Bungeni: Mbowe aweka msimamo wa posho

Bungeni: Mbowe aweka msimamo wa posho

Mheshimiwa sokomoko hili suala lako ni jipya na muhimu sana labda ungeazisha thread yako ingekuwa na maana zaidi ili watu waijadili kwa mapana yake

Mkuu hizi elfu sabini kwa wabunge hazifiki hata nusu bilioni kwa miaka mitano ila kwa makusudi wanasiasa wanatufanya sisi mazezeta. Si ulimwona kitila alikuwa kwenye hii sredi kwa muda baada ya kusoma hoja yangu akala kona! Ipo siku tutafungua macho na kuona.
 
Habari haijakamilika. Tafuta Gazeti la Majira usome upate context ya hoja zangu vizuri. Sikuongelea uwajibikaji katika context ya serikali. Nilikuwa nawaasa vijana juu ya umuhimu wa kuwajibika kikamilifu kitaaluma na kitaalamu, kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na kasumba iliyoanza kujengeka nchini mwetu ya kutaka mafanikio kwa njia ya ujanjaujanja na njia za mkato. Nikasisitiza kwamba waweke kipaumbele kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kuipenda nchi yao. Hakuna short cut ya mafanikio zaidi ya kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii na upendo wa dhati kwa nchi.

Sasa watu wamezoea wakisikia uwajibikaji wanafikiria serikali-that was not my point mkuu.
Dr. Mkumbo,
Nafurahi kwa ufafanuzi. Very disguising habari hii nimeisikia toka redion asubuhi kwenye vichwa vya magazeti and all of a sudden nakuja kiuikuta hapa JF ikiwa vile vile kama ilivyosomwa kwenye vichwa vya magazeti asubuhi!
Tafabdali JF watu waandike yanayotamkwa na si yanayokuja kichwani mwao!
 
Mheshimiwa Dokta Kitila Mkumbo hisima yako,

Nikiwa Mtanzania mwenye uchungu na nchi hii sijafurahiwa na hatua iliyochukuliwa na wabunge wa chama chako mpaka sasa kuhusu kupunguza matumizi ya Serikali. Kama kawaida yetu kwa ajili ya ujuha tulionao mmefanikiwa "kututeka" na hoja ya posho. Lakini ukiangalia hizo posho wanazozizungumzia kina Zitto Bungeni ni pesa ndogo sana.

Je ni lini mtarudia ile dhamira ya Mhe Dr Slaa ya kupunguza mishahara ya wabunge? maana hapo ndio Serikali itafanya savings ya uhakika si tunafahamu kwa mujibu wa kiinua mgongo kwa wabunge kinatolewa kwa mujibu wa sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa namba 3 ya mwaka 1999 ambayo ilianza kutumika 2000 na kisha kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 katika kipengere cha sheria namba 12.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, iliyotokana na marekebisho ya sheria ya awali ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986, sio wabunge wote watakaovuna kiasi hicho cha fedha, kwa kuwa muda wao wa kuwa bungeni unatofautiana.

Mfano tukichukulia idadi tuseme Bunge la Jamhuri ya Muuungano lina wabunge 327, kati yao 49 ni mawaziri na manaibu waziri. Ukiondoa mawaziri na manaibu wao ambao kinua mgongo chao hulipwa na serikali, hivyo watakaolipwa na Bunge ni 278. Kwa mantiki hiyo, jumla ya Sh12,724,704,000 zitalipwa kama kiinua mgongo kwa wabunge hao ukiondoa mawaziri.

Fedha hizo ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miaka yote mitano ya utumishi bungeni ambapo kwa mujibu wa marekebisho ya mishahara ya viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa yaliyofanywa Julai mwaka 2009.

Ukilinganisha na kazi wanayoifanya wabunge hawastahiki kupokea kiwango kikubwa kama hiki huu ni unyonyaji na wizi wa mchana kweupe kuliko wizi wa posho ambazo mnazipigia kelel ili kuwin popularity. Tujaribu kuwa wazalendo kidogo tufanye ya ukweli.

Asante sana mheshimiwa na ni matumaini yangu kina Zitto wataibua hoja ya mishahara ya wabunge ili kupunguza viinua mgongo vyao.

Songela sana/

Mkuu sokomoko hapo ndipo kwenye hoja. Yaani umeiweka vizuri sana tena sana. Kuongelea posho ya vikao tu na kufumbia macho marupurupu mengine ni kujaribu tu kutudanganya. Tuangalie mishahara, posho zingine zaidi ya za vikao, tuangalie mikopo ya wabunge, tuangalie posho za mafuta, posho za viburudisho, rsponsibility allowance ya wenyeviti, nk. Huyu kuibuka akakataa posho hii na huyu posho nyingine tunakosa standard. Mimi kuna nimesema hapa kwamba Mbowe - KUB anakataa gari lakini anakubali posho ya viburudisho; Zitto anakataa posho ya vikao lakini anakubali responsibility allowance ya uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma: Je Ambaye si KUB na si Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge mfano Mr. II atachagua kukataa posho gani?
 
Habari haijakamilika. Tafuta Gazeti la Majira usome upate context ya hoja zangu vizuri. Sikuongelea uwajibikaji katika context ya serikali. Nilikuwa nawaasa vijana juu ya umuhimu wa kuwajibika kikamilifu kitaaluma na kitaalamu, kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na kasumba iliyoanza kujengeka nchini mwetu ya kutaka mafanikio kwa njia ya ujanjaujanja na njia za mkato. Nikasisitiza kwamba waweke kipaumbele kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kuipenda nchi yao. Hakuna short cut ya mafanikio zaidi ya kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii na upendo wa dhati kwa nchi.

Sasa watu wamezoea wakisikia uwajibikaji wanafikiria serikali-that was not my point mkuu.

Kwa hiyo Dr. hujaongelea suala la posho au?
 
Posho zetu! Bunge letu! Tulizikuta na tutaendelea kuzitafuna! Kama hupendi tafuta bunge lako ambalo linakataza posho tuache wenzako tujimanulile.kafe mbele!!!
With due respects kama wote wanakuwa na uchambuzi km huu ndio mawazo ya wengi...basi kilaaniwe kizazi hiki kwani hakijui kitakacho, na wala kwao hakuna kesho wala jana! Laanatullah!
 
Mkuu sokomoko hapo ndipo kwenye hoja. Yaani umeiweka vizuri sana tena sana. Kuongelea posho ya vikao tu na kufumbia macho marupurupu mengine ni kujaribu tu kutudanganya. Tuangalie mishahara, posho zingine zaidi ya za vikao, tuangalie mikopo ya wabunge, tuangalie posho za mafuta, posho za viburudisho, rsponsibility allowance ya wenyeviti, nk. Huyu kuibuka akakataa posho hii na huyu posho nyingine tunakosa standard. Mimi kuna nimesema hapa kwamba Mbowe - KUB anakataa gari lakini anakubali posho ya viburudisho; Zitto anakataa posho ya vikao lakini anakubali responsibility allowance ya uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma: Je Ambaye si KUB na si Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge mfano Mr. II atachagua kukataa posho gani?
Mkuu Kimbunga,Tumekuwa vipofu na hoja nyepesi mie kwangu hizo posho sio deal naangalia mbunge gani mzalendo atakaeweza kuokoa 15 bil za kiinua mgongo na kuwa injected to projects such us powe pojects and hospitals sitaki kusikia posho ambazo hazifiki hata nusu bilioni kwa miaka mitano kwa wabunge wote. Mishahara ya wabunge ikipunguzwa kwa asilimia 30 mpaka 40 tutakuwa na uwezo wa kuokoa shs 12 bil mpaka 15 bil halafu hizo posho ziwe za mwisho kufutwa kwani kiwango chake sio kikubwa kihivyo! Wanasiasa wanawacheza shere wananchi kwa kuwa wanajua ni majuha na watawa support kama kusapoti upupu wa posho ni ujanja na uelewa mimi ngoja nibali mbumbumbu mzungu wa reli.
 
Mheshimiwa sokomoko hili suala lako ni jipya na muhimu sana labda ungeazisha thread yako ingekuwa na maana zaidi ili watu waijadili kwa mapana yake

ni kweli kabisa, anzisha tuanze mkuu, maana umekokotoa vizuri, kama unajua kila mmoja anapata sh ngap pamoja na viinua mgongo vya mawazir tujuze.
 
Mkuu Kimbunga,Tumekuwa vipofu na hoja nyepesi mie kwangu hizo posho sio deal naangalia mbunge gani mzalendo atakaeweza kuokoa 15 bil za kiinua mgongo na kuwa injected to projects such us powe pojects and hospitals sitaki kusikia posho ambazo hazifiki hata nusu bilioni kwa miaka mitano kwa wabunge wote. Mishahara ya wabunge ikipunguzwa kwa asilimia 30 mpaka 40 tutakuwa na uwezo wa kuokoa shs 12 bil mpaka 15 bil halafu hizo posho ziwe za mwisho kufutwa kwani kiwango chake sio kikubwa kihivyo! Wanasiasa wanawacheza shere wananchi kwa kuwa wanajua ni majuha na watawa support kama kusapoti upupu wa posho ni ujanja na uelewa mimi ngoja nibali mbumbumbu mzungu wa reli.

Tuko pamoja mkuu. Tusipotezwe na viposho tena wanaongelea kaposho kamoja wakati wanajifanya hawajui kuwa wanapora viinua mgongo! Mika mitano kiinua mgongo million 45; miaka 4o kwa mwalimu kiinua mgongo million 15! Inapokuja suala la mapato yao wote huwa pamoja!
 
Tena huyo mwalimu atasaga lapa mpaka atakufa hajapata kiinua mgongo chake, hili swala la kuweka matabaka ya watumishi wa umma ni la hatari sana. Natamani ningekuwa mbunge asie na chama pasingetosha pale mjengoni.

Ni ukweli usiopingika kuwa wabunge wengi wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi na ya watu wao wa karibu. Ndio maana huwezi kushangaa kumwona mtu na mkewe wote wabunge wakimaliza muda wao wanakuwa wanajumla ya mil 90 and above. Utakuta kuna family nzima bungeni utakuta mtu yupo yeye mkwe wake yeye mwenyewe mwanae yaani wanajua kule kuna ulaji ndio maana wanajazana kiukoo. Hizi hadidhi za kusema wanaenda kule kututumikia zimeziba masikio yetu na macho kwa pamoja na ukisema unazibwa mdomo kwa BAN. Utashangaa unatafutiwa sababu yaani imekuwa ni maisha ya kuviziana tu wanangoja uteleze wakulime. Mie nitasimamia ninachokiamini mpaka nakufa.

Wanasiasa si kina Zitto Mbowe wala Mwakyembe wapo pale kwa maslahi yao binafsi kuwatumikia wananchi ni wimbo wa kumzubaisha *****
 
Waziri mkuu Mizengo Kayanza Pinda amekiri kuwa serikali ipo katika mchakato wa kuziangalia upya posho hizo kama gazeti la Mwananchi linavyohabarisha hapa "CHADEMA imeibuka mshindi dhidi ya Serikali kuhusu suala la posho baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza bungeni kuwa Serikali imekubali pendekezo la kutafakari na kuziangalia upya posho mbalimbali wanazolipwa wabunge na watumishi wote umma.Ushindi huo wa Chadema katika hoja ya posho dhidi ya Serikali, umekuja baada ya malumbano yaliyozuka mwanzoni mwa mkutano wa nne wa Bunge la Kumi unaoendelea mjini Dodoma, huku ukiacha makovu ya kutupiana maneno na tuhuma miongoni mwa wabunge na mvutano na ofisi ya Bunge." Kwa habari kamili Chadema yaibwaga CCM kuhusu posho.
 
Mwandishi hakuwa sahihi kusema Chadema wameshinda bali wananchi wazalendo wameshinda. Wabunge wa CCM hawana uzalendo na weledi wa kufahamu wakati umebadilika. Nchi zilizoendelea zimepitisha miswada ya kupunguza gharama za matumizi ili kubana matumizi (austerity measures). Nchi zilizokuwa wakaidi kupunguza matumizi kama Greece zimefilisika na kufilisika kwao kumewapelekea kukubali kubana matumizi kwa kulazimishwa. Tanzania nayo haina budi kubana matumizi kwa wakati kama huu wa mtikisiko wa kiuchumi na kimaendeleo duniani.
 
And Chadema has how Many Member's of Parliament? Go Chadema...

ANd they say CCM is the party for People... Corruption and hypocrisy ought not to be inevitable products of democracy, as they undoubtedly are today...
 
CHADEMA imeibuka mshindi dhidi ya Serikali kuhusu suala la posho baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza bungeni kuwa Serikali imekubali pendekezo la kutafakari na kuziangalia upya posho mbalimbali wanazolipwa wabunge na watumishi wote umma.Ushindi huo wa Chadema katika hoja ya posho dhidi ya Serikali, umekuja baada ya malumbano yaliyozuka mwanzoni mwa mkutano wa nne wa Bunge la Kumi unaoendelea mjini Dodoma, huku ukiacha makovu ya kutupiana maneno na tuhuma miongoni mwa wabunge na mvutano na ofisi ya Bunge.

Ikiwa siku ya pili jana tangu Pinda kukubalika kwa pendekezo la kutafakari na kuangalia upya posho za watumishi wa Serikali na wabunge Ijumaa usiku, Naibu Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Zitto Kabwe, aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa ajenda yao inaonekana kushinda.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema lazima Chadema isimamie hilo hadi ushindi upatikane, kwa sababu nia yao ni kufika walipokusudia ambako ni kufutwa kwa posho hizo.

Juni 7, mwaka huu Zitto aliwasilisha barua ofisi ya bunge kukataa posho akisema watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida.

Zitto alisema posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao. Wabunge wanalipwa posho za vikao sh 70,000 kwa siku.

Alisema kitendo cha Waziri Mkuu kueleza kuwa watatafakari na kuangalia upya na kwamba suala la posho ni sera ya taifa na Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni ishara ya kiongozi huyo wa juu kukubali wazo la Chadema na safari ya kufuta posho hizo.

Awali, mara baada ya Chadema kutangaza msimamo huo, Spika Anna Makinda alipinga uamuzi wa kususia posho akisema suala hilo lipo kisheria na kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuamua kuliondoa.

Alisema Wabunge wa Chadema wataendelea kulipwa posho za vikao kupitia akaunti zao za benki na watatakiwa kusaini fomu ya mahudhuriao ya Bunge, vinginevyo watajiweka katika wakati mbaya.

Hata hivyo, akihitimisha hoja za wabunge katika hotuba yake ya makadirio ya matumizi ya ofisi yake na zilizo chini yake juzi, Pinda alisema suala la posho lipo kwenye mchakato wa kuzingatia upya na kutekeleza mpango wa maendeleo kwa kufuta posho za vikao (sitting allowance).

Waziri Mkuu ambaye awali alionekana kupigana na Chadema, alisema Katiba inakataza suala la posho zisizo za msingi na kwamba utaratibu huo umeandaliwa kwa kufuata utaratibu mzuri bila ya kuathiri mazingira na mfumo uliopo ndani ya Serikali kwa watumishi wake.

hata hivyo, Ziito alisema jana kuwa Pinda amejipinga mwenyewe kwa kukubaliana na hoja yao ya kupinga posho, hasa aliposema kwamba, Katiba inapinga masuala ya posho zisizo za msingi na kwamba.

Zitto alisema chama chake (Chadema) kitalisimamia kwa nguvu zao suala hilo hadi mafanikio yatakapopatikana.

“Mimi nimepokea majibu ya Waziri Mkuu kwamba utaratibu wa posho unafanyika ili kuziangalia upya na kutekeleza mpango wa maendeleo kwa kufuta posho za vikao, kwa hiyo nasema Waziri Mkuu amekubaliana na hoja yetu ya kufuta posho zisizo na msingi ili kuijenga Tanzania, lakini lazima mfahamu kuwa Waziri Mkuu amejipinga mwenyewe,’’ alisema Zitto.

Mbunge huyo alisema baada ya majibu ya Pinda, kazi iliyopo mbele yao kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mpango wa maendeleo unatekelezwa kwa nguvu zote kwa vitendo, bila ya kuweka nadharia na siasa ndani yake.

Zitto alisema Chadema itaendelea kushikilia msimamo wake wa kutosaini posho za vikao katika kipindi chote cha uhai wa Bunge ikiwa ni pamoja na kutokusaini fomu za vikao hivyo.

Alisema yeye kama Naibu Kiongozi wa Upinzani, aliamua kuwa mfano mwema wa kuigwa posho yake, alipoamua kuachia posho zake zote na kuapa kuwa hatazichukua kabisa.

“Mimi ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni, niliamua tangu Juni 8, mwaka huu kutokuchukua posho na napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa, sijachukua posho hizo na sitapokea hata nikipewa,’’ alisema na kuongeza:

“Tangu wakati huo sijasaini fomu za mahudhurio na mkakati wa wabunge wote wa Chadema ni kuhakikisha kuwa zinatengenezwa fomu nyingine kwa ajili ya wabunge wa Chadema ili kusaini pindi wanapohudhuria vikao hivyo,’’ alisema Zitto.

Mbunge huyo ndiye alikuwa wa kwanza kuibua hoja hiyo, kabla ya Mwenyekiti wa Chadema ambaye ndiye Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Freeman Mbowe, kuiwasilisha rasmi bungeni kama hoja ya chama.

Hata hivyo, taarifa zinaonyesha kuwa kabla ya hoja hiyo kuwasilishwa bungeni rasmi na Mbowe, mvutano mkubwa ulizuka miongoni mwa wabunge wa Chadema wakati wa kujadili hoja hiyo.

Inadaiwa kwamba baadhi ya wabunge wa Chadema walipinga hatua ya kususia poshondani ya vikao vya chama, huku Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda alipinga msimamo huo wa chama chake.

Shibuda wiki hii alikaririwa akisema hawezi kususia posho za vikoa kwa sababu uamuzi huo umechukuliwa kwa kuzingatia misingi ya ubinafsi.

Alisema kuwa wanaongoza hoja ya kukataa posho ndani ya chama hicho inaonekana hawana majukumu mengi katika majimbo yao.

Bajeti ya posho kwa walimu
Uamuzi huo wa Chadema, umekuja huku taarifa za utafiti wa taasisi ya Policy Forum inayojihusisha na tafiti mbalimbali za sera zikionyesha kuwa, katika mwaka 2008/2009, Serikali katika bajeti yake ilitenga Sh506 bilioni kwa ajili ya malipo ya posho.

Kwa mujibu wa utafiti huo, ambao taarifa yake ilitolewa mwaka uliopita, fedha hizo ni sawa na mishahara ya mwaka mzima kwa walimu 109,000 ambao ni robo tatu ya walimu wote nchini.Kwa mujibu wa utafiti huo mwaka 2009/10 kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya posho za watumishi wa umma kilikuwa sawa na asilimia 59 ya malipo ya wafanyakazi wa ngazi ya chini.

Katika hatua nyingine, juzi Mbowe, aliitaka Serikali ndani ya mwaka mmoja kutengeneza sera ya kubana matumizi.Mbowe alisema hayo alipokuwa akiuliza swali Bunge lilipoketi kama kamati kwa ajili ya kupitisha bajeti hiyo.Baada ya kupewa nafasi ya kuomba ufafanuzi, Mbowe alisema ni vyema Serikali ikatoa muda maalum ambapo itatoa sera ya kubana matumizi ya Serikali.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, alisema serikali haiwezi kueleza muda maalum wa kufanya hivyo, badala yake muda uliotolewa katika Mpango wa Maendeleo wa Serikali wa Miaka mitano, utatumika pia kutengeneza sera hiyo.

Baada ya jibu hilo Mbowe alisimama tena na kusema ni vyema suala hilo likafanyanyika ndani ya mwaka mmoja, au katika bajeti ijayo kwa vile miaka mitano ni mingi kulingana na unyeti wa suala hilo.
 
Mwandishi hakuwa sahihi kusema Chadema wameshinda bali wananchi wazalendo wameshinda. Wabunge wa CCM hawana uzalendo na weledi wa kufahamu wakati umebadilika. Nchi zilizoendelea zimepitisha miswada ya kupunguza gharama za matumizi ili kubana matumizi (austerity measures). Nchi zilizokuwa wakaidi kupunguza matumizi kama Greece zimefilisika na kufilisika kwao kumewapelekea kukubali kubana matumizi kwa kulazimishwa. Tanzania nayo haina budi kubana matumizi kwa wakati kama huu wa mtikisiko wa kiuchumi na kimaendeleo duniani.
Japokuwa mimi siyo mnazi wa chama chochote lakini CDM walionyesha uzalendo juu ya suala hili la posho. CCM bila la shinikizo hili wasingelegea, PM mwenyewe alitetea lakini baadae akaona kuwa maji yamefika shingoni ndiyo anajitia kufungua mlango wa majadiliano.
 
Mkuu ,

Mie sina chama chochote, ila hili suala lilianza tangu bunge lililopita Dr Slaa alipokuwa akilikataa bungeni. Ila kuna wanaharakati mbali mbali walikuwa wakilisemea hilo. Credits zote ukiwapelekea Chadema unawavunja moyo wale wanaharakati waliokuwa wakilikemea hilo jambo katika matamasha na semina mbali mbali. Serikali ilikuwa haisikilizi tu ila sasa maji yako shingoni ndio wameamua kusikiliza.
 
Back
Top Bottom