Kwa muktadha wa kichwa cha habari na kilichomo ndani ya bandiko lako na ukisoma pale nilipoweka wino mzito, bandiko lako linajikanganya sana, kimantiki na kisheria pia.
1. Operesheni hiyo ilifanywa na Serikali = hivyo hakutakuwa na "posthumous judgment" dhidi ya Serikali kwni Serikali haijafa na ni nadra sana kwa Serikali kufa. Na hata inapotokea mapinduzi au nchi mpya kuzaliwa kutoka nchi ya zamani na Seikali mpya kuingia/kuzaliwa, madeni na madai huendelea kuwapo na kudaiwa, "subject to the statute of limitation".
2. Kama ulimaanisha watu/watendaji waliofanya dhuluma hiyo, itakuwa ngumu kuwadai kwani walifanya wakiwa kazini, i.e in the course of emplyoment.
Kwa hiyo hoja yako inakosa msingi kwa mantiki ya mkanganyiko huo wa kisheria. Na kama ulimlenga Nyerere hapo ndio ngumu kabisa kwani ana kinga ya kikatiba.