Brg Gen Mwakanjuki afariki dunia

RIP Brigadier General Mwakanjuki.

Lakini habari kwenye IPPMEDIA ya leo na sehemu zingine zinadai alikuwa mmoja wa Wakristo kama watatu hivi kwenye SMZ.
 
Duh,, mwaka huu Tanzania TUNAPATA darasa la Nguvu kutoka kwa MOLA. Yaani wakongwe wote wanaondoka, moja baada ya mwingine. R.I.P Mkuu. Poleni sana wafiwa.
 
Nawashukuruni wote kwa salamu za rambirambi, aidha kupitia hapa tutaendelea kuwa pamoja kwa taarifa zaidi juu ya msiba huu wa baba yangu mzazi.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Pole sana Best yangu Kibunango ... Mwenyezi Mungu akupe nguvu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu sana.

Sote njia yetu ni hiyo ... ametutangulia, ipo siku nasi tutamfuata.

RIP Brig. Gen. Mwakanjuki
 
Nawashukuruni wote kwa salamu za rambirambi, aidha kupitia hapa tutaendelea kuwa pamoja kwa taarifa zaidi juu ya msiba huu wa baba yangu mzazi.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Poleni sana Mkuu kwa Msiba huu mzito. Mungu awape Nguvu na Subira.
 
Nawashukuruni wote kwa salamu za rambirambi, aidha kupitia hapa tutaendelea kuwa pamoja kwa taarifa zaidi juu ya msiba huu wa baba yangu mzazi.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Pole sana ndugu yangu, inauma ila ndiyo dunia!
 
Pole Kibunango

RIP Mzee ret Brg Gen Mwakanjuki

update ya Habari za maziko ni aje?
 
Nawashukuruni wote kwa salamu za rambirambi, aidha kupitia hapa tutaendelea kuwa pamoja kwa taarifa zaidi juu ya msiba huu wa baba yangu mzazi.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
well, hutakiwi kuwa mitandaoni kama baba yako mzazi amefariki, nenda uka focus msibani!
 
well, hutakiwi kuwa mitandaoni kama baba yako mzazi amefariki, nenda uka focus msibani!

Mtu aliyezoea kula kwa mikono hata umpe vijiko vya dhahabu atanawa mikono tu. Wewe kwa vile lazima uende internet cafe kupost humu basi unajdhani kila mtu ni hivyo. Kwa maana nyingine unamwambia aache kutumia simu vile yuko msibani, huoni uwepo wake hapa ni muhimu sana kutujulisha yanayojiri msibani..................Pole sana Kibunango
 
Kwa maana nyingine unamwambia aache kutumia simu vile yuko msibani, huoni uwepo wake hapa ni muhimu sana kutujulisha yanayojiri msibani.................
kutujulisha kwenye mitandao ili iweje? wenye uchungu wa kwanza na msiba wa baba yake akili zao ziko msibani, anatakiwa awe nao kimwili na kiroho, badala ya kushinda anaranda randa mitandaoni.
 
Nawashukuruni wote kwa salamu za rambirambi, aidha kupitia hapa tutaendelea kuwa pamoja kwa taarifa zaidi juu ya msiba huu wa baba yangu mzazi.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.

Mkuu Kibunango, pole sana kwa msiba wa Baba!.

Niliproduce documentary yake huko Zanzibar akiwa Waziri wa Kilimo. Ilirushwa TVT na TVZ.

Kwa sasa ni jirani yanu, niko nyumba ya tatu kutoka kwenu, next to Kahatano na Deo Mtui.

Mchana huu nimetoka hapo na kuelezwa uamuzi wa maziko Zanzibar au bara` utatolewa jioni hii!

RIP Brig. Gen. Mwakanjuki!.
 
Pole sana bwana Kibunango kwa kuondokewa na mzazi. Ni pigo kubwa sana kwa sababu yeye ndiye anayewaunga ninyi nyote. RIP the Bingwa. I think that is your nick name for him.
 
RIP Brigadier General Mwakanjuki.

Lakini habari kwenye IPPMEDIA ya leo na sehemu zingine zinadai alikuwa mmoja wa Wakristo kama watatu hivi kwenye SMZ.

Hii habari ya mnavyotofautina dini yake , sidhani kama inahusu hapa, ama itatupa faida ya kimsingi kwenu na kwetu. Awe Muislam au Mkristu, Pagani haijalishi.
Au mmealikwa kwenye ibada ya mazishi yake ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…