Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!

tundu; kwa maana hiyo mswaada huu unaonyesha uso wa watanzania na si rais na chadema peke yake ndo imeshinikiza kama inavyosemwa. rais alitumia siku nne na kukaa hadi saa sita usiku akijadili jambo hilo. hiyo inaonyesha rais anataka hili jambo lipewe kipaumbele.
Ni kweli mswaada huu umeletwa hata kabla miezi 3 kupita. ni kweli kipindi hiki ni kifupi sana. kuna watakaosema kitendo hiki ni ni dharau kwa bunge. lakini katiba yetu haijaweka kipindi cha kulekebisha mswaada.
 
Nimependa paragraph ya kwanza inavyokumbushia jinsi utawala wa Mchonga ulivyoingiza tabia za kihuni, kishenzi, na kimabavu za kutunga taratibu zilizo nje ya sheria na katiba. Sungusungu walinyanyasa sana watu.


Sungu sungu wali restore law and order. Walikuwa wakiogopwa sana.
 
That's very true and let them [CCM's MPS] be ashamed. Sasa hatuko kwenye siasa za kufurahishana na kubebana hapa while watanzania wanahangaika na maisha magumu. Dawa yao 2015 tu hawa....
 
Update:

Muswada umewasilishwa, maoni ya kamati ya bunge ya sheria na katiba pia yamewasilishwa.
Maoni ya kambi ya upinzani ndiyo yanawasilishwa, majadiliano yatafuatia.
 
Tundu Lisu na Chadema wamfagilia kikwete bungeni, utadhani si hawa waliotoka nje wakidai hawamtambui... Hata hivyo ni ukomavu kisiasa, kumtambua Rais na nia yake njema ya kutaka nchi yetu ipate katiba nzuri kwa masilahi ya watanzania wote! Bravo Lisu, bravo Chadema kwa kuamua kula matapishi yenu... Mwendo mdundo
" Rais Kikwete ameonyesha uungwana na busara za hali ya juu sana, hakika ametoa muda wake mwingi kuhakikisha nchi yetu inapata katiba bora na safi kwa miaka ijayo, huu ni uzalendo na ukomavu mkubwa wa kiuongozi. Rais Kikwete anastahili pongezi"
 
Du! kwa mara ya kwanza kuona upinzani wakisifia raisi wa ccm kiasi hiki.ni ktk hotuba yake ya mswaada wa sheria ya kuunda tume ya katiba mpya.hapa sifa hizi ni kwa sababu raisi amechukua mawazo yao? Au kuna makubaliano ya chini chini
 
>Anazungumzia mabadiliko ya katiba.
>Amsifia Jk kukubali kusaini machanges ya katiba.
>Awaponda wanaomsema vibaya jk kuhusu kukubali mabadiliko pia kuonana na vyama vya upinzani.
>Anawasilisha mswada wa machanges kupitia vyama vya upinzani.
>MENGINEYO YANAYOCONTINUE 2TAWAJUZENI.
>ATAKAYEDAKA MAPOINT MENGINE AYAADD HAPA WATZ WAKNOW.
 
tundu;
watu ambao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa ni wabunge na wanabaraza wa zanzibar.
kuwaondoa wanasiasa ilikua ni kosa kwani iliwatenga watu wenye sifa na uzoefu wa kazi hii. kambi rasmi bungeni inalidhika na marekebisho ya mswaada kifungu 6a.
 
Du! kwa mara ya kwanza kuona upinzani wakisifia raisi wa ccm kiasi hiki.ni ktk hotuba yake ya mswaada wa sheria ya kuunda tume ya katiba mpya.hapa sifa hizi ni kwa sababu raisi amechukua mawazo yao? Au kuna makubaliano ya chini chini
Nahisi hawa wapinzani hawakuwa wanamjua jk vizuri , baada ya upinzani kuwa karibu nao sasa ndio wameelewa kuwa jk ni jembe, ila wabunge wake ndio janga.
 
Mode, badili headline, andika Bungeni Live: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!.
 
wakuu ntaandika kwa ufupi sababu haya maneno tindu lissu anayo yaongea yatawekwa hapa mda si mlefu so ntaandika kwa jujuu.
 
Ama kweli huyu Kamanda yupo makini

Anapangua mapendekezo vipengele kwa vipengele!
Ama kwl upinzani upo bungeni!
 
tundu; itaandikwa kwenye historia "rais kikwete ndo rais wa kwanza tanzania kukubali katiba ya wananchi na sio katiba ya rais".
 
Back
Top Bottom