Bunge kuwaka moto, Kambi Rasmi ya Upinzani Kufutwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge kuwaka moto, Kambi Rasmi ya Upinzani Kufutwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Feb 7, 2011.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wandugu, mpaka muda huu kuanzia saa nane mchana leo tarehe 07/02/2011 Spika wa bunge kwa kutumia kanuni za Bunge ambazo zinampa mamlaka ya kuunda kamati ya kanuni za Bunge na hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 115 (3) imempa mamlaka ya kuteua kamati ya kanuni za Bunge na kanuni hiyo imetamka kuwa yeye ndio atakuwa mwenyekiti, yaani anateua kisha anaongoza !

  Kutokana na hilo leo ameteua kamati hiyo na mpaka sasa wapo kwenye kikao, lengo ni kuhakikisha kuwa wanafuta neno kambi rasmi ya upinzani Bungeni ---ili eti kuwe na kambi ya upinzani ili kila mmoja aweze kuunda kambi.

  Ubishi ni mkubwa sana kwani hata sheria iliyounda bunge inatambua uwepo wa kambi rasmi, ila wanaendeleza Ubabe.

  Upande mwingine anafanyia kazi barua ya CUF iliyoandikwa kwa spika decemba 13 ,2010 wakimtaka spika kufuta neno kambi rasmi.

  Lengo lingine ni kuhakikisha kuwa zile kamati za bunge za kusimamia matumizi ya fedha za umma wanapewa watu wao kama ifuatavyo:

  1. Mashirika ya umma (POC) - Hamad Rashid
  2. Fedha za serikali (PAC) John Cheyo.
  3. Serikali za Mitaa (LAC) -David Kafulila ... ila huyu bado hawajakubaliana naye kwani wamempa sharti ambalo anapaswa kulitimiza kwanza kuhusu hoja yake juu ya dowans.

  Hivyo kama mapendekezo yakienda kama ambavyo wanataka ni kuwa sasa bungeni kutakuwa ama na kambi mbili za upinzani ama kusiwepo na kambi ya upinzani kabisa.

  Nitawaletea taarifa zaidi pindi kikao kikimalizika, waliopo humo ni pamoja na Hamad Rashid, Anna Makinda, Job Ndugai, Tundu Lissu, Mustafa Akoonay, Freeman Mbowe, Andrew Chenge, George Simbachawene, Nimrod Mkono etc.

  Nitawajuza zaidi hapo baadaye, kwani bado kikao kinaendelea.

  Hii ndio kazi ya kwanza ya Anna Makinda akiwa spika, Je, inaashiria jambo gani?
  Bunge hili litaenda ama ni malumbano kila kukicha?
  Kwanini wanaihofia CHADEMA?
  Je, wanataka tuwe kama Zanzibar ambako waliondoa kambi rasmi ya upinzani kwenye baraza la wawakilishi?
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Ukifikiria sana performance ya mabunge yetu haya unaona tu wastage of time na kula fedha zetu, I mean wabunge woote tu. lakini utakuta kama tumerogwa vile masikio na macho yoote bungeni, watu wanasisimka, na kupiga kelele mwisho wa siku CCM wanafanya wanachotaka..ndio si wako wengi?? bunge is another addiction to Tanzanians zile addictions zakupenda wasemaji na ku-quote walichosema!! action ZERO!!

  asante mkuu!
   
 3. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Bado cuf wanaendelea kutudanganya kwamba wao ni wapinzani? Motivation ya Makinda kuhujumu Chadema ni kubwa ukizingatia uwezo wake mdogo wa kukabili upeo mkubwa wa wabunge wa Chadema.
   
 4. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  watabana wee,,,,ipo siku wataachia...
   
 5. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Siasa za tz bana yan hapo wanagombea izo kamati ili wapate ulaji,yan mpk sasa sijaona mwanasiasa yoyote aliye madarakani kwajili ya kutuondolea mattz yenu na kuleta maendeleo wote wazi na mafisadi tu,hao upinzani wanapiga kelele sbb hawapo ktk receving end ya izo pesa wakichukua nchi mambo yale yale tu
   
 6. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Asante kwa kutujuza, natumai kitaeleweka huko ndani. Endelea kutujuza tuko pamoja
   
 7. c

  cray Senior Member

  #7
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  I don't think if that can possible, can you analyze source please?
   
 8. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sijui nianze kudai kodi zote wanzonikata??? Mh! Inauma:twitch:
   
 9. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #9
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Anayelilia kukosa cheo ana uchu wa madaraka.
   
 10. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Hapa ndipo utaona watanzania wanavyo weka mbele maslahi yasiyokuwa ya taifa. BTW ngoja tuone.
   
 11. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hii ni hatari, Anna makinda kwa sasa ni kama kuku alokatwa kichwa. Anatumika na ccm kuharibu utulivu na asipojitambua atakuwa wa kwanza kufanya nchi izidi kumshinda JK, na bunge halitatawalika na ukombozi wa taifa ni dhahiri utaanzia ktk uovu na matendo yake ya kuburuzwa na ccm inayokufa, ikishirikiana na cuf wanasubiri kudra za ccm ili wasitawi kisiasa! Aibu yao!

  Makinda aangalie asiwe wa kwanza kuleta ghasia. Naamini kama kweli akina Mbowe na Lissu kama wapo, watapasua jipu kikao kikiisha na ukweli utaleta matokeo yasiyotabirika kama yatakuwa ya dhuluma kwa Cdm. Tusubirie ukweli.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Bunge hili ni usanii mtupu hakutakuwa na chochote cha maana zaidi ya usanii. Wanaostahili kuunda kambi ya upinzani ni CHADEMA lakini huyo mama wa chama cha mafisadi ameamua kutumia ufisadi ili kuwapora CHADEMA haki yao baada ya kupata viti vingi kuliko chama kingine chochote kile.
   
 13. i

  ibange JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  wakifanya hivyo tutaandamana hadi kieleweke kama tunisia na cuf watakosa sympathy ya umma kwa kujali maslahi binafsi zaidi
   
 14. Y

  Yabisi Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inaonyesha CCM hawataki changamoto na hakuna maendeleo bila changamoto,so let us get rid this stuck minds
   
 15. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 261
  Trophy Points: 180
  Makinda in action. Tutaona mengi awamu hii. Mwelekeo wake ni kwenye udikteta
   
 16. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Hapa ndipo utaona watanzania wanavyo weka mbele maslahi yasiyokuwa ya taifa. BTW ngoja tuone.
   
 17. c

  cray Senior Member

  #17
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 172
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wana JF Dr. Kashilila ametangaza rasmi kutojadili hoja binafsi ya Kafulila kwa madai ipo mahakamani.

  Source. Taarifa ya habari TBC
   
 18. c

  carefree JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  duh anne makinda linda heshima ya wanawake siku zote ni waaminifu usituharibie mama :clap2:
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Feb 7, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hoja binafsi kuhusu sakata la dowans kutojadiliwa bungeni kisa eti suala hilo lipo mahakamani linasubiri hukumu.
   
 20. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,003
  Trophy Points: 280
  JK na Genge lao wanadhani wanajenga kwa kuwaweka watu wao kila kona, lakini ni ukweli usiopingika kuwa hao walioweka ndio wamekuja kuua Chama rasmi
   
Loading...