Bunge lageuzwa ukumbi wa ngonjera.

Bunge lageuzwa ukumbi wa ngonjera.

Mbunge wa nzega dr. Hamis kigwangala wakati akijibu na kuhitimisha hoja yake bungeni anashindwa kufanya hivyo bali anamshambulia tu Tundu lissu, kwa mimi namshangaa msomi daktari akishindwa kukontrol hasira zake na kuonmgea matusi bungeni! Nashangaa sana jamani hiki kitendo na naibu spika anaruhusu tu vitu kama hivi ndani ya bunge letu.
Aliivamia hoja bila kuijua, ndiyo maana anashindwa kuitetea. Nilimwandikia aniambie kwanini amekopi hoja yangu bila kuniconsult akajikausha. Sasa aitetee basi, kwanini anawarukia watu?
 
Ukiwaondoa akina Januari Makamba,Dr. Faustine Ndugulile na Esther Bulaya,sioni wanasiasa vijana wengine kutoka CCM ambao unaweza ukasema baadaye watakua viongozi bora! Ni matusi,ugomvi na mambo mengine ya kijinga jinga yamewatawala!
 
Lissu Kasema anaweka rekodi sawa kwenye hansard kwamba hajawahi kutibiwa ugonjwa wa aina yeyeote mahali popote na Dr H Kingwangwala ila yeye ndie aliyewatete na madaktari wenzake walipofukuzwa bure
baada ya hapo Dr Kingwangwala akawa emotional akaloose control akawa anropoka matusi ya kumdhalilisha Lissu kwamba leo amepania kudeal nae kwa sababu alisema hoja yake ni ya kutongozea eti hoja yake imeungwa na wabunge wengi wakiwemo wa chadema kasoro mtu mmoja anayejifanya anaju leo atulie atampatia dozi yake ,jamani mipasho kuliko hata ile ya mtaa wa mtwara kule ilala haha Kingwangwala angeona mood za mawaziri wake angetambua hawakufurahishwa cheko zilikuwa kule nyuma,nadhani sasa mawaziri wanaanza kujua kuwa bunge nalo ni kichocheo cha wananchi kuichukia CCM ndio maana TBC walikuwa wakizima akiongea LIssu,Mnyika duh
 
Ukiwaondoa akina Januari Makamba,Dr. Faustine Ndugulile na Esther Bulaya,sioni wanasiasa vijana wengine kutoka CCM ambao unaweza ukasema baadaye watakua viongozi bora! Ni matusi,ugomvi na mambo mengine ya kijinga jinga yamewatawala!

Umemsahau deo
 
Mkuu huko waelevu ni wachache sana!!! Wengi wanaropoka sasa kinachomkuta Mwigulu kiko njiani kwa huyu Dr. Vitumbua
 
ndo maana Bashe alitaka kumfyatua kwa risasi.kwanza kura za maoni ccm hakushinda wakati wa ubunge alikuwa wa tatu wakamuonga agombee.
 
NDIO MAANA NASEMAGA CCM WALISHAPOTEA NJIA, KWAKUZANI CDM NDIO ADUI WAO MKUBWA.
WANANCHI WALISHAWACHOKA CCM, WANAHITAJI MAENDELEO NA SIO SIASA ZA KIKE KUTUPIANA MIPASHO.sikuhizi mbunge wa ccm hawapimwi kwa uwezo wao kiutendaji, bali ccm wanaangalia ameijibu vipi mapigo ya wapinzani.
 
Wote tu wamezoea mipasho siyo ccm,cuf wala chadema ambao hawapigi ngonjera,wanawakera wananchi kwakweli... Maneno alosema kigwangwala yalikuwa nje ya kauli za kistaarabu,alipanik akapoteza busara.hoja yake ni nzuri sana ila lugha ake alotumia leo kwa bw lissu ni mbaya sana.hata hvyo lissu kudai hoja ni ya kutongozea kura sio jambo zuri mana km kila hoja nzuri inayoletwa bungen ni kutongozea kura basi wapinzani wanatongoza zaidi
 
Mr Vitumbua...... Mr vigwangala.

View attachment 81947

Hivi huyu Kigwangala si ndo huyo mara alikwepa ngumi kisa vitumbua, baadae wakaoneshana BINDUKI na yule raia wa somalia, afu siku alipopanda pikipiki alikuja kutusimulia humu, afu lile jina lake halisi nikumbusheni.. hawa jamaa waliopora majina wanasumbua sana, angalia Amim, Lameki madelu, leo huyu njegele naye....!!!!
 
kuna siku mayai viza yatarushwa bungeni wee subiri
 
Nilisha waambia na leo narudia, wasomi ndo wanaotumika kuliangamiza taifa hili. kigangwalaaa huyu ni mchumia tumbo, hana lolote, masters ya uchumi ni nini bana?, mbona hata Lameck Mkumbo a.k.a vuvuzela anayo.
Usiwasahau WANASIASA😱hwell:
 
kigwa mpuuzi sana,hakuna alilofanya nzega hlf anakaa kutukana bungeni......ndo maana ht bosi wake hamjali,wakati wa ziara ya bosi wao mkoani tabora,esp nzg...kigwa alimtaka aondoke na mkurugenzi matokeo yake mkurugenzi kahamishwa tu.
 
Huyo ndiyo SAID BAGAILE aka Hamis Kigwangallah

Mimi nafikiri hii ni laana ya KUIBA JINA la Mtu kama Mkumbo Madelu alivyoiba jina la marehemu Mwigulu Nchemba.
 
Kama tuliowaamini kutuwakilisha kwenye chombo muhimu wanafanya hivi, tutegemee maendeleo kweli?
 
Kigwangallah ni blockhead person. Simshangai kwa maneno wala vitendo vyake bali nawashangaa wana Nzega waliomchagua kuwa mbunge wao!
 
Kama Dr. K amesoma kupita kiasi, angepigana na Bashe? CCM ya JK ni sumu inayoua akili za vijana wasomi na kuwa kama wapiga debe
 
Back
Top Bottom