Bunge kuwaka moto, Kambi Rasmi ya Upinzani Kufutwa?

anne makinda usituangushe wanawake tunaaminika na kuheshimika kwa kuwa waaminifu tenda haki kutulindia heshima wanawake wa tz
 
AKIZUNGUMZA NA ITV KATIBU WA BUNGE AMESEMA HAMNA HAJA YA HOJA YA KATIBA KWANI SERIKALI IMEANZA MCHAKATO WA KATIBA

NA KUHUSU DOWANS KASEMA SWALA HILO LIKO MAHAKAMANI NA BUNGE HALIWEZI KULIZUNGUMZIA

moto wa CCM umeanza
 
hatufiki popote ng'o adhabu ya kudhulumu umma ni kubwa. Tunisia na misri ni mifano hai michache, na hapa itatokea
 
Mie nilifikiri hizo Kamati na mambo ya kambi rasmi ya upinzani, yako kwenye katiba.

Kumbe ni mambo ambayo yaliwekwa tu na watu wachache na watu hao wachache wanaweza kuyatoa?

Kama yako kwenye katiba, inakuwaje wasiletwe kwanza bungeni ili tuwasikie wanaoyapigia debe?

Nnaona Egypt itahamia hapa Tanzania kwa siku kadhaa zijazo.
 
Hilo mbona lilikuwa wazi tulikuwa tunasubiri muda tu..... sasa bado ya mnyika na yenyewe kuzimwa
 
Aisee, inatia shaka sana kuona jinsi mambo yanavyokwenda. Historia itawahukumu mwaka 2015
 
Ndo Tanzania ya CCM hiyo na tutaendelea kuwa wendawazimu hivyo hivyo siku zote za maishe yetu
 
Its a game,kinachoumiza tu ni kuwa maamuzi ya namna hii yanamuumiza sana mtanzania wa kawaida na si yule anayeyafanya.....lets see!!
 
Tuliyategemea hayo. Maisha magumu kila kukicha. Wenye ufumbuzi wananyimwa nafasi za ktoa maoni.
 
Wana JF Dr. Kashilila ametangaza rasmi kutojadili hoja binafsi ya Kafulila kwa madai ipo mahakamani.

Source. Taarifa ya habari TBC

Kafulila usiofu, kesi ikiisha kama hakijaeleweka basi toka tena na Single yako ya Dowans!
 
..CCM wana wabunge wengi kushinda Chadema, hivyo msitegee kuwa Chadema wanaweza ku-influence maamuzi huko bungeni.

..mimi ningependelea Chadema waendeshe siasa vijijini,mitaani,na kwenye vyombo vya habari.

..hoja yoyote ile ambayo itazimwa kimizengwe bungeni, basi Chadema wailete nje kwa wananchi na kuwasomesha nini kilichoendelea.
 
Anne Makinda anataka kufa vibaya. Taarifa ya habari saa 2:00 usiku imesema kuwa hoja mbili kati ya saba hazitajadiliwa. Moja, hoja ya Mh.Mnyika kuhusu katiba eti kwamba rais atateua tume. Hoja ya Pili ni ya Kafulila. hili limeachwa kwa vigezo kuwa suala hilo lipo mahakamani.

Hivi Watanzania kumbe tunanyanyaswa hivi? Rais akiona mbunge anapeleka hoja bungeni yeye anawahi kwa usanii wa kusema ataunda tume.

Wabunge wetu njoni kwa wananchi tutawaunga mkono tuandamane. Wanaotakiwa kuachia madaraka ni kuanzia rais na spika. hatukubali usanii wa kucheza na maisha yetu.mambo ya tume hadi lini?
 
Hii nchi bana naona Makinda ameshaanza kutumikia mafisadi shame on u ccm:sad::sad::sad:
 
Nadhani wabunge wote wa CCM, CUF, CHADEMA, TLP nk wenye mapenzi mema na nchi hii, wataongelea DOWANS na KATIBA hata kama nani katataa. Wananchi wanataka hayo mambo mawili yaongelewe kwa kina na ni hayo tu ndo muhimu kwa sasa. Kama Spika atasema kuna kanuni, basi wao waseme, wananchi wako juu ya kanuni, na hakuna kanuni kubwa isiyoweza kutenguliwa kwa maslahi ya umma.

Kila mbunge akiinuka na kuongela DOWANS, KATIBA, hata kama ajenda iliyoletwa siyo hiyo, Spika wa Bunge ataruhusu tu. Akikataa bila hoja, yaani kwa nguvu, basi ashitakiwe kwa wanachi. Wabunge wote wa vyama vyote wenye mapenzi mema, WAKATAE KWA NGUVU ZAO ZOTE kuingizwa mjini.....

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki WADANGANYIKA.....
 
Back
Top Bottom