hao wasioenda kazini au maofisini unafikiri huwa wanazubaa ndani kuangalia bunge?kwa taarifa asilimia 80 ya nyumba mda huu ziko empty,au wapo mahousgal au wamama wa nyumbani na wako busy wanafanya usafi,kupiga deki kuosha vyombo,kufua,kuenda sokoni,kuandaa mlo wa mchana etc.
Wanaongaliaga TV mida kama hii hawazidi 5000 nchi nzima.
mkumbusheni kuwa kipindi cha jioni huanza saa 11 jioni hadi saa moja hao wa maofisini huwa wameshatoka, halafu wametuambia huu mfumo wa digital tv tutaona kupitia simu zetu kwa hiyo tutaaccess bunge waache uoga, wanatuthibitishia kuwa ni kweli mbunge 1 wa cdm ni 10 wa ccmHii ni kuthibitisha kwamba uamuzi wa kutaka bunge lisionyeshwe live umefanywa na ccm na katibu wa bunge ndugu Kashilila ameutangazia umma maamuzi ya ccm kwa mgongo wa ofisi ya bunge.
Nape Nnauye anachekesha sana tena huyu bwana mdogo ni wa kuhurumiwa. Yani hajui kwamba kuna watu wengi sana wanafuatilia bunge? ni ukweli kwamba wananchi wengi wanafuatilia bunge na ndio maana wamekuwa mstari wa mbele kukosoa mwenendo mbaya wa uendeshaji wa vikao vya bunge hasa kwa vitendo vya spika na naibu wake kusigina kanuni kukipendelea chama chao.
Nape akipata wasaa, asome tena hiyo nukuu aliyotoa kwenye gazeti la Nipashe. Inamvunjia heshma - yeye Nape- na pengine ni vema , in the future, akavuta pumzi na kutulia kabla ya kuongea na waandishi wa habari.
Kuonesha ni jinsi gani Nape amelikoroga, anasema: 'anaunga mkono jambo lolote linalota heshma kwa bunge'. Lakini anaendelea kwa kusema kuwa bunge linarushwa 'live' wakati wa asubuhi, na wakati huo (kwa maoni ya Nape) watu wako makazini, hivyo hawana muda wa kufuatili'
Kwa maneno mepesi sana, Nape anataka watu waazima na akili zao waamini kuwa kuonesha vikao vya bunge live- asubuhi kunalivunjia heshma bunge! Hii ni hadithi ya ajabu kabisa toka kwa Nape, na ndio maana nashauri asome tena nukuu yake ili aepushe chama chake na taifa kwa jumla na haya masimulizi ya kuanga-unga.
Heshma ya bunge haina uhusiano wowote na kurushwa live asubuhi, mchan, jioni au usiku wa manane. Kama bunge linaendeshwa kihuni kihuni, bila kufutata kanuni na taratibu zilizowekwa, usitegemee heshma. Kwa bahati nzuri tunayo mifano halisi. Bunge la Tanzania lilipata hesham kubwa wakati wa Spika Sitta. Na hii ni kwa sababu ya uelewa wake na kuheshimu utawala wa sheria lakini pia kuelewa kuwa bunge ni mhimili huru na wa muhimu kwa uhai wa taifa. Sitta aliongoza bunge kwa HAKI.
Makinda, kwa sababu anazozijua yeye, licha ya kuwa Naibu Spika wakati wa Sitta, amerudisha nyuma hatua zote tulizofikia, kama taifa kwenye suala zima la utawala wa sheria. Bunge haliwezi kuwa na heshma kama anayeongoza haelewi 'equation' ya heshma ya bunge inajumuisha nini? Bunge haliwezi kuwa na heshma kama mkalia kiti cha Spika anavuruga kanuni, taratibu,tamaduni/desturi zilizowekwa kuongoza bunge? Ukisshavuruga kanuni maana yake unaruhusu 'chaos'. Na dawa yake si kutoonesha vikao vya bunge 'live'. Hivyo, hoja ya Nape ni ya kipuuzi na haiwezi kutatua tatizo la msingi linaloharibu bunge.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.
Suala la Bunge kurushwa live halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi? alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.
Source:Nipashe Ijumaa
Naam, swadakta maumivu ya kichwa huanza pole pole na huko ndio tunakoelekea.Dalili za mwisho wa Uhai wa ma CCM. Bado kidogo tu wapige marufuku vikao vya bunge kwa singizio hakuna pesa za kuendesha shughuli za bunge
Oh noo.....poor you
Asubuhi ni muda wa kazi. Ukienda ofisini halafu usihudumiwe kisa mfanyakazi yupo busy kwa kuangalia bunge utajisikiaje?
Bunge lisionyeshwe live, wawe wanaonyesha marudio yake yote saa tano na nusu usiku.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

ni hatari sana kufikiri kwa kutumia tumbo
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.
Suala la Bunge kurushwa live halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi? alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.
Source:Nipashe Ijumaa
hao wasioenda kazini au maofisini unafikiri huwa wanazubaa ndani kuangalia bunge?kwa taarifa asilimia 80 ya nyumba mda huu ziko empty,au wapo mahousgal au wamama wa nyumbani na wako busy wanafanya usafi,kupiga deki kuosha vyombo,kufua,kuenda sokoni,kuandaa mlo wa mchana etc.
Wanaongaliaga TV mida kama hii hawazidi 5000 nchi nzima.
POOR Nape..Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.