Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,599
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali, Bunge letu jipya linalokwenda kuundwa hivi karibuni baada ya uchaguzi Mkuu, lina hali mbaya sana ya kuwa liko kwenye hati hati ya kutokuwepo kwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Swali ni Jee NEC, Rais Dr. Mwinyi na Rais Dr. Magufuli wataingia huruma na kuokoa jahazi kwa kuliokoa Bunge letu la JMT ili liweze kuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni?.

Declaration of Interest
Japo mimi ni kada wa chama cha siasa, na uchaguzi umekwisha, sasa narejea kwenye zile safu zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo zinatanguliza uzalendo kwa maslahi ya taifa letu Tanzania, hivyo nakuomba unisome with clear conscious kama mnamsoma Mtanzania mwingine yoyote, lakini kama tayari umeisha ni lebo mimi ni kada na kujiambia kila ninachoandika ni kwa maslahi ya chama changu na sio maslahi ya taifa, nakushauri uishie hapa, maana hata ukiendelea kunisoma with preconceived biased opinions, hautaweza kuiona rationale ya bandiko hili.

Na kwa vile hili ndilo bandiko langu la kwanza Jukwaa la Siasa baada ya Uchaguzi, naomba kuchukua fursa hii kumpongeza Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa ushindi wa kishindo, nakipongeza Chama changu CCM, na kupongeza wote walioshinda.

Japo ni lengo la kila mwana CCM, kuona chama chake kinashinda viti vyote na kata zote, ila pia kuna baadhi ya wana CCM, tunaojiita "CCM Contemporary" ambao ni makada wazalendo zaidi kwa nchi kuliko kwa chama, wamefurahishwa na ushindi wa kishindo wa CCM, ila pia ni wazalendo zaidi kwa nchi kuliko chama, tungependa kuona wapinzani makini wachache wakiingia Bungeni ili kuleta a balance of power na kujenga ile dhana ya Bunge la vyama vingi. Hivyo kushindwa kwa mtu kama Zitto ni masikitiko kwa wana CCM wazalendo wengi wa type yangu!. Tunapenda Bunge la CCM, lakini pia lenye mwamko na msisimko wa challenges za upinzani.

Hivyo kwenye kushangilia ushindi, nawasihi viongozi wetu na wana CCM wazalendo wenzangu, tushangilie kwa kiasi, tusiwatambie upinzani, tusiwakejeli, kuwatukana wala kuwabeza, kwasababu nao ni Watanzania wenzetu na wamechaguliwa na Watanzania, ila kura zao hazikutosha, hivyo kwenye hotuba zetu, tupunguze kujimwambafy na badala yake tuongeze humility na kuhutubia hotuba za upendo to heal the wounded ili kuliponya taifa na machungu ya kushindwa na kuliunganisha taifa tuwe na upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano kuijenga nchi yetu, badala ya ku add an insult to an injury.

Wapinzani
Asiyekubali kushindwa sio mshindani, uchaguzi umekwisha, aliyeshinda ameshinda na aliyeshindwa ameshindwa, iwe ni kwa haki na kihalali, au ni bao la mkono, mshindi ni mshindi na mshindwa ni mshindwa, tujikubali aliyeshindwa ameshindwa kwa haki na kihalali, kwa kutumia kanuni ya " the end justifies the means", tukubali matokeo, kazi sasa ibaki ni moja tuu, kuijenga nchi yetu kwa kutoa kila aina ya ushirikiano kwa washindi.

Vitabu vya dini zote vinafundisha Wananchi kutii mamlaka halali. Baada ya uchaguzi kumalizika na rais kupatikana na kuapishwa, kile kitendo cha kuapishwa ni kumhalalisha rasmi hivyo baada ya rais Magufuli kuapishwa, sasa yeye ni mamlaka halali, ndiye rais wa JMT, ni rais wa Watanzania wote, waliomchagua, wasio mchagua, hata ambao hawakupiga kura, rais Magufuli ndiye rais wa nchi, tutii mamlaka halali.

Baada ya kuapishwa na kuanza kazi, hakuna kitu kinachoitwa kususa, kutokubali matokeo au kutomtambua rais, huko ni kujifurahisha tuu, kwa sababu tayari rais yupo na ana exist, umtambue, usimtambue, yeye ndio rais wako na yupo kwa ajili yako. Unaweza usimpende, unaweza usimkubali, lakini huwezi kutomtambua!. Hivyo viongozi wa upinzani acheni hadaa za kuwahadaa wafuasi wenu kuwa hamumtambui rais. Rais ni mtu mwenye status of duality.

1. Rais Magufuli ni mtu, ni binadamu, unaweza usimpende, usimkubali na ukakataa kutambua ushindi wake, that is human, kama humpendi mtu, hakuna anayeweza kukulazimisha umpende au umkubali, hilo una uhuru nalo.

2. Rais Magufuli ni Taasisi ya urais, president institution, hii ni mamlaka, hakuna choice ya kuipenda, kuikubali au kuitambua, ipo kisheria hivyo ni lazima uiheshimu, na kuitii mamlaka hii, it's not a matter of choice, its an obligation, ni lazima kuitii mamlaka na usipotii, mamlaka inakushughulikia, ndio maana hata sheria, kutokujua jambo fulani ni kosa kisheria, is not an excuse sheria isi act on you, hivyo hakuna kitu kinachoitwa kutokumtambua rais.

Huo ulikuwa ni utangulizi tuu kuwekana sawa, mada ya leo ni hii.
Kufuatia poor performance ya vyama vya upinzani kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kwa Watanzania kuvikataa na badala yake kukichagua CCM pekee, but 4!, idadi hiyo haiwezi kutimiza akidi inayotakiwa kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Ibara ya 14 ya Kanuni za Bunge zinaeleza
2) Wabunge wote wa Upinzani wanaweza kuunda Kambi Rasmi ya Upinzani iwapo idadi yao itakuwa si chini ya asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge wote.
(3) Chama cha Upinzani hakitakuwa na haki ya kuchagua Kiongozi wa Upinzani Bungeni, isipokuwa tu kama kina idadi ya Wabunge wasiopungua asilimia kumi na mbili na nusu ya Wabunge wote.

Idadi ya Wabunge wote wa Bunge la JMT ni 357, hivyo asilimia 12.5% ni wabunge 44.

Kwa matokeo ya uchaguzi huu, hata baada ya allocation ya wabunge wa viti maalum, idadi hiyo haiwezi kufikiwa, hivyo Bunge lijalo, lina hati hati ya kutokuwa na kambi ya upinzani Bungeni, kambi hii ikikosekana, maana yake, hakutakuwa na serikali kivuli, hivyo bajeti za serikali tuu zitawasilishwa bila maoni ya kambi ya upinzani, jambo ambalo is not healthy kwa Bunge la vyama vingi.

Watu watatu pekee wenye uwezo wa kuokoa jahazi hili, ni
1. Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ikubali kutoa nafasi ya upendeleo kwa viti maalum vya upinzani hata kama hawakukidhi vingezo.
Mfano, maadam sifa ya kupata viti maalum ni chama kupata asilimia 10 ya kura zote, then Tume inaweza kuamua, wale wagombea urais wote waliopata kura zaidi ya asilimia 10%, wote waingie Bungeni.

2. Rais wa Zanzibar, anazo nafasi 10 za uteuzi wa wawakilishi, katika nafasi hizo zote 10, ateue wawakilishi 10 wa vyama vya upinzani, kati ya hao 10, wawakilishi 5, waingie kwenye GNU, na wawakilishi 5 waingie kwenye Bunge la JMT toka Baraza la Wawakilishi. This is a very big sacrifice to make.

3. Rais wa JMT, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na yeye ana nafasi zake za uteuzi wa wabunge 10. Usually lengo la uteuzi huu ni ili rais aweze kupata watu wa kutosha kumsaidia, kwa kuwa mawaziri, lakini kwa line up ya walioshinda CCM, kuna line up ya kushibisha mawaziri wote, na bado akabakiwa na reserve team inayoweza kuunda Baraza la Mawaziri la akiba.

Hivyo kama rais Magufuli akiingia huruma, akaamua kuliokoa Bunge letu tukufu, then na yeye ateue angalau wabunge 6 wa upinzani kuingia Bungeni kwenda kuimarisha upinzani, na rais Magufuli anaweza kuitumia kete hii kupiga ndege wawili kwa jiwe moja.
1. Kuuokoa Upinzani 2. To heal the nation from the election wounds ambazo to some ni very painful na kuna watu wako very bitter!.

Kwa ushauri wangu, napendekeza rais Magufuli awateue hawa wafuatao
1. Freeman Mbowe- M/Kiti chama kikuu cha upinzani
2. Tundu Lissu- aligombea nae
3. Zitto Kabwe - Most Interactive MP
4. James Mbatia- Very Compromising
5. Prof Haruna Lipumba - Good Puppeteer
6. JJ.MNYIKA- Mjengaji hoja mzuri
Nafasi tano zilizobaki ni za wanawake, tunamuomba Magufuli amuangazie yule Queen Sendiga miongoni mwa wanawake hao.

Hili likifanyika, litatibu makovu ya uchaguzi Mkuu huu, na kuingiza vichwa vya upinzani ambavyo vitalichangamsha Bunge letu na kuliongezea msisimko.

Hili lusipofanyika, Bunge la chama kimoja, bila any challenges, japo litaharakisha maendeleo bila upinzani, litakosa msisimko na lita bore!.

Kwa kumalizia, namalizia kwa lile swali la msingi, kuwa Bunge jipya lina hali mbaya liko kwenye hati hati ya kutokuwepo kambi rasmi ya upinzani Bungeni.

Swali ni Jee NEC, Rais Dr. Mwinyi na Rais Dr. Magufuli wataingia huruma kuliokoa Bunge letu la JMT ili liweze kuwa na kambi rasmi ya upinzani Bungeni?.

Jibu la swali hili, litapatikana ndani ya kipindi cha wiki moja kuanzia Jumatatu Ijayo.

Nawatakia Jumamosi Njema

Paskali
Rejea za Bunge la Chama Kimoja

1. Uchaguzi 2020 - Japo ni mchungu 'Kumesa' lakini ndio ukweli wenyewe; watakaorudi Bungeni ni 'wa kijani', kubali kataa. Mwenye masikio na asikie!

2. Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

3. The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja
 
In short unamaaana wateuliwe watu waende bungeni wakampinge aliyewateua

Uzalendo ni kuwataka wateuaji waunde taasisi huru za kitaifa zitakazoweka mazingira ya haki kwenye chaguzi na sio ujinga ujinga unaofanyika!!!

Na ukumbuke dhamira ya chama kilichopo sasa hiv ni bunge kuwa la kijani kwa asilimia 1000000
 
Mkuu kaa kimya tu, endelea kutukuza uchaguzi wenu wa mgumashi. Acha kutupunga sisi wapinzani kuhusu kuongezewa wabunge hatutaki kabisa. Hata huyo mmoja aliyepata hatumtaki.

Mna nini nyie CCM, mnalazimisha kuwe na wabunge wa upinzani kilazima? Tumesema hatutaki ,full stop.
 
Jiwe walilolitupa waashi hatimaye wamelifanya kuwa jiwe la pembeni. Mlitusema wapinzani kuwa kazi yetu ni kupinga kila kitu leo hii tumekuwa sehemu ya maslahi ya Tz, tumeamua tuwaachie nchi mwenyewe ili msipate pa kusingizia. Maeneo yana vyama na chama cha kutuletea maendeleo ni cha kijani na sio wapingaji wa maendeleo.
 
Mawazo mazuri sana, tena sana. But wao CCM waliona bora njia hii waliyotumia kuliko hiyo ambayo unawaza kaka yangu Paskali.

Wao wanataka upinzani ufe, na sio ufe tu but Tanzania mzima kusiwe na mtu mwenye mawazo mbadala.

Watu wote tuwe na wazo moja la mirad mikubwa, sisi inchi Tajiri, tunaonewa wivu na Wazungu, madaraja, flyover Yan watu wote tuwe na lugha moja.
 
mkuu kaa kimnya tu, endelea kutukuza uchaguzi wenu wa mgumashi,
acha kutupunga sisi wapinzani, kuusu kuongezewa wabunge hatutaki kabisa ,hata huyo mmoja aliyepata hatumtaki,

mna nini nyie ccm mnalazimisha kuwe na wabunge wa upinzani kilazima?
tumesema hatutaki ,full stop
Hivi Pascal Mayalla unaweza kuthubutu kuuita ule ulikuwa uchaguzi huru na haki?

Hivi uchaguzi gani watu wanaingia na mabegi kwenye vyumba vya kupigia kura, wakiwa na ballot papers zikiwa tayari zimetikiwa kwa wagombea wa CCM?

Hata hivyo naamini Mwenyekiti wako atakuwa amefurahi sana kwa kutimiza azma yake ya kuuua upinzani ifikapo mwaka huu Wa 2020..........

Kwa hiyo hakuna haja ya kufikiria tutaundaje kambi rasmi ya upinzani, ili mradi tu mmetimiza azma yenu.

Hivi unawezaje kufikiria kuwa Mheshimiwa Rais anaweza kwenye nafasi zake za uteuzi Wa wabunge 10 awateue wabunge Wa aina ya akina Zitto Kabwe, wakati yeye mwenyewe ndiyo alikuwa akiomba usiku na mchana kuwa wabunge Wa aina hiyo wasiweze kurejea tena kwenye Bunge hili?

Ninaamini kuwa Jiwe atakuwa amefurahi hadi jino la mwisho kwa kuua upinzani kwa kifo cha kikatili cha aina hii kwa kutegemea vyombo vyake vya dola vimfanyie kazi hiyo!
 
Mjumbe umejaribu kwa Kila namna kujificha nyuma ya huruma kwa wapinzani na uzalendo wa nchi, hakika nakwambia uandishi wako,ujengaji wako wa hoja unakuanika mahaba yako yaliopitiliza kwa ccm kwenye situation hii.

Kitu pekee ulicho fanikiwa kwenye pandiko hili ni kutumia lugha ya upole na staha, maneno ya huruma kuonyesha tambo za kisiasa na majivuno kwa hao unaowaita wapinzani....
 
Hatuhitaji huruma ya mtu, tunahitaji uchaguzi huru na wa haki na pia kuwa na mahakama huru yenye kuweza kuamua mshindi halali pasipo kupokea maagizo kutoka kwa mtu yoyote.

Alafu acheni unafiki.Mnachokitafuta sasa ni wapinzani wachache ili mridhishe wafadhili na ili mfute aibu ya ubakaji wa demokrasia mlioufanya.

Endeleeni na Bunge lenu.
 
Unaweza kuandika post kila wakati lakini umeshinda kutetea hoja yako ya kwanza uliyopata bahati ya kuingia Ikulu.

Tafakari hili tena

TRUMP kaomba msaada wa NEC ya Marekani - imegoma.

Kajaribu mahakama kuu - wakamwambia awe mpole.

Police wanawaangalia waandamanaji wa Trump na kuwapa ulinzi. Hadi ambulance zipo.

Guys, independent institutions are more important than democracy.

Lakini independenti institutions sehemu ya demokrase.

Tetea hoja zako acha hamu! Wanasema "hamu uondoa ufahamu"
 
Kama "mzee baba" ataka kuwa na Bunge la kumsaidia, nadhani atafute watu walipinga au kumsifu "praise team"
Atafute watu wa kum-stretch to think what his has not thought of na in the course of stretching him, atende zaidi.

Mtu kama Husein Bashe alikuwa na constructive critiques na hata toka kateuliwa na NW anatembea kwenye nini alitamani kuona kinanyika.

JPM is the doer; na kuna lots should be done kutengeneza uchumi jumuishi na sio ule wa "figures".

Tanzania has lots of potential people hasa nje ya circles za watawala ambao wanaweza kuifanya 2020-25 ikawa miaka ya neeema sana kwa TANZANIA na Watanzania.

Nchi itoke kwenye biashara za uchuuzi mpaka wa mifagio, moppers, chupina leso toka China tuwe kwenye jukumu la kuzalisha mid industries ambazo zitazalisha ndani na mauzo a ndani yafanywe na Watanzania kwa fedha kuibakiza humu ndani.

Waziri wa Elimu ajae hatakiwi kuwa mtu wa nadharia na kufurahia maksi nzuri za wanafunzi kwa ufaulu na kukariri notice/madesa.

Kila la kheri wateuliwa wapya 2020-25.
Prof. Kilangi kashakuwa wa kwanza kuvuka upande wa pili wa mto.
 
Back
Top Bottom