Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Hiyo point ya mwisho muhimu sana...
a. Hakuna streamlization ya company information. TRA, NSSF, BRELA lazima ziwe na habari sawa kuhusu kampuni. Kabla ya kampuni kujiandikisha NSSF lazima ionekane ina kibali cha BRELA, na wakati huo huuo lazima iwe na namba ya kodi. Kampuni isianze kazi hadi iwe na kibali cha "compliance"
Idara ya BRELA inahitaji kupanguliwa haraka; Baada ya kufuatilia habari za kampuni ya Kinorwei kufanya kazi nchini bila kibali, sakata la Richmond, mambo ya Benki Kuu na makampuni hewa, suala la Kiwira na mambo mengi ambayo yanahusiana na uandikishwaji na utendaji wa makampuni nchini.
Idara hii inahitaji mabadiliko ya haraka na ya lazima kwani tusipoangalia tutakuja kuandikishiwa makampuni hewa!!!.. or we already have?
Mtanzania.. tatizo kubwa ni sheria na si watu; sheria zinapotungwa kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kutokuwajibika basi watu wasipowajibika ni kwa sababu sheria zinawaruhusu kutokuwajibika.
Kama sheria haisemi kuwa cheti cha usajili lazima kioneshe mmiliki na contacts zake watu wakiandika hivyo vyeti wakikosa habari za mmiliki tunaweza kuwalaumu? Kama sheria inasema Usalama wa Taifa hawatakiwa kuenforce usalama je wasipoenforce usalama tunaweza kuwalaumu?
Kama sheria inapokuwa kimya kuhusu Rais au waziri kufanya biashara akiwa ofisini na katika eneo analohusika nalo je akifanya hivyo anakosea?
Naamini BRELA matatizo yake ni zaidi ya watu bali pia sheria na muundo mzima. Ni nani anawasimamia Brela?
Mwanakijiji,
Umewahi ku deal na BRELA? Labda wenye experience na hapo mahali waseme. Kwa maoni yangu BRELA inahitaji documents nyingi mno kusajili.
Ndio maana nimeshangaa ilikuwaje Norconsult wakaendesha biashara bila kuwa na usajili wa BRELA?
Nenda bank kufungua account ya company, moja ya documents ni pamoja na registration ya BRELA, na documents nyingine kibao. Sasa hata kwenye bank Norconsult wakapeta tu, hapo kweli utasema tatizo ni sheria?
Kuhusu Mkapa, sheria zilizopo zinatosha kabisa kumfikisha Mkapa mahakamani kama will ya viongozi wetu itakuwepo.
Tatizo la TZ sheria zina sura, zinaangalia nani mtenda kosa. Kwa sheria hizo hizo ingetakiwa polisi wawe na mamlaka ya mwisho na sio kusubiri JK anasema nini.
Ndio maana mimi siamini kabisa kwamba tatizo ni sheria, sheria zilizopo zinatosha hasa, sanasana ni marekebisho ya hapa na pale. Watanzania ndio tunatakiwa kubadilika na kuanza kuuza maadili ya kazi kwa pesa.
..............ningependa kuhoji inakuwaje NSSF wanasawapa watu uanachama,mathalani wa Norconsult wakati kampuni haijasajiliwa?waliingia nao Mkataba vipi??
BRELA inapaswa kuwa mamlaka inayojitegemea kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo sasa ili iweze kufanya akzi zake kwa ufanisi. Isiwe chini ya mamlaka ya Waziri moja kwa moja.
Nchi nyingine usajili wa kampuni hufanywa na vyombo gani? Mliopo nje ya Tanzania mtusaidie tupate mifano ya nchi nyingine. Sio manispaa kweli? Ujerumani, Chambers of Commerce ndio husajili makampuni.
Kwetu inabidi tuwe makini zaidi. Lets study nchi nyingine
Zitto