Bunge lageuzwa ukumbi wa ngonjera.

Bunge lageuzwa ukumbi wa ngonjera.

ndo maana Bashe alitaka kumfyatua kwa risasi.kwanza kura za maoni ccm hakushinda wakati wa ubunge alikuwa wa tatu wakamuonga agombee.

Umesema ukweli hakika mjuaji unajua,Huyu mtu hata CCM hawamtaki anamtaka ni JK na mama S maana angekubalika na CCM angeshinda kura za maoni. Ila anajimaliza mwenyewe maana dhambi hiyo haitapita bure tusubiri 2015 majibu yatatoka. Bashe 2015 JK na mama S hawatakubania tena njia nyeupe hiyo wewe anza kupiga jaramba leo ndio kavamia chaka kabisa.
 
naibu spika ndungai,mwenyekiti jestina mhagama na mabumba usitegemee hicho unachokisema hiyo ndiyo kazi waliyopewa kufanya.

Kwa hiyo bi kiroboto ana uafadhari?
 
Wote tu wamezoea mipasho siyo ccm,cuf wala chadema ambao hawapigi ngonjera,wanawakera wananchi kwakweli... Maneno alosema kigwangwala yalikuwa nje ya kauli za kistaarabu,alipanik akapoteza busara.hoja yake ni nzuri sana ila lugha ake alotumia leo kwa bw lissu ni mbaya sana.hata hvyo lissu kudai hoja ni ya kutongozea kura sio jambo zuri mana km kila hoja nzuri inayoletwa bungen ni kutongozea kura basi wapinzani wanatongoza zaidi

Lissu ana maana ina lack substance! Mikopo ya chuo kikuu tu shida, uje ukopeshe watu bila dhamana?
 
Kigwangala hata angesoma hadi afike wapi uelewa wake utaendana tu na kufeli kwake STD 7. Mtu aliyeshindwa mitihani ya 300x 300 leo awe na hoja makini????
 
Kigwangala kachemka,badala ya kujibu hoja akafanya personal attack. Kweli Elimu si kipimo cha ustaarabu.
 
Hakika hii ya kutongozea kura, maana hata mikopo ya elimu ya juu walianza hivi hivi, watu wakakataa kuwa sio sahihi wao walisoma bure sisi tudaiwe, wakashawishi ikapita. Mwka mmoja tu baadaye, mara hela hazitoshi, wale wa masomo ya sayansi ndio watapata 100%, mara wengine 40% kimsingi issue imewashinda. sasa leo mnakuja na janga jingine la kuwafanya watanzania wakopeshwe kodi zao. hata hivyo sina hakika kama wale maskini ndio watakopa hizo pesa. maana walafi wa ccm watajipa mamlaka ya kukopa pesa yote muda mfupi tu baada ya kutolewa kibali cha kukopesha. na hio mamlaka ya kukopesha sijui itatoka wapi??? maana mamlaka hizi chini ya ccm ni mabingwa wa kuanzisha na kupotezea. Kumbuka CRDB ilianzishwa kwa malengo gani na sasa inafanya nini?? Community Rural development Bank-nani wa Rural anayeijua CRDB??
 
Kuwa mwanachama, mpenzi au shabiki wa ccm, kunakuhitaji uwe na akili kama maiti au kama ya kigwangala.h.
 

Sasa, Naibu Spika na Spika wake si wale wale tu Mjomba! Hao ni wa kuwekwa tu hapo, hamna kitu. Hii ndio Tanzania na hao ndio viongozi wetu. Halafu kuna mtu eti hajui, pamoja na rasilimali zote tulizonazo ni kwanini sisi bado ni Masikini! Angalia aina ya viongozi tulionao, Utapata jibu.

na wamekuja kuomba dhamana ya kuwaongoza mkawaruhusu sasa unadhani hapo mbovu zaidi ni nani?
 
Mbunge wa nzega dr. Hamis kigwangala wakati akijibu na kuhitimisha hoja yake bungeni anashindwa kufanya hivyo bali anamshambulia tu Tundu lissu, kwa mimi namshangaa msomi daktari akishindwa kukontrol hasira zake na kuonmgea matusi bungeni! Nashangaa sana jamani hiki kitendo na naibu spika anaruhusu tu vitu kama hivi ndani ya bunge letu.

Sibure jamani Dr kigwangala naye atakuwa anafikiri kwa kutumia masaburi kwi kwi kwi
 
Kwani hii ya kingwangala ilikuwa hoja. Bodi ya mikopo ipo, anataka ziwe mbili? Suala ni kuboresha tu. Huyu jamaa ni hovyooooo.
 
Achakua tomaso wee vip, mpaka werema leo kanifurahisa sana alikuwa abisha kufuta usemi kingangwala akahamliwa kufuta na hakafuta...
halafu na wewe kiswahili chako hatukusomi kabisa inamaana uso wambuzi na mhete hukuwaelewa darasani?
 
Wote tu wamezoea mipasho siyo ccm,cuf wala chadema ambao hawapigi ngonjera,wanawakera wananchi kwakweli... Maneno alosema kigwangwala yalikuwa nje ya kauli za kistaarabu,alipanik akapoteza busara.hoja yake ni nzuri sana ila lugha ake alotumia leo kwa bw lissu ni mbaya sana.hata hvyo lissu kudai hoja ni ya kutongozea kura sio jambo zuri mana km kila hoja nzuri inayoletwa bungen ni kutongozea kura basi wapinzani wanatongoza zaidi

Staki Shari
Hii hoja ina tofauti gani na mabilioni ya Kikwete aliyoyatoa/gawa baada ya kuingia madarakani Mara ya kwanza? Pengine tofauti yake ni kuwa hayo yalikuwa shukurani baada ya kuchaguliwa na hizi zitatolewa kabla ya kura!
 
hivi huyu kigwangala anafikiri level zake sawa na TL?he is insane.....
 
Wanatukana wanavyotaka si wanajua kaka yao Ndugai atawakingia kifua!!? Ccm ni janga la Taifa.
 
miaka ipi?
..ha ha ha Mkuu ni kile kipindi cha Ezekieli Maige a k a Mwenekiti bweni la chuwi .......hiii mkuu imenikumbusha mambo mengi sana...niendele kufunguka....??? kuna mdau kagusia Zeganzo kanikumbusha mambo ....mivukoss...
 
Back
Top Bottom