunge na waziri wa CCM.
sms sent and delivered and understood in the same manner i intended.
religious political masquarads zitakuua wewe. Endelea na ccm
 
Sasa hapa rangI yako halisi inaanza kuonekana,toka uzi unaanza nilijua tu angle yako ni ipi!Mpaka mwisho wa mjadala utakuwa umejiweka wazi vizuri!It's all about personal attacks,Nyerere itakuwa alikutenda vibaya sana,lakini u r fighting a dead body!It won't give u any relief!

One more thing,usiwalazimishe watu kufikiria ndani ya box,kila ukibanwa unasema wakafungue nyuzi wajadili hayo!Mjadala hauwezi kuishia dhulma iliyofanyika wakati Nyerere akiwa madarakani, lazima tufikiri zaidi!je,mambo hayo ni kweli?je,kwanin ilitokea hivyo?Kulikuwa na dhamira hiyo au walikumbwa na kimbunga kiliwapitia?je,dhuluma bado ipo Mpaka sasa?Hatua gani zimechukuliwa?

NB:katika baadhi ya waliodhulumiwa ni pamoja shule za dini ili mimi,mleta mada,mpagani,JK na watz wote tupate elimu!
Hizo taasis nazo zijitokeze kudai haki zao!

Naona huna hoja, sasa wakati wa "uhujumu uchumi" ulikuwa ni utawala wa nani? Kama unafikiri unavyofikiri basi ungeanza kumlaumu waziri aliyekiri hilo bungeni, si mimi.
 
Afadhali umeanza kujibainisha uarabu koko wako!!
Nyerere aliwakomesha nyie. Hata kama mlidhulumiwa mali hizo zilienda kwa walalahoi ambao walipewa huduma bora ikiwamo shule na matibabu bure.
Sijui utasemaje kwa dhuluma kubwa inayofanywa na serikali yako hii kwa walalahoi. Wataamka tu.
Hao unaosema walidhulumiwa wanadai leo baada ya kuona serikali ni ya ubabaishaji, haina msimamo, kwa nini wasidai angalau wakati wa Mwinyi na Mkapa wadai leo? Huoni sababu ni kuwa serikali nayo ni ya kifisadi tu? Wanasema mvuna janga hula na wa kwao. Ndicho kinachotendeka
 
Jee, UKAWA ikitokea bahati mbaya mkachukuwa nchi mtaendeleza hili la kurudishia watu mali zao walizodhulumiwa?

Kwahyo unataka kusema ukawa wakiingia magogoni hawatafanya chochote?
 
Na hizi dhuluma zitaisha kwa kukiondoa chama dhalimu cha ccm,ungana na UKAWA wakati ni sasa kungwi.

Uzuri ni kuwa aliyeleta hiyo mada bungeni ni mbunge wa CCM na waziri wa CCM amekiri na amesema atalishughulikia hilo alilolalamikiwa na kama kuna wengine basi wapeleke malalamiko yao na wapo ambao tayari wameshalipwa fidia kwa dhulma walizofanyiwa.

UKAWA sijawasikia hata wakigusia hayo.
 
Hapana si wana siassa tu, kuna watu nnawajuwa ambao hawako kwenye siasa wamerudishiwa baadhi ya mali zao.

Hizo limitation za gari kuwa central na masuala haya kwa muono wangu ni vitu tofauti.

Kwanini viziondolewe limitation au iwekwe ya kmuda mrefu ili watu wapate fursa ya kudai mali zao, kwani kuna wenye mali waliodhulumiwa na wamekufa lakini kuna warithi wao.
Siyo wanasiasa per se ila wengi waliorudishiwa majumba ni wale ambao walikuwa kwa namna moja au nyingine wapo connected na siasa.

Kuhusu, muda najua ilo lipo ila sina uhakika ni muda gani na uspotokea kuclaim basi inapigwa mnada. It's the same principle na magari kwa sababu hata uagizaji wa magari used ulikatazwa na yalikamatwa mengi ila wengine walirudishiwa na wengine ikala kwao.

Huyo waziri ameifanya ionekane rahisi kwa sasa, ila ni too late. Sidhani kama kuna kitu kitabdilika.
 
Afadhali umeanza kujibainisha uarabu koko wako!!
Nyerere aliwakomesha nyie. Hata kama mlidhulumiwa mali hizo zilienda kwa walalahoi ambao walipewa huduma bora ikiwamo shule na matibabu bure.
Sijui utasemaje kwa dhuluma kubwa inayofanywa na serikali yako hii kwa walalahoi. Wataamka tu.
Hao unaosema walidhulumiwa wanadai leo baada ya kuona serikali ni ya ubabaishaji, haina msimamo, kwa nini wasidai angalau wakati wa Mwinyi na Mkapa wadai leo? Huoni sababu ni kuwa serikali nayo ni ya kifisadi tu? Wanasema mvuna janga hula na wa kwao. Ndicho kinachotendeka

Aliyekomeshwa na Nyerere ni mlalahoi siyo aliyedhulumiwa.

Nani aliyekufa na njaa kijijini?

Nani aliyekula ugali wa njano wa misaada?

Nani alikula mlo mmoja kwa siku?

Nani aliyetembea na matambara mabovu kama nguo?

Umeshawahi kusoma wahindi waliofukuzwa na Idi Amin wanateseka London? Google usome biashara zao leo.
Museveni mwenyewe kawarudishia mali zao na leo wana viwanda vingi na ni wakulima wakubwa Uganda.

Angalia matajiri wa Tanzania leo.
Nani mtoaji mkubwa wa ajira na mlipa kodi?

Kuwa mkweli. Acha chuki binafsi na ubaguzi.
 
MpigfilimbiwTHANKS to Prof. Jafvert Chad for some kind of "seed funding" which helps Hilonga to test his business model for Africa Prize for Engineering Innovation. Order your Unit at a DISCOUNTED PRICE NOW! Prof.Chad's support provides for one of the three components of Hilonga's integrated filter. The price of complete integrated filter NOW is Ths.250 said:
hilonga@gmail.com[/email] for details. ...........................X........................X..........................x..........................x..aHamelin;12947927]Afadhali umeanza kujibainisha uarabu koko wako!!
Nyerere aliwakomesha nyie. Hata kama mlidhulumiwa mali hizo zilienda kwa walalahoi ambao walipewa huduma bora ikiwamo shule na matibabu bure.
Sijui utasemaje kwa dhuluma kubwa inayofanywa na serikali yako hii kwa walalahoi. Wataamka tu.
Hao unaosema walidhulumiwa wanadai leo baada ya kuona serikali ni ya ubabaishaji, haina msimamo, kwa nini wasidai angalau wakati wa Mwinyi na Mkapa wadai leo? Huoni sababu ni kuwa serikali nayo ni ya kifisadi tu? Wanasema mvuna janga hula na wa kwao. Ndicho kinachotendeka

Hawa wananchi ndiyo walioteseka.

Nionyeshe picha moja tu ya "mwarabu koko" au mhindi "amekomeshwa" na Nyerere na anaishi maisha ya dhiki kama haya.

Mali zipi zilizodhulumiwa zilifika hapa kuwakomboa?

ImageUploadedByJamiiForums1433829221.058638.jpg
 
Back
Top Bottom