KWA NINI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KILIMDHULUMU MWIGULU NCHEMBA HIVI KWA KUTOKUMFANYA AFANANE NA ALAMA ZA KI-TAALUMA HIZO ANAZOZIIMBA SANA?
Laiti Mwalimu wa Mwigulu Nchemba, pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, angefanikiwa kumrekebishia kijana huyu SPIDI ya kufikiri ikawa kubwa zaidi kuliko SPIDI ya kuongea sana mitaani, pengine hiyo 'A' yake anayoitembeza kila jukwaa ingepata maana na kutambulika zaidi hata bila ya yeye kulazimika kutumia nguvu nyingi mno kulitangaza katika jamii ya Tanzania.
Nasema Mtanzania yeyote hata yule ambaye hakuwahi kuona ndani ya darasa kunafananaje bado ANAO UWEZO wa kupambanua na kuelewa kwamba kama ndani ya Mwigulu kuna kitu alama ya 'A' kweli basi ni vema watu tukahoji uwezo wa aina ya watu aliokua nao darasani, uhusiano wake na huyo mwalimu mtoa alama isioridhisha jamii kabisa tena kwa vigezo vyote.
Naam, nasema wapo vijana wengi sana kote ndani ya CHADEMA, CCM, CUF na NCCR-Mageuzi ambao wala mtu hahitaji maelezo ya ziada juu yao kama waliwahi kuwa 'A'-Material au hapana.
Hakika kwa mtaji wa historia ambayo huyu kijana keshajiandikia kule kwenye uchaguzi mdogo Igunga, Arumeru Mashariki na hivi sasa pale sebuleni kwetu Dodoma; WaTanzania tuna maswali mengi mno juu yake kuliko majibu yanayopatikana hadi hivi sasa.
Ndio, ni matarajio ya jamii nzima kwamba Mtu mwenye alama za juu kitaaluma, popote duniani - matendo yake, ubunifu wa hali ya juu na matunda mazuri kwa jamii nzima, hoja maridhawa pamoja na aina ya lugha anayotumia kila wakati sirini au jukwaani bila shaka zitamtambulisha vema zaidi kuliko kitu kingine chochote kile.
Hata hivyo, Mwigulu Nchemba bado hajachelewa sana, kuna nafasi nyingine ya yeye mwenyewe kuweza kujifanyia tathmini binafsi na, pengine akiwa mkweli , huenda akatupongeza sisi vijana wenzake tunaomfanyia TATHMINI NA UPEMBUZI binafsi kwa lengo la kumjenga zaidi kuja kuwa kweli kiongozi anayetumainika.
Lakini kwa hivi sasa kwa huyu mwenzetu .... mmmmhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!