Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bungeni: Muswada wa Katiba Unajadiliwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 9, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,210
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,


  Hatimaye ile sintofahamu kuhusu kuwasilishwa kwa muswada huu wa marekebisho madogo ya ule ile sheria ya Tume ya kukusanya maoni ya katiba, itamalizika rasmi leo asubuhi hii kwa muswada huo kuwasilishwa rasmi asubuhi hii katika kikao cha bunge.


  Hata hivyo mjadala wa marekebisho hayo haitaanza kujadiliwa ili kutoa fursa kwa wabunge kujadili hoja ya dharura ya mgomo wa madaktari ambayo itawasilishwa leo na M/Kiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Magret Sitta.


  Akitoa uthibitisho huo, Waziri wa Mahusiano ya Umma, Mhe. Stephen Wasira, ameiambia TBC leo asubuhi kuwa marekebisho hayo ni ya serikali na sio ya chama chochote!.


  Nawasilisha.  Pasco.
  Update:


  Muswada umewasilishwa, maoni ya kamati ya bunge ya sheria na katiba pia yamewasilishwa.
  Maoni ya kambi ya upinzani ndiyo yanawasilishwa, majadiliano yatafuatia.


  NB, hoja yangu ya kuanza kwa hoja ya dharura ya kujadili mgomo wa madaktari, nimeshaitolea ufafanuzi kwenye ile thread yake.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  What is new katika mswada huu?

  Hacha kuwaadaa watanzania
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kuna element ya ubabaishaji sana katika kuwasilisha hoja, yaani spika amekaa kisiasa zaidi. Alikuwa wapi siku zote kuruhusu hiyo hoja ya dharura ya mgomo wa madokta mpaka leo hii?


   
 4. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Spika anatakiwa awajibike kwa kukataa kujadilì hoja ya mgomo
   
 5. F

  Fikra chanya Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  'Hassira' - waziri wa mahusiano, nani asiyejua mabadiliko haya yametokana na chadema, kwani nyie si mlipitisha vile vile(ndiyo mzee) hapo awali?, siku hizi si kama enzi za mwalimu, tunamiliki TV na Radio zetu, tunafuatilia kwa umakini kinachoendelea bungeni, mheshimiwa utajuaje na huwa unalala?
   
 6. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hillo nalo neno kwenye red hapo,AMEAMKA SAA NGAPI?
   
 7. k

  kiche JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mswada ulikuwa wa serikali hayo marekebisho serikali wameyatoa wapi??hata hivyo la msingi ni mabadiliko yawe yametoka cdm au taasisi yoyote lakini yana lengo la kurekebisha ni jambo zuri,ccm walifikiri kuwa wanaandaa katiba ya chama!!!
   
 8. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mwaka 1984 Jaji Mkuu, Francis Nyalali alifikia kikomo cha uvumilivu kwa jinsi nchi inaendeshwa huku sheria na haki zikipuuzwa. Kwa mfano wakati huo askari na mahakama ambazo hazitambuliwi na katiba na sheria au katiba zilishika hatamu wakiitwa kwa jina “Sungusungu”.

  Nyalali alivyoona hivyo hakutaka kubishana na Nyerere. Alimfuata Msasani akamuambia kwamba anataka ku-resign kwa sababu mambo yanaendeshwa bila kufuata sheria hivyo yeye kama Jaji Mkuu, mhimili wake hauna kazi ya kufanya.

  Nyerere akaongea naye kwa kirefu na siku hiyo kulikuwa kumebaki siku kadhaa Halmashauri ya CCM (NEC) ilikuwa inafanyika. Nyerere akamuambia atamkaribisha ili aeleze hali hiyo kwenye NEC. Siku ya NEC ikafika. Nyalali akajieleza ile mbele ya NEC ila hakusema alitaka kujiuzuru maana hiyo ikawa ni siri yake na Nyerere.

  Nyalali alipomaliza maelezo, alipomaliza akawaacha NEC na Nyerere waendelee na ajenda zingine yeye akarudi kwenye kazi zake za Ujaji Mkuu.

  Sijui kilijadiliwa nini huko nyuma baada ya kuondoka Nyalali, lakini inaelekea kulikuwa na ulazima wa kumutia tena Nyalali katika kikao kingine kinachofuata cha NEC. Kwenye masimulizi yake mwenyewe Nyalali yaliyochapishwa kwenye RAI mwishoni mwa 1990s na kurudiwa baada ya kifo chake, Nyalali anasema kwamba aliamua hii mara ya pili asiende peke yake, bali akaita majaji wengine wawili wakamsaidie kutoa ufafanuzi wa jinsi gani kila mtu anavyotakiwa kuishi kwa kuongozwa na sheria na si vinginevyo. Maana alihisi kwenye kikao cha kwanza zilijitokeza dalili za wajumbe kutokumuelewa.

  Siku ikafika, Nyalali akatinga na majaji wenzake kwenye NEC. Nyerere akafungua kikao na kina Nyalali wakaaza kufafanua kwamba kila mtu hapa nchini anatakiwa kuishi kwa kufuata ssheria yaani hakuna aliye juu ya sheria. Walipomaliza ikaja zamu ya wajumbe wa NEC kutoa maoni yao.

  Kabla sijasema walisema nini tujikumbushe kwamba wakati huo na hata sasa NEC ilikuwa na watu kadhaa ambao professional lawyers. NEC ilikuwa ngazi ya kupatia vyeo kama uwaziri kama ilivyo sasa. Hivyo, NEC ilikuwa imesheheni wanasheria na wanahistoria ambao kwenye proeffesssion zao wanajua wazi kwamba kila mtu hata Rais lazima aishi kwa kufuata sheria.

  Sasa, tuone wajumbe wa NEC wakiwemo hwa wanasheria wali-react vipi kulingana na maelezo ya Nyalali na wenzake. Wajumbe wengi waliwashambulia vibaya sana Nyalali na wenzake. Walioongoza mashambulizi si watu mbumbumbu, bali ni wasomi wazuri wa sheria. Mmoja alidiriki kusema hivi “Sasa mnakuja hapa kutuambia kuwa kila mtu anatakiwa kuwa chini ya sheria, je, kwa maana hiyo hata Rais Nyerere mnataka atawaliwe na sheria??!!”

  Wakati ule kulikuwa bado kuna Preventive Detention Act yaani rais alikuwa amepewa uwezo wa kumtia mtu kizuizini. Hivyo, palepale wajumbe kadhaa wakaleta hoja wakimuomba Nyerere kwamba huyu Nyalali na wenzake wawekwe kizuizini.

  Nyerere aliacha uwanja mpana na akahakikisha wote wametoa dukuduku lao. Kikubwa ni kwamba Asilimia kubwa ya NEC hawakukubaliana na anachosema Nyalali na wenzake. Lakini wajumbe hawakujua kuwa Nyerere ndiye aliyemzuia Nyalali kujiuzuru na ukumbuke hiyo ni miaka mitano baada ya Edwin Mtei kujiuzuru kwa kutofautiana na Nyerere kwa mambo mengine. Si sheria bali uchumi.

  Je, baada ya wote kusema , unadhani hadi hapa Nyerere alikuja na jibu gani? Nyerere alifunga mjadala kwa njia ambayo wajumbe hawakuamni na wakaaibika.
  Alifunga mjadala kwa jibu fupi sana kwa kusema “Ndugu wajumbe, kuanzia sasa kila binadamu nchini Tanzana hatakuwa juu ya sheria, kila mtua atakuwa chini ya sheria na tunalazimika kuongozwa na sheria”

  Nyalali anasema alifarijika na ndilo jibu lililomfanya afute wazo la kujiuzuru na aendelee kuwa Jaji Mkuu hadi alipostaafu. Ila anasema, hakuamini macho na masikio ndani ya NEC kuona wajumbe waliochachamaa ni wale ambao ni wasomi wazuri wa sheria lakini wanahoji kwa nini wanasiasa, mawaziri na rais wawe chini ya sheria.

  Nyalali anasema, wasomi hao walikuwa wanasaliti taaluma yao kwa kujipendekeza kwa Nyerere bila aibu lakini wakaumbuliwa na jibu la Nyerere.

  Sasa, tuje kwenye Muswada huu wa Katiba. Tuliona CHADEMA wakitoka nje kwa sababu ya ubovu wake. Lakini wabunge wa CCM wakaushangilia na kuuona safi. BInafsi nilimshuhudia Mh. Angelah Kairuki akijadili kana kwamba si mwanasheria wakati hadi sasa yuko Sabatic Leave kama State Attorney.

  CHADEMA wakaona waende kumuona Rais Kikwete kama Nyalali alvyoenda kumuona Rais Nyerere. Nyerere akaona kweli hali ya Chama kushika hatamu na viongozi kuwa juu ya sheria ni upuuzi mtupu. Tumeona Nyerere alivyoitisha NEC kujadili hoja ya Nyalali. Wajumbe wa NEC badala ya kujadili hoja wakaanza kumjadili na kumkebehi Nyalali mbele ye Nyerere wakidhani kwa kufanya hivyo wanamfutahisa Nyerere.

  Haina tofauti na wabunge wa CCM ambao waliutetea Muswada mbovu wakidhani wanamfurahisha Kikwete, sasa Kikwete kaamua kuleta marekebsho. Kuletwa kwa marekebisho maana yake wabunge wa CCM wameumbuka kama walivyoumbuka wale wajumbe wa NEC,

  Hadi hapa nimemaliza maelezo yanakuja maoni yangu. Aoni yangu ni kwamba mazoea ya kuishi kwa kujipendekeza kwa bosi yoyote kujikubali kwamba wewe mwenyewe ni dhaifu.
  Siamini kama wabunge wa CCM waliosoma Sheria kama wangepelekewa Muswada ule kwenye University Exam wangekuja na majibu ovyo kama waliyokuwa wanayatoa bungeni siku wanaupitisha. Hili ndilo lilikuwa kosa lao kama lilivyokuwa NEC members against Nyalali.

  Walichofanya CHADEMA kwenda Ikulu wala hakikuwa kigumu kwa msomi yoyote. Hata Ridhiwani Kikwete ambaye ni mwanasheria kwa taaluma yake angejibu sawa na CHADEMA walivyotaka maana CHADEMA walisimama kwenye profession base na hapo hakuna Rais yoyote wa dunia hii angewakatalia hoja yao, achilia mbali.

  Sasa, kuna mawazo kwamba wabunge wa CCM wanaona aibu kwamba wenzao CHADEMA ni vipanga. Ukweli ni kwamba haya wameyataka wenyewe kwani ni ukweli kwamba wamo baadhi yao ni lecturers wa profession mbalimbali ikiwemo sheria na sidhani kama hili walishindwa kuliona.

  Hivyo, zama za kufanya siasa za kuukwepa ukweli zimepitwa. CCM au chama chochote wakiukwepw ukweli basi CHADEMA watautumia ukweli huo na jamii itawaheshimu kuwa ni wasomi na wataumbuka.

  Jadili
   
 9. cjilo

  cjilo JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  msawad wamarekebisho ya katiba unawasilishwa ss bungeni
   
 10. a

  ansynshoba Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jaji werema soon ameanza kuusoma muswada wa mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011.
  source tbc1
   
 11. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Nimependa paragraph ya kwanza inavyokumbushia jinsi utawala wa Mchonga ulivyoingiza tabia za kihuni, kishenzi, na kimabavu za kutunga taratibu zilizo nje ya sheria na katiba. Sungusungu walinyanyasa sana watu.
   
 12. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,068
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  mwanasheria mkuu amesema anasoma mswaada wa katiba kwa mara ya pili. na mswaada utafanyiwa marekebisho katika kifungu cha 6, 12, 17, 18 na 21.
  wanasiasa wataruhusiwa kushiriki, rais ndo ataretewa majina ambayo atayapendekezwa, vikundi, taasisi na asasi zitaruhusiwa kuandaa mikutano baada ya kutoa taarifa. athabu isiopungua milioni 2 na isiozidi milion 5 baadala ya ile ya milion 5 hadi 15. na mwaka 1 hadi 3. katoa hoja na hoja hiyo imeungwa mkono.
   
 13. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Tujuze zaidi mkuu!!
   
 14. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,068
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  kamati ya katiba inamshukuru rais kwa kusaini mswaada wa katiba. wanasema waliita watu / wadau mbele ya kamati ili kutoa maoni yao.
   
 15. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,068
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  yesi ngoja nijipange. ntawajuza kwenye michango itakayo tolewa. wabunge wote wapo, hakuna aliyetoka nje wala kuguna. ntawajuza michango ikishaanza
   
 16. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  vyama vimetajwa including ccm lakini chadema hakijatajwa, hapa sijaelewa vizuri
   
 17. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Umemsahau Wakili maarufu na mmiliki wa Shule ya St Anne Marie Mhe Jason nRweikiza naye pia ni mbunge kupitia CCM lakini akisimama huwa anaongea pu,ba tupu utafikiri mmachinga.
   
 18. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wana JF baada ya kuiskia Kamati ya kudumu ya Bunge sasa nangoja Kuskia Maporomoko ya Marekebisho ya Muswada wa Katiba toka kwa TUNDU lissu..
   
 19. fikrapevu sungura

  fikrapevu sungura Senior Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shwari endelea kuleta full details.
   
 20. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,068
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  tundu lissu ndo anasoma kuhusu mswaada huu kwa upande wa upinzani. anasema;
  18/11/2011 bunge lilipitisha mswaada. sheria ilianza kutumika 1/12/2011.
  tumekutana leo hii ili Bunge liweze kupitia tena. 20/11/2011 chadema iliunda kamati ya kuonana na rais. 27/11/2011 ndo siku rais alikutana na chadema kwa masaa 3 na kesho yake masaa 8. vilevile rais alikutana na nccr, cuf na vikundi mbalimbali ikiwemo ccm iliyotoa mapendekezo 8.
   
Loading...