Tundu Lisu na Chadema wamfagilia kikwete bungeni, utadhani si hawa waliotoka nje wakidai hawamtambui... Hata hivyo ni ukomavu kisiasa, kumtambua Rais na nia yake njema ya kutaka nchi yetu ipate katiba nzuri kwa masilahi ya watanzania wote! Bravo Lisu, bravo Chadema kwa kuamua kula matapishi yenu... Mwendo mdundo
" Rais Kikwete ameonyesha uungwana na busara za hali ya juu sana, hakika ametoa muda wake mwingi kuhakikisha nchi yetu inapata katiba bora na safi kwa miaka ijayo, huu ni uzalendo na ukomavu mkubwa wa kiuongozi. Rais Kikwete anastahili pongezi"
Hafagilii ovyo huyo. Anafanya hiyvo ili kukata miguu ya magamba ambao walipanga kuukwamisha
hakutakiwi mbegu yyt ya kijani au njano kujipenyeza kwenye mchakato huu
huyu Machali baada ya kumsikiliza nimegundua kumbe chadema hawana wabunge walioiva, mbunge anazungumza kama yuko kwenye kikao cha wanachadema wakizungumza kishabiki, badala ya hoja, kashikilia uasi kutokubaliana na mapendekezo ya serikali.bunge si muhuri wa serikali wao wamepelekewa mswaada waujadili na waangalie kama kuna la kuzidisha wazidishe la kuondoa waondoe hio ndio kazi ya bunge. sasa kushinikiza wakubali kama ilivyo. ina maana gani kujadili? huyu jamaa bure kabisa. alau kidogo Mzee Arif ameongea kilogic unaweza kuhisi nn anakusudia kuzungumza
Machali yupo Nccr siyo Chadema kama unavyo sema.huyu Machali baada ya kumsikiliza nimegundua kumbe chadema hawana wabunge walioiva, mbunge anazungumza kama yuko kwenye kikao cha wanachadema wakizungumza kishabiki, badala ya hoja, kashikilia uasi kutokubaliana na mapendekezo ya serikali.bunge si muhuri wa serikali wao wamepelekewa mswaada waujadili na waangalie kama kuna la kuzidisha wazidishe la kuondoa waondoe hio ndio kazi ya bunge.
Hatimaye mapendekezo ya kambi ya upinzani kuhusu katiba mpya yapokelewa kwa makofi na kuondoa aibu wamesema ni maoni ya serikali duh kweli hatuna serikali kabisa.
Wanabodi,
Hatimaye ile sintofahamu kuhusu kuwasilishwa kwa muswada huu wa marekebisho madogo ya ule ile sheria ya Tume ya kukusanya maoni ya katiba, itamalizika rasmi leo asubuhi hii kwa muswada huo kuwasilishwa rasmi asubuhi hii katika kikao cha bunge.
Hata hivyo mjadala wa marekebisho hayo haitaanza kujadiliwa ili kutoa fursa kwa wabunge kujadili hoja ya dharura ya mgomo wa madaktari ambayo itawasilishwa leo na M/Kiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Magret Sitta.
Akitoa uthibitisho huo, Waziri wa Mahusiano ya Umma, Mhe. Stephen Wasira, ameiambia TBC leo asubuhi kuwa marekebisho hayo ni ya serikali na sio ya chama chochote!.
Nawasilisha.
Pasco.
Update:
Muswada umewasilishwa, maoni ya kamati ya bunge ya sheria na katiba pia yamewasilishwa.
Maoni ya kambi ya upinzani ndiyo yanawasilishwa, majadiliano yatafuatia.
NB, hoja yangu ya kuanza kwa hoja ya dharura ya kujadili mgomo wa madaktari, nimeshaitolea ufafanuzi kwenye ile thread yake.
kwa kweli kuhusu Mkuu wa wilaya kumuondoa inaonekana serikali na Chadema hawakujipanga, kiukweli umuhimu wake upo na ni mkubwa
Kusoma hawasomi hata kuona hawaoni halafu wanachangia mjadala!Mimi huwa sielewi CHADEMA wamewafanya nini nyie vichenchede!!!!!KAMA HUJUI KUSOMA, HATA PICHA HUONI?:yawn::yawn::yawn:
huyu Machali baada ya kumsikiliza nimegundua kumbe chadema hawana wabunge walioiva, mbunge anazungumza kama yuko kwenye kikao cha wanachadema wakizungumza kishabiki, badala ya hoja, kashikilia uasi kutokubaliana na mapendekezo ya serikali.bunge si muhuri wa serikali wao wamepelekewa mswaada waujadili na waangalie kama kuna la kuzidisha wazidishe la kuondoa waondoe hio ndio kazi ya bunge. sasa kushinikiza wakubali kama ilivyo. ina maana gani kujadili? huyu jamaa bure kabisa. alau kidogo Mzee Arif ameongea kilogic unaweza kuhisi nn anakusudia kuzungumza
Kiboko yake huyu hapa!!!Wanabodi,
Waziri wa Mahusiano ya Umma, Mhe. Stephen Wasira, ameiambia TBC leo asubuhi kuwa marekebisho hayo ni ya serikali na sio ya chama chochote!.
Nawasilisha.
Pasco.
Hafagilii ovyo huyo. Anafanya hiyvo ili kukata miguu ya magamba ambao walipanga kuukwamisha
esther amos bulaya anasema;
nampongeza tundu lissu kwa hotuba yake nzuri.
hii imeonyesha rais ndo kimbilio la kila mtu. na hii aliisema hapa na leo limedhihilika. mimi nilikuwa nawammbia solution sio kutoka nje bali kuyaongelea hapa kama tunavyo fanywa hapa. Kwanza naunga mkono hoja.
serikali itoe ufafanuzi wa kutosha kuhusu hii ya elimu kwa umma itafanyikaje. je kwa radio, tv au mihadhara? kuna wengine wataenda kufanya mikutano ya hadhara wakisema ni elimu kwa uma, natoa angalizo. by bulaya.
Sasa anaongea Mhe. Andrew Chenge, ambaye ni mmoja wa wabunge wachache wenye busara sana na uelewa wa hali ya juu kuhusu masuala ya kisheria.
Sasa anazungumza Mhe. Pindi Chana, huyu ni mmoja wa wabunge mahiri na makini ambaye kitaaluma ni mwanasheria mwenye LL.M, Tangu siku nyingi alistahili kuwa waziri, tatizo lake yuko too strict!, hakai mguu upande!, hivyo uwaziri hapati!
Angalizo, simaanishi kila anayeupata uwaziri ni lazima akae mguu upande!.
mwanasheria mkuu amesema anasoma mswaada wa katiba kwa mara ya pili. na mswaada utafanyiwa marekebisho katika kifungu cha 6, 12, 17, 18 na 21.
wanasiasa wataruhusiwa kushiriki, rais ndo ataretewa majina ambayo atayapendekezwa, vikundi, taasisi na asasi zitaruhusiwa kuandaa mikutano baada ya kutoa taarifa. athabu isiopungua milioni 2 na isiozidi milion 5 baadala ya ile ya milion 5 hadi 15. na mwaka 1 hadi 3. katoa hoja na hoja hiyo imeungwa mkono.