Bunge la Pakistan kupiga kura ya kutokuwa na imani Waziri Mkuu Imran Khan

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Bunge la Pakistan linatarajiwa kukutana Ijumaa kwa lengo la kushiriki zoezi la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Imran Khan, katika kile kinachotazamwa kuwa ni wakati mgumu kwake tangu aingie madarakani 2018.

Mapema mwezi huu muungano wa vyama vya upinzani nchini humo uliwasilisha hoja dhidi ya Khan, ikisema amepoteza idadi kubwa ya uungwaji mkono bungeni baada ya wabunge kadhaa kukihama chama chake.

Hali hiyo inatajwa kuongeza hatari ya mpasuko wa kisiasa kwa taifa hilo lenye kujihami kwa silaha za nyuklia la Kusini mwa Asia.

Kwa mujibu wa katiba, spika atapaswa kuitisha kikao cha bunge ndani ya siku 14, baada ya kupokea hoja hiyo, ambayo ingeangukia leo Jumatatu lakini taarifa ya ofisi ya spika imesema tarehe imesogezwa mbele kutokana na uwepo wa kongamano la mataifa ya Kiislamu, mjini Islamabad ambalo limepangwa kufanyika Machi 23.
 
Huyu mwongo wa karne sisi tutamuondoa lini?
 
Baada ya kukataa kusapoti eu dhidi ya russia wamembandika skendo, wazungu si watu wazuri,
Na hao wabunge wote ni vibaraka
 
Back
Top Bottom