Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!

Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!

kilango apendekeza wakuu wa wilaya warudishwe kwenye tume badala ya wakurugenzi
 
nina wasiwasi huko field watakapoanza kuimplement hii sheria wapinzani wasije kulia,..jk hatabiliki,hiyo misifa wanayomwaga..mmmh
 
esther amos bulaya anasema;
nampongeza tundu lissu kwa hotuba yake nzuri.
hii imeonyesha rais ndo kimbilio la kila mtu. na hii aliisema hapa na leo limedhihilika. mimi nilikuwa nawammbia solution sio kutoka nje bali kuyaongelea hapa kama tunavyo fanywa hapa. Kwanza naunga mkono hoja.
serikali itoe ufafanuzi wa kutosha kuhusu hii ya elimu kwa umma itafanyikaje. je kwa radio, tv au mihadhara? kuna wengine wataenda kufanya mikutano ya hadhara wakisema ni elimu kwa uma, natoa angalizo. by bulaya.
 
Bulaya; hiki kifungu cha elimu kwa umma kiwekwe wazi kwamba kule lissu anakoenda hakuna mtu mwingine. naungana na ana kilango juu ya mkuu wa wilaya. je mkuu wa wilaya sio mwanasiasa? mkuu wa wilaya ndio anatoa vibari coz yeye ndio mkuu wa usalama. nampongeza rais na naendelea kusema katiba nzuri itatoka bungeni. naunga mkono hoja by bulaya.
 
Mhe. Mnyaa amezungumza, ameunga mkono hoja. Sasa anachangia Mhe. Mama Kilango, amsifu Lissu kwa kuchangia kistaarabu sana!.
Atoa fungo "Jambo la Shari Limeleta Heri", ile shari ya wenzetu ambao walikuwa hawamtambui rais Jakaya Kikwete, imegeuka heri kwa kumtambua JK kuwa ndiye rais wa JMT!, anapigiwa makofi. Mhe. Ester Bulaya amechangia kwa kumpongeza Lissu na baada ya hapo kumpiga vijembe!
 
Tundu Lisu na Chadema wamfagilia kikwete bungeni, utadhani si hawa waliotoka nje wakidai hawamtambui... Hata hivyo ni ukomavu kisiasa, kumtambua Rais na nia yake njema ya kutaka nchi yetu ipate katiba nzuri kwa masilahi ya watanzania wote! Bravo Lisu, bravo Chadema kwa kuamua kula matapishi yenu... Mwendo mdundo
" Rais Kikwete ameonyesha uungwana na busara za hali ya juu sana, hakika ametoa muda wake mwingi kuhakikisha nchi yetu inapata katiba bora na safi kwa miaka ijayo, huu ni uzalendo na ukomavu mkubwa wa kiuongozi. Rais Kikwete anastahili pongezi"

Chadema hawajawahi kusema kwamba hawamtambui Rais. Pia si vibaya kumsifia mtu anapofanya jambo zuri hata kama kuna mambo mengine mengi hukubaliani naye. Kumpongeza Rais kwa kukubali kufanya marekebisho kwenye mswada huu ni jambo jema kwa manufaa ya Taifa na wala siyo chama.
 
Said Amour Arfi wa chadema anasema;
tuwe kitu kimoja katika hili. namshukuru rais kwa kusikia kelele zilizokuwa zinapigwa nje ya ukuta huu wa bunge. kama heshima zisipotamaraki katika jambo hili la msingi tunaweza kuligawa taifa hili vipande. mapendekezo yaliyoletwa na serikali yamepitiwa na wataaramu wa kila aina. sikubaliani na Kilango. katiba si mali ya chama chochote. mkuu wa wilaya tunawajuwa utendaji wao ndo maana wakatolewa. na hii itafanya watu wajue hii ni katiba ya watanzania. by Arfi
 
Naangalia bunge lakini naona wabunge walioongea hadi sasa wa ccm wanajadili swala la kumtambua rais badala ya hoja iliyowekwa mezani.du bulaya easter nilikua namheshimu lakin nimeona leo jinsi anavyoacha kuzungumza hoja za msingi na kuanza vijembe(udaku).du kweli hawa hawaangalii maslahi ya taifa.mjadala wa mabadiliko ya katiba mpya.kaz kwenu wakuu
 
Sasa anaongea said arfi cdm,kama kawaida yake kwa busara yake anaunga mkono busara iliyotumika na anawasihi wabunge wakubaliane na wakuu wa wilaya wasisimamie ukusanyaji maoni
 
Wanajamvi,

Wakati akiwasilisha hotuba ya marekebisho ya sheria ya kuandaa katiba mpya msoma hotuba hiyo kwa niaba ya Waziri wa katiba na sheria alianza kumshukuru mwenyekiti wa kamati na makamu wake na kisha akamshukuru rais. Hakumshukuru waziri kivuli wa katiba na sheria japo hata mtoto wa darasa la kwanza anajua mchango wa huyu waziri kivuli katika kufanikisha marekebisho haya. Je, ni chuki binafsi?
 
Guys,

What we really need is a good katiba for the people regardless of chama.
Tukianza kuchochea CCM or Chadema or CUF, hao wanasiasa watazidi kukomoana kichama, in turn sie ndio tutaimia in the end just because CCM atapinga mapendekezo ya CDM sababu ya kuwakomoa tu hata kama ni mapendekezo mazuri.
Tuwasaidie wabunge wetu regardless of chama kupitisha vipengere bora vyenye manufaa kwa nchi na si chama.
 
Arfi anasema;
mimi nilikuwepo kwenye mazungumzo. wakuu wa wilaya tuliwatoa kwenye mchakato kwa sababu wanaonekana kwenye katiba ya ccm toleo la 2010 kifungu cha 80.1c na 78.1c. hatutaki watu waje waseme hii katiba ni ya watu wa aina fulani. by Arfi
 
Mh mwenyekiti msaidizi cdm apinga mkuu wilaya kurudishwa kwenye tume kwani katiba ni ya Tanznia co ya chama lakini mkuu wa wilaya ameonekana kwenye katiba ya CCM ya 2010 sasa mkuu wa wilaya atasimamia maslahi ya nani?
Saidi Arfi amepresent vizuri sana...kweli cdm hawabahatishi nafikiri mbunge yeyote wa ccm atakayeliongelea hilo tena basi atakuwa mbishi sana m/kiti hakubahatisha
 
andrew chenge anaongea naona anaanza kuwaponda chadema walivyotokaga bungeni
 
Sasa anaongea Mhe. Andrew Chenge, ambaye ni mmoja wa wabunge wachache wenye busara sana na uelewa wa hali ya juu kuhusu masuala ya kisheria.
 
Back
Top Bottom