Brg Gen Mwakanjuki afariki dunia

Mzizi wa Mbuyu

JF-Expert Member
May 15, 2009
7,309
6,739
Waziri wa zamani katkia SMZ Brg Gen Mstaafu amefariki dunia mchana wa leo ktk hosp ya jesh Lugalo!!
Nilikuwa hapo punde pata habari hizi, sijui alikuwa anasumbuliwa nanini mwanasiasa huyu mkongwe!
 
Majenerali wa Ukweli wanaishia hivyo......tunabaki na MASHIMBOSHIMBO

RIP Mjomba

p+046.jpg
 
Waziri wa zamani katkia SMZ Brg Gen Mstaafu amefariki dunia mchana wa leo ktk hosp ya jesh Lugalo!!
Nilikuwa hapo punde pata habari hizi, sijui alikuwa anasumbuliwa nanini mwanasiasa huyu mkongwe!

Namkumbuka sana huyu Adam Mwakanjuki, wakati akiwa waziri wa Serikali ya Mapinduzi huko visiwani, alitembelea kwetu kirafiki, wazazi walipokuwa nje kikazi, tulimwandalia chakula cha mchana tukifikiria ni mwenzetu kiimani kwa vile jina la Adam Mwakanjuki si la ustaadhi Maalim. Alipokaribishwa alikula aina ya vyakula vyote vilivyowekwa mbele yake ila hakugusa nyama. Naona alifikiri ni kiti moto kwa vile siku iliyotangulia tulimtembeza kwa majirani wanaofuga kiti moto na kwetu kwenye zizi la ndama wa Maziwa.

Kwa vyo vyote tunamkumbuka alikuwa mstaarabu na asiye na ubaguzi na kujenga uvumilivu wa hali ya juu kwa ajili ya umoja wa kitaifa.
RIP Adam Mkwakanjuki.
 
watu wazuri wanafariki wanabaki wabaya na wezi wa taifa. Natamani angekuwa waziri moyo wangu ungefurahi!. Ee Mungu kama hakuwa fisadi mpokee apumzike kwa amani.
 
Hoo!! Malafyale Mwakanjuki Jamani. Nakumbuka nilipokuja Tanzania mwezi Febr 2012 nilipata bahati ya kumtembelea kule kwake Mbezi beach.

Ni mtu makini sana na alikuwa mpenda watu na mwakilishi wa malafyale wote kule Znz.

Pole familia yake yote pamoja na akina "Save water Drink beer" na member wengine hapa barzani.

Mola ailaze pahala panapo stahikh. Adam Mwakanjuki.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom