Bunge lageuzwa ukumbi wa ngonjera.

Bunge lageuzwa ukumbi wa ngonjera.

wenye shahada za ukweli bongo ni wachache sana wengi ni za kuangalizia, kuhonga au kuchakachua sasa hapo tukisema mtu msomi tunapaswa kupima uelewa wake na sio amefikia wapi kielimu....
 
ukiangalia uelewa wa mama Makinda unaweza kuutilia mashaka lakini kuna uafadhali mkubwa ukilinganisha na wasidizi wake akina Ndugai na sometimes Jenesta Mhagama.
Hawa wenyewe wapo tu kuitetea serikali hata mambo yasiyokuwa na mantiki, nadhani ndio Bwana Maendeleo (aka JK) amewasema jana kuwa ni wanachama wenye uelewa mdogo!

Wenzetu duniani huko wanatumia mabunge haya haya kusimamia mipango ya nchi zao ilik watua wao waweze kuishi maisha mazuri na hata kupata ziada ya kuja kutusaidia sisi kutuchimbia visima kwenye nchi iliyojaa mito. Wakati hawa wakuu wetu wanasimama kuhakikisha hata wale wenye mawazo ya kuanzia kujikwamua na huu umasikini na matatizo yetu hawapati hata sekunde ya kuelezea. Hii ni ajabu kabisa!!!
 
Mkuu @Hkingwangalla huwa nakuheshimu sana na kukubali sana kamanda japokuwa upo CCM lakin kwa hii ya leo umenifanya nizidi kuamini ule msemo unaosema kwamba HAKUNA MTU TIMAMU YEYOTE ALIYEPO CCM.
 
mimi nawambieni muislamu hata asome afike mwisho, kuna element za ujinga hataziacha ndio akina kigwangalah. Jaribuni muone na kufanya research mtakubalina namimi japo siwachukii kabisa.
hv mkuu huwezi kuchangia bila kuweka udini??
 
Kigwangala sio makosa yake ni makosa ya kamti kuu ya ccm kumpitisha kugombea ubunge wakati wana ccm wa nzega hawakumpitisha. anajivunia kiburi cha mama 1
 
Juzi alijisifia humu jf eti atampa lisu darasa.kumbe darasa lenyewe ni matusi.huyu jamaa nimewithdraw respect zote nilizokuwa nampa kama one of the wasomi.alafu mbona leo hawaonyeshi bunge.au kingamuzi changu kimeexp.
 
Kingwangala kasema yeye ni msomi mwenye masters ya uchumi na kwa sasa anafanya Phd sijui ya vitu gani vile, kwa hiyo hawa wapinani watulie dawa iingie.

aache ujinga kwani waliotufikisha hapa kwenye haya majanga si hao hao wanaojiita wasomi
Uongozi ni kipaji... ni wasomi gani ambao hawajui kwanini nchi yao maskini??
 
Hapo kwenye blue, Lissu alikuwa anawasilisha hoja gani hadi yamemkumba hayo na huyo KIGWA wa JF??



Mkuu Chakaza, hebu nipe hoja ya Lissu japo kwa muhtasari tu
Kifupi ni kuwa Lissu aliwaambia kuwa hoja kama hii ni ya kutongozea kura 2015 maana kama ni mifuko ya Elimu na mazagazaga mengine ipo ila hakuna utekelezaji wowote. Na suala la kuanzisha utoaji wa mikopo kibenki haliwezekani kutokana na umasikini wa vijana wa kitanzania kwa vile hawana mali za kuweka dhamana ili kukopa. Kuwa ni hoja ya kutongozea ni kwa vile wanataka kuwaaminisha vijana kuwa wanawajali sana wakati ni mpango usiotekelezeka kama hiyo mingine kisha wawape kura.
 
Last edited by a moderator:
Ukilikamua chungwa/embe ndio unapata juice yake halisi. Mtu anapokua kwenye hasira/ akikerwa ndio huwa anaonyesha hali yake halisi, hapo dr. kigwangala ameonyesha yeye ni mtu wa aina gani.

Alaf humu JF kuna mdau mmoja alijitokeza kumsifia huyu jamaa, eti sura 2 za kigwangala....
 
unaweza mtu ukawa na doctorate na ukashidwa kuvitumia,, hekima ndo swala la muhimu kwa viongozi wetu wa siasa, bila hekima lazima ngumi zipigwe na matusi yatukanwe
 
Kigwangala sio makosa yake ni makosa ya kamti kuu ya ccm kumpitisha kugombea ubunge wakati wana ccm wa nzega hawakumpitisha. anajivunia kiburi cha mama 1
Inaweza kuwa ni sababu nzuri na mujarabu, ikizingatiwa kuwa Saidi alishika nafasi ya tatu kwenye matokeo ya kura za maoni kwa nzega, mwaka 2010.
Bado siamini kuwa Ccm imekosa vijana werevu dizaini ya Filikunjombe, hadi imteue huyu kuwa mgombea!
 
matusi c ndo yamempa ulaji Mwigula Madilu Lameck Nchemba so huyo poyoyo naye anasubiri mbeleko,ndo.ccm yetu hiyo,ucje shangaa na yy akatangaza nia ya kuwania urais
 
Namwona waziri wa maji J Maghembe anapendekeza hoja Mnyika iondolewe..
 
shukrani ya punda siku zote mateke,lisu amevuna matusi hata baada msaada wa bule kwa kigwangala ama kweli dunia ina mambo
 
Mbunge wa nzega dr. Hamis kigwangala wakati akijibu na kuhitimisha hoja yake bungeni anashindwa kufanya hivyo bali anamshambulia tu Tundu lissu, kwa mimi namshangaa msomi daktari akishindwa kukontrol hasira zake na kuonmgea matusi bungeni! Nashangaa sana jamani hiki kitendo na naibu spika anaruhusu tu vitu kama hivi ndani ya bunge letu.

Huyu Dr. Vitumbua (Kigwangala) si ndiye aliyemtisha mwenzie wa CCM kwa bastola huyu katiak vile viuchaguzi vyao vya Chama Cha Mafisadi? Na huyuhuyu Ndugai na Mabumba ndiyo mabingwa wa kuwatoa wabunge nje wanapokaidi amri za kiti? Ajabu leo licha ya Mwanasheria wa Serikali kukerwa na Kigwangala lakini yaelekea naibu spkika kafurahia sana Tundu Lisu kukashifiwa. Adhabu yao yaja 2015 tusikubali kuingiza wabunge hawa wanaofikiri kwa kutumia makalio. Na lile la Mbatia sasa wako kuchakachua ile rasimu ya mitaala ili Jumatano wawarubuni wabunge kwa kuwasilisha mitaala feki. Tunajua wazi tangu 2005 nchi hii haina mitaala rasmi bali ina rasimu ya mitaala lakini Jumatano watawasilisha bungeni mitaala feki. AIBU HIYO SERIKALI INADANGANYA? Kweli Tanzania “Akili ndogo inatawala akili kubwa”. SHAME OF THIS GOVERNMENT.


Yaliyotokea Dodoma jana pia ni aibu kubwa kwa CCM endapo vurugu zile zingefanywa na CHADEMA lazima raia angekufa, lakini wabunge wa CCM wanashiriki kuwapiga wananchi na CCM na Polisi wao wanafurahia vurugu hizo kwa vile zinatekelezwa na CCM.
 
Tenda wema nenda zako Lissu usingoje shukurani kwa Lijani Kigwangala
 
Back
Top Bottom