Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!

Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!

Kwa nini mkuu wa wilaya anang'ang'aniwa na hawa wenye magamba???wanajulikana wanateuliwa na raisi na watalinda kile boss wao atakachowaambia wafanye,Wabunge CDM kazeni uzi hao wakuu wa wilaya ni mamluki wa raisi watachakachua mchakato mzima wa katiba mpya.
 
Mbowe anaongea sasa..anamshukuru raisi kwa kuleta muswada tena ..unapongeza jinsi wabunge walivyoshirikiana katika kujadili mswada..anasema nafasi ya maDC wasiingie katika tume ya katiba kwa sababu ni wenyeviti wa ccm wa wilaya katika kamati ya siasa ya ccm ya wilaya, anaendelea DED anafaa kwa sababu yeye ni mkuu wa structual yote ya utendaji ndani ya wilaya akishilikiana na madiwani ambao ni wawalishi wa wananchi..kamaliza.
 
Hawa Wabunge mbona kila mtu anadai marekebisho ya serikali ni yake? Mfano ni huyu Jaffo na Serukamba. Pole sana Wabunge wa Chichiemu
 
Mdee anapinga wakuu wa wilaya kuingia kwenye mchakato wa katiba anashauri ded waingie kwenye mchakato wa katiba
 
Wakuu wa wilaya wafutiliwe mbali, wako hapo kwa itikadi za kisiasa zaidi..
 
Wabunge wa ccm hawachambui kifungu kwa kifungu wanapiga siasa tu bungeni na kumsifia rais
 
Kwa ujumla wabunge ccm wanataka wakuu wa wilaya wawe wasimamizi wa mchakato wa katiba na chadema wanataka DED Ndio wawe wasimamizi wa mchakato wa katiba, hapo ndipo kuna malumbano makubwa ya hoja..
 
Mwaka 1984 Jaji Mkuu, Francis Nyalali alifikia kikomo cha uvumilivu kwa jinsi nchi inaendeshwa huku sheria na haki zikipuuzwa. Kwa mfano wakati huo askari na mahakama ambazo hazitambuliwi na katiba na sheria au katiba zilishika hatamu wakiitwa kwa jina “Sungusungu”.

Nyalali alivyoona hivyo hakutaka kubishana na Nyerere. Alimfuata Msasani akamuambia kwamba anataka ku-resign kwa sababu mambo yanaendeshwa bila kufuata sheria hivyo yeye kama Jaji Mkuu, mhimili wake hauna kazi ya kufanya.

Nyerere akaongea naye kwa kirefu na siku hiyo kulikuwa kumebaki siku kadhaa Halmashauri ya CCM (NEC) ilikuwa inafanyika. Nyerere akamuambia atamkaribisha ili aeleze hali hiyo kwenye NEC. Siku ya NEC ikafika. Nyalali akajieleza ile mbele ya NEC ila hakusema alitaka kujiuzuru maana hiyo ikawa ni siri yake na Nyerere.

Nyalali alipomaliza maelezo, alipomaliza akawaacha NEC na Nyerere waendelee na ajenda zingine yeye akarudi kwenye kazi zake za Ujaji Mkuu.

Sijui kilijadiliwa nini huko nyuma baada ya kuondoka Nyalali, lakini inaelekea kulikuwa na ulazima wa kumutia tena Nyalali katika kikao kingine kinachofuata cha NEC. Kwenye masimulizi yake mwenyewe Nyalali yaliyochapishwa kwenye RAI mwishoni mwa 1990s na kurudiwa baada ya kifo chake, Nyalali anasema kwamba aliamua hii mara ya pili asiende peke yake, bali akaita majaji wengine wawili wakamsaidie kutoa ufafanuzi wa jinsi gani kila mtu anavyotakiwa kuishi kwa kuongozwa na sheria na si vinginevyo. Maana alihisi kwenye kikao cha kwanza zilijitokeza dalili za wajumbe kutokumuelewa.

Siku ikafika, Nyalali akatinga na majaji wenzake kwenye NEC. Nyerere akafungua kikao na kina Nyalali wakaaza kufafanua kwamba kila mtu hapa nchini anatakiwa kuishi kwa kufuata ssheria yaani hakuna aliye juu ya sheria. Walipomaliza ikaja zamu ya wajumbe wa NEC kutoa maoni yao.

Kabla sijasema walisema nini tujikumbushe kwamba wakati huo na hata sasa NEC ilikuwa na watu kadhaa ambao professional lawyers. NEC ilikuwa ngazi ya kupatia vyeo kama uwaziri kama ilivyo sasa. Hivyo, NEC ilikuwa imesheheni wanasheria na wanahistoria ambao kwenye proeffesssion zao wanajua wazi kwamba kila mtu hata Rais lazima aishi kwa kufuata sheria.

Sasa, tuone wajumbe wa NEC wakiwemo hwa wanasheria wali-react vipi kulingana na maelezo ya Nyalali na wenzake. Wajumbe wengi waliwashambulia vibaya sana Nyalali na wenzake. Walioongoza mashambulizi si watu mbumbumbu, bali ni wasomi wazuri wa sheria. Mmoja alidiriki kusema hivi “Sasa mnakuja hapa kutuambia kuwa kila mtu anatakiwa kuwa chini ya sheria, je, kwa maana hiyo hata Rais Nyerere mnataka atawaliwe na sheria??!!”

Wakati ule kulikuwa bado kuna Preventive Detention Act yaani rais alikuwa amepewa uwezo wa kumtia mtu kizuizini. Hivyo, palepale wajumbe kadhaa wakaleta hoja wakimuomba Nyerere kwamba huyu Nyalali na wenzake wawekwe kizuizini.

Nyerere aliacha uwanja mpana na akahakikisha wote wametoa dukuduku lao. Kikubwa ni kwamba Asilimia kubwa ya NEC hawakukubaliana na anachosema Nyalali na wenzake. Lakini wajumbe hawakujua kuwa Nyerere ndiye aliyemzuia Nyalali kujiuzuru na ukumbuke hiyo ni miaka mitano baada ya Edwin Mtei kujiuzuru kwa kutofautiana na Nyerere kwa mambo mengine. Si sheria bali uchumi.

Je, baada ya wote kusema , unadhani hadi hapa Nyerere alikuja na jibu gani? Nyerere alifunga mjadala kwa njia ambayo wajumbe hawakuamni na wakaaibika.
Alifunga mjadala kwa jibu fupi sana kwa kusema “Ndugu wajumbe, kuanzia sasa kila binadamu nchini Tanzana hatakuwa juu ya sheria, kila mtua atakuwa chini ya sheria na tunalazimika kuongozwa na sheria”

Nyalali anasema alifarijika na ndilo jibu lililomfanya afute wazo la kujiuzuru na aendelee kuwa Jaji Mkuu hadi alipostaafu. Ila anasema, hakuamini macho na masikio ndani ya NEC kuona wajumbe waliochachamaa ni wale ambao ni wasomi wazuri wa sheria lakini wanahoji kwa nini wanasiasa, mawaziri na rais wawe chini ya sheria.

Nyalali anasema, wasomi hao walikuwa wanasaliti taaluma yao kwa kujipendekeza kwa Nyerere bila aibu lakini wakaumbuliwa na jibu la Nyerere.

Sasa, tuje kwenye Muswada huu wa Katiba. Tuliona CHADEMA wakitoka nje kwa sababu ya ubovu wake. Lakini wabunge wa CCM wakaushangilia na kuuona safi. BInafsi nilimshuhudia Mh. Angelah Kairuki akijadili kana kwamba si mwanasheria wakati hadi sasa yuko Sabatic Leave kama State Attorney.

CHADEMA wakaona waende kumuona Rais Kikwete kama Nyalali alvyoenda kumuona Rais Nyerere. Nyerere akaona kweli hali ya Chama kushika hatamu na viongozi kuwa juu ya sheria ni upuuzi mtupu. Tumeona Nyerere alivyoitisha NEC kujadili hoja ya Nyalali. Wajumbe wa NEC badala ya kujadili hoja wakaanza kumjadili na kumkebehi Nyalali mbele ye Nyerere wakidhani kwa kufanya hivyo wanamfutahisa Nyerere.

Haina tofauti na wabunge wa CCM ambao waliutetea Muswada mbovu wakidhani wanamfurahisha Kikwete, sasa Kikwete kaamua kuleta marekebsho. Kuletwa kwa marekebisho maana yake wabunge wa CCM wameumbuka kama walivyoumbuka wale wajumbe wa NEC,

Hadi hapa nimemaliza maelezo yanakuja maoni yangu. Aoni yangu ni kwamba mazoea ya kuishi kwa kujipendekeza kwa bosi yoyote kujikubali kwamba wewe mwenyewe ni dhaifu.
Siamini kama wabunge wa CCM waliosoma Sheria kama wangepelekewa Muswada ule kwenye University Exam wangekuja na majibu ovyo kama waliyokuwa wanayatoa bungeni siku wanaupitisha. Hili ndilo lilikuwa kosa lao kama lilivyokuwa NEC members against Nyalali.

Walichofanya CHADEMA kwenda Ikulu wala hakikuwa kigumu kwa msomi yoyote. Hata Ridhiwani Kikwete ambaye ni mwanasheria kwa taaluma yake angejibu sawa na CHADEMA walivyotaka maana CHADEMA walisimama kwenye profession base na hapo hakuna Rais yoyote wa dunia hii angewakatalia hoja yao, achilia mbali.

Sasa, kuna mawazo kwamba wabunge wa CCM wanaona aibu kwamba wenzao CHADEMA ni vipanga. Ukweli ni kwamba haya wameyataka wenyewe kwani ni ukweli kwamba wamo baadhi yao ni lecturers wa profession mbalimbali ikiwemo sheria na sidhani kama hili walishindwa kuliona.

Hivyo, zama za kufanya siasa za kuukwepa ukweli zimepitwa. CCM au chama chochote wakiukwepw ukweli basi CHADEMA watautumia ukweli huo na jamii itawaheshimu kuwa ni wasomi na wataumbuka.

Jadili

Thanks dude...jf zaidi ya habari..
 
Olesendeka anamshukuru tundu lisu anasema ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kisheria na mpiganaji shupavu amesifia hotuba yake nzuri
 
Kiboko yake huyu hapa!!!
Tundu-Lisu.jpg

Huyu jamaa mbona mchemfu sana kule bungeni wanamwita ' MCHICHA MWIBA' mwisho wa kunukuu
 
Jioni hii nimeshuhudia wabunge wawili wa magamba wakimpa salute Tundu Lissu kwa umahiri wake..

Kaanza Sendeka: "kwa moyo wa dhati kabisa natambua upeo wako mkubwa, uwezo wako wa kuchambua sheria.. unastahili pongezi"

Lukuvi: "Nampongeza sana Tundu Lissu kwa uwezo wake kisheria. Haya mambo ni mengi lakini ameweza kuyachambua vizuri"

My take: Sifa zikiwa nyingi huwa si nzuri sana, je ataendelea kuperform as expected?
 
Mheshimiwa Lissu,Leo nimekuangalia TBC wakati unatoa Maoni ya Kambi ya Upinzani,kwa kweli umeongea vizuri sana na kuwasilisha Hotuba yako vyema,nilipata Mstuko kdg ulipoanza kumsifia Rais na kikubwa Zaidi KUUNGA MKONO Hoja,ila ungesoma Vizuri alama zao Usingeunga Mkono hoja wao Wangeunga..
MY TAKE: Ukienda kulia wao wanaenda kushoto
 
huyu jamaa alipewa heshima na wamarekani kwa umahili wake,wanamagamba wote pale bungeni wanamuheshimu ila basi tu hawasemi.
 
Back
Top Bottom