Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!
CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012
Mimi nadhani ndio lile dai la Naibu spika kuwa WABUNGE WENGI WANAINGIA BUNGENI WAKIWA WAMELEWA POMBE NA SIGARA KALI KALI.
This is too abnormal!
Kimbunga mimi sitaandamana kwanza, nitakwenda Mbeya wanipe mbinu za kupopoa viongozi, ushanfahamu!
Halafu nifanye sahihisho katika bandiko lako, hatukuwatuma bali sisi ndio tumewaajiri. Tukisema tumewatuma watasema wakirudi watatupa habari. Tumewaajiri na kama waajiri tunatatka kujua wanafanya kazi tuliowatuma?
Naunga Mkono hoja
Nashukuru kwa wazo lako. "UHURU WA MAONI"Nepi Naweye
Sijawahi kuandamana miaka ya hivi karibuni lakini yakiitishwa maandamano ya kupinga hii hoja mimi Kimbunga nitashika bango na kuwa mstari wa mbele. Hawa wabunge wetu wamepatwa na nini? Karne hii ya utandawazi, uwazi na uhuru wa kupata habari wao wanataka kutunyima kujua wanatuwakilishaje? Hivi wamesahau kwamba sisi ndio tumewatuma na tunatakiwa tujue wanatuwakulisha vipi? Wanataka kufanya siri?
Ama kweli madaraka kitu kibaya sana. Mtu akiitwa mheshimiwa basi anadhani anaweza kufanya analotaka? Mimi binafsi nataka tuendelee kupata habari za kibunge LIVE bila Chenga. Kama hawatimizi wajibu ipasavyo tuwaone wasitake kujificha.

Thanx mkuu, nimetafuta kitufe cha like cjakiona ila umemaliza mkuu wangu.Siwezi kuwashangaa, nilisikiliza mawazo yao wakati wanaharakati wanapinga mfuko wa jimbo na sikuamini. Ni kipindi kile nilipong'amua kuwa hawa wabunge ni miongoni mwa watanzania wanaodhani wapo juu ya sheria.
Utasikia michango yao bungeni wakiwa wanawashambulia watumishi wa serikali kwa kula rushwa na huku wakiwataja majina kwa mbwembwe lakini ilipofika wao kula rushwa hawataki kabisa majina yao kutajwa!
Baada ya hapo wataamuru vyombo vya habari kutoandika habari ambazo ni "negative" dhidi zao! Huu ni ulevi usio na mfano na kama jamii itachelewa basi taifa litazidi kuongeza idadi ya "untouchables"!