Kila anayetoa hoja anatafuta umarufu. Haijibiwi hoja linatolewa hitimisho. Hitimisho la kumkatisha tamaa mtoa hoja. Lengo la viongozi wanasingizia kila anayetoa hoja kinyume na wao ni kufanya watu wasiifikirie hoja hiyo bali waone haja ya kutoa hoja ni umarufu tu. Ndiyo kusema viongozi hawa ni maadui wa umarufu. Hawautaki umarufu waupate watu wa upande tofauti nawao isipokuwa wa upande wao tu. Ni uchoyo na uroho wa UMARUFU unawatawala.
Lakini mtu anapataje umarufu pasipokuwa na jambo tofauti na wengine? Katika michezo (mpira) mchezaji maarufu ni yule anayecheza vizuri kuliko wachezaji wengine wote, katika vita ( Mayunga) ni hodari kuliko wapiganaji wengine katika uwanja wa mapambano. Katika siasa kwenye mashindano ya hoja, mwanasiasa maarufu ni yule mwenye hoja inayokubalika kwa wananchi waliowengi.
Dawa yake sio kusema Mayunga usiwe hodari vitani usije ukapata umaarufu, ni wewe pia kuwa mpambanaji hodari kumzidi Mayunga ndipo utatambulika. Halikadhalika katika siasa dawa sio kumkataza Mnyika kutoa hoja yake ili asijeakawa maarufu bali ni kutoa pia hoja inayoizidi ya Mnyika. Kumzima Mnyika sio jambo rahisi kama anavyofikiri Jenista Mhagama kwa sababu hoja hizo hutoka kichwani mwake, ndivyo anavyoyaona mambo na kufikiri tena kwa haraka.
Ukitaka kumzuia kuwa maarufu mzuie asifikiri vile anavyofikiri au utoe hoja yenye nguvu kuliko yake. Mashindano ya hoja ni hoja pia. Hoja ndiyo kitu pekee kitakacho mpa mwanasiasa umaarufu au kitamzuia kuwa maarufu. Spika hana uwezo wa kumzuia mtu kuwa maarufu ijapokuwa Spika anaweza kupata umaarufu kwa kuwa kiongozi mbaya kuliko wote waliopata bahati ya kuliongoza Bunge la Tanzania kwa kuzia hoja nzito zilizopata kutolewa wabunge makini kama Mnyika.
Lakini Bunge laweza kufaidika kwa kutumia hoja za watu makini kwa sababu kunena sio kutenda. Mbunge akinena serikali ikatekeleza, serikali ndiyo itasika zaidi na kujipatia umaarufu. ACTION SPEAKS LOUDER THAN WORDS. Waweza kupoka umaarufu mtoa maneno kwa kutenda yale aliyoyasema na watu wakasema '' Aaa bwana huyu maneno tupu lakini huyu mtu wa vitendo zaidi'' Serikali waacheni wapinzani wawe maarufu wa kusema lakini ninyi muwe maarufu wa matendo.
Umaarufu hugawanyika kila mtu kwa jambo lake.