Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 873
- 4,065
Unaweza kujenga Imani Kwa wageni kuja kuwekeza nchini Kwa wingi; wageni wakafika Kwa wingi na kutumia fursa Ila usinufaike na kuwepo Kwa wageni hao.
Juhudi za Mhe. Rais zinaweza zisizaie matunda Kwa Sababu aliowaamini kwamba wanaweza kukusanya na kuhifadhi mapato yatokanayo na uwekezaji wa Kigeni pamoja na utalii hawapo serious kuifanya kazi Yao.
Naomba niwakumbushe taasisi zifuatazo umuhimu wa kumuunga Rais Mkono tuweze kulipa madeni tunayodaiwa na kuendesha Serikali.
1. IDARA INAYOSIMAMIA AJIRA KWA WAGENI; Wapo wageni wengi Sana katika makampuni na taasisi mbalimbali wanaofanya KAZI Bila vibali.. waajiri wanatambua gharama za vibali na mchango wake Kwa uchumi wa nchi yetu. Lakini pia hakuna mwajiri anayependa kulipa fedha ya serikali Bila kusukumwa. Idara ya KAZI ikiweka sheria Kali na faini kubwa Kwa wageni wanaoishi na kufanya KAZI Bila vibali hakutakuwepo usumbufu wala udanganyifu WA kukwepa mapato ya serikali.
2. UHAMIAJI; Mnaporuhusu wageni kuingia nchini jitahidini kufuatilia wanafanya nini nchini. Mnapoboresha huduma mipakani mkaacha ufuatiliaji wa ndani ya nchi mnafanya vijana wa Kitanzania kukosa ajira na wageni kupewa ajira bila kuwa na sifa.
Maviwanda yaliyopo mkoa wa Mwanza sekta ya uvuvi, viwanda vilivyopo mkuranga na eneo lote la Pwani ikiwemo Dar es salaam, mahoteli na Mashamba yalipo Arusha kuna vibarua wengi wasio Watanzania na hakuna anayelipa Kodi, anayelipa vibali.
Watu wanaofanya kazi na wachina wanaweza kueleza namna ambavyo hawa ndugu zetu wanaweza kutumia kitambulisho kimoja hata watu Kumi Bila kukamatwa. Chukieni hatua makampuni haya Yanamchezea Mhe. Rais.
3. Mifuko ya Jamii: Hawa watu wamekaa ofisini wakisubiri waajiri wapeleke Makato ya wafanyakazi. Nani kawaambia makampuni ya Kigeni yanaweza Acha kazi zao wawapelekee idadi ya waajiriwa. Kodi kubwa inapotea katika eneo hili.
4. Taasisi za fedha; trend inaonyesha mabenki yetu yameshindwa kabisa kutoa huduma za kimataifa. Hapa pameibuka ufunguaji na utumiaji WA mabenki ya nje kufanya biashara za kimataifa. Natambua BOT wapo macho Ila nataka niseme kwenye eneo hili la udhibiti wa fedha kupitia Benki za Kigeni mamlaka zimeshindwa kabisa. Fedha nyingi zinapita kwenye haya mabenki.
5. Economic Intelligence Unit- Sijui kama tuna watu wanaofanya jukumu hili hapa nchini. Kwa mambo yanavyokwenda NI kama tumewekeza Sana kwenye intelijensia ya jinai na siasa kuliko uchumi. Naamini BOT kama Wana unit kama hii basi wanapaswa kuipanua ifanye kazi yakunusa fursa na kuzitangaza wakati huo ifanye jukumu la kuona mianya na kuiziba bila kuleta taharuki ya kamatakamata.
6. TRA - punguzeni au ikiwezekana ondoeni kabisa ujeshi na upolisi kwenye kukusanya Kodi. Mkiwa rafiki wa wananchi mkaweka na bonasi Kwa yeyote atakayefichua ukwepaji Kodi ntaona kazi yenu itakavyokua nyepesi.
Badilikeni. Tengeni muda wenu kukaa na jamii