BRELA Ipanguliwe

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,710
40,777
Idara ya BRELA inahitaji kupanguliwa haraka; Baada ya kufuatilia habari za kampuni ya Kinorwei kufanya kazi nchini bila kibali, sakata la Richmond, mambo ya Benki Kuu na makampuni hewa, suala la Kiwira na mambo mengi ambayo yanahusiana na uandikishwaji na utendaji wa makampuni nchini.

Idara hii inahitaji mabadiliko ya haraka na ya lazima kwani tusipoangalia tutakuja kuandikishiwa makampuni hewa!!!.. or we already have?
 
Yes Mwanakiji,

Nakuunga Mkono kwa hili,Ipanguliwe na kuwe na uwazi,na kwa kuanzai ningependa mambo haya yatiliwe mkazo.

1.Information zote zinazozihusu Kampuni zote nchini ziwekwe katika Tovuti ambayo wao watakuwa wameianzisha,ila kila mwanachi awe na uwezo wa kujua kampuni flani ni ya nani na ilianza mwaka gani,na shughuli zake ni zipi.

2.Kuwe na Bodi ya wadhamini ambyo itaundwa na pande mbili ,yaani serikali pamoja na vyama vya upinzani,Lengo ni kuhakiki Kampuni zote zinazosajiliwa toka Nje ni za kina nani na uwezo wao wa kufanya kazi ambazo zitakuwa zimeaanishwa katika usajili wa hizo kampuni.

3.kila mwezi wawe wanatoa ni kampuni ngapi zimesajiliwa na kama hizo kampuni zinalipa kodi,sbabu kuna vi kampuni hewa ambavuyo hata Kodi hazilipi.hii itasaida kwa TRA kufuatilia kwa ukaribu suala hilo.

Baada ya kusema hayo,ningependa kuhoji inakuwaje NSSF wanasawapa watu uanachama,mathalani wa Norconsult wakati kampuni haijasajiliwa?waliingia nao Mkataba vipi??
 
Hiyo point ya mwisho muhimu sana...

a. Hakuna streamlization ya company information. TRA, NSSF, BRELA lazima ziwe na habari sawa kuhusu kampuni. Kabla ya kampuni kujiandikisha NSSF lazima ionekane ina kibali cha BRELA, na wakati huo huuo lazima iwe na namba ya kodi. Kampuni isianze kazi hadi iwe na kibali cha "compliance"
 
Napata picha nzuri sana kuhusu BRELA majuzi tuu rafiki yangu alienda kusajili kampuni yake...jamanii...usisikie urasimu na ukiritimba...uliopo pale..wamemuibia jina la kampuni yake ....hawako wazi na jinsi ya kujua kama jina limeshatumika au halijatumika...ni waongo sana sana...ameenda na jina la kwanza wamesema limetumika...akapeleka jina la pili...wakasema limetumika...watu walio karibu naoo wakamtonya kuwa asipotoa kitu kidogo(rushwa...)hatapata usajili kamwe...ikabidii abonyee mfukoni..amepata jina lile la kwanza...inasikitisha sana sana sana.......uwekwe utaratibu ambao utakuwa huru kujua na ku search kama jina bado lipo au limetumika vingionevyo...mwanya mwingine wa rushwaaaaa
 
Gembe imetulia hiyo angalau kuwe na uwazi katika uendeshaji wa shughuli zao "BRELA" kamekuwa kama kakichaka ka kujificha wahalifu...It's real shame kwa taasisi kama BRELA kwenda kienyeji kiasi hicho. au ndio funika kombe mwanaharamu apite watu wapige bao??
 
Hiyo point ya mwisho muhimu sana...

a. Hakuna streamlization ya company information. TRA, NSSF, BRELA lazima ziwe na habari sawa kuhusu kampuni. Kabla ya kampuni kujiandikisha NSSF lazima ionekane ina kibali cha BRELA, na wakati huo huuo lazima iwe na namba ya kodi. Kampuni isianze kazi hadi iwe na kibali cha "compliance"

Hata bank zinahitaji information kuweza kufungua accounts na mambo mengine.

Swali kubwa hapa ni nani huwa anayalinda makampuni kama haya wanaweza kwenda kila mahali bila kuulizwa hivyo vivuli vya kuandikishwa??
 
BowBow.. point nzuri, kampuni isifungue akaunti ya biashara kama haina usajiri; isifungue akaunti ya fedha za kigeni kama haina usajili n.k hivi hadi wazungu watufikirie ndipo tutaona haja ya kutenda?
 
Tatizo sio kuwa hayo makampuni hayana "vyeti" vya usajiri kutoka BRELA! Wakati wa kufungua akaunti, au kuomba tenda hivyo "vyeti" vyote vya BRELA vinakuwepo (na hata Benki ikitaka proof kutoka BRELA huambiwa kweli hii kampuni tumeisajiri), lakini ghafla baada ya kufanikiwa either kufungua hiyo akaunti ama kupata tenda, faili lao kule BRELA linachomwa moto!!

Kwanza hiyo Certificate ya usajiri inamapungufu, haionyesha nani ni mmiliki wa hiyo kampuni zaidi ya kuwa kampuni imesajiri tarehe ... kwa ajili ya shughuli .... full stop.

Certificate kama hii waki-submit Benki au kwenye tenda, bado haisaidii kujua nani mmiliki wa kampuni! So zoezi zima la usajiri BRELA linatakiwa kuwa reviewed!
 
Idara ya BRELA inahitaji kupanguliwa haraka; Baada ya kufuatilia habari za kampuni ya Kinorwei kufanya kazi nchini bila kibali, sakata la Richmond, mambo ya Benki Kuu na makampuni hewa, suala la Kiwira na mambo mengi ambayo yanahusiana na uandikishwaji na utendaji wa makampuni nchini.

Idara hii inahitaji mabadiliko ya haraka na ya lazima kwani tusipoangalia tutakuja kuandikishiwa makampuni hewa!!!.. or we already have?

Mwanakijiji,

Ninaweza kuwa wrong lakini mimi nafikiri tatizo pale ni watu na wala sio muundo wa BRELA au sheria.

Kikawaida haya mashirika mengi yanapoundwa huwa wana copy sheria na muundo wa UK na kufanya mabadiliko machache. Huenda hizo sheria zinatosha kabisa
kama kutakuwa na will ya wahusika kutimiza wajibu.

Tatizo la TZ ni watu na wala sio sheria.
 
BRELA needs to automate their business process and create a comprehensive ERP and Management Information system for tracking all key info from registration turnaround time, actual file location, all registration input data etc to holding all data regarding the process taken.

Those seen not to be meeting the perfomance standards (that should be set!!!) should either be retrained or let go. Duplications will aso be a thing of the past as the system can be configured to resrict registration if the name already exists. The turnaround time will shrink from weeks to 24 hours. Many other benefits will naturally originate from this.

It is also only when an extensive BRELA database system is created in which all registration info is stored, updated and extracted from that we can then talk of a transparent and idependent (possibly online) comapany search application to determine whether a comapany exists.

Problem is of course migrating from the current system is not a small task. Just cleaning up the mess and confusion created by incompetency, corruption and pure neglect and disregard from the current physical file and storage approach system is going to take the best part of several years.

Other than that corruption, and the fact that there are people who want things to continue as they are with no accountability are some of the other factors why brela has not technologically advance from a physical file based system to a comprehensive ERP, DBMS, MIS system approach.
 
Mtanzania.. tatizo kubwa ni sheria na si watu; sheria zinapotungwa kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya kutokuwajibika basi watu wasipowajibika ni kwa sababu sheria zinawaruhusu kutokuwajibika.

Kama sheria haisemi kuwa cheti cha usajili lazima kioneshe mmiliki na contacts zake watu wakiandika hivyo vyeti wakikosa habari za mmiliki tunaweza kuwalaumu? Kama sheria inasema Usalama wa Taifa hawatakiwa kuenforce usalama je wasipoenforce usalama tunaweza kuwalaumu?

Kama sheria inapokuwa kimya kuhusu Rais au waziri kufanya biashara akiwa ofisini na katika eneo analohusika nalo je akifanya hivyo anakosea?

Naamini BRELA matatizo yake ni zaidi ya watu bali pia sheria na muundo mzima. Ni nani anawasimamia Brela?
 
Umewahi ku deal na BRELA? Labda wenye experience na hapo mahali waseme. Kwa maoni yangu BRELA inahitaji documents nyingi mno kusajili.

Ndio maana nimeshangaa ilikuwaje Norconsult wakaendesha biashara bila kuwa na usajili wa BRELA?

Nenda bank kufungua account ya company, moja ya documents ni pamoja na registration ya BRELA, na documents nyingine kibao. Sasa hata kwenye bank Norconsult wakapeta tu, hapo kweli utasema tatizo ni sheria?

Kuhusu Mkapa, sheria zilizopo zinatosha kabisa kumfikisha Mkapa mahakamani kama will ya viongozi wetu itakuwepo.

Tatizo la TZ sheria zina sura, zinaangalia nani mtenda kosa. Kwa sheria hizo hizo ingetakiwa polisi wawe na mamlaka ya mwisho na sio kusubiri JK anasema nini.

Ndio maana mimi siamini kabisa kwamba tatizo ni sheria, sheria zilizopo zinatosha hasa, sanasana ni marekebisho ya hapa na pale. Watanzania ndio tunatakiwa kubadilika na kuanza kuuza maadili ya kazi kwa pesa.
 
Mimi nimefanyanao kazi mara nyingi tu,
1,ukisha sajili kampuni majina ya wamiliki huwa yapo katika fomu ya maombi ambayo muhusika hupewa na na brela.
-hivyo fomu wahusika hujaza anwani zao za nyumbani pamoja na eneo la biashara.
-pia lazima upeleke udhibitisho wa eneo la biashara
eg,risiti ya malipo ya kodi ambayo itakuwa na jina la mmoja wa wakurugenzi.
- au kitu chochote kinacho tambulika kisheria ambacho kinamilikiwa na mmoja wa wakurugenzi aw wote kwa pamoja.
2,pia wamiliki wa kampuni huwa wameorodheshwa kwenye m/a

sasa matatizo ya brela,
-baada ya watu kujisajili pale brela wanatakiwa kisheria kupeleka return kila mwaka pale brela waliowengi huwa awapeleki kabisa na kwakuwa brela hawapo komputerized sijui sasa sio rahisi kujua ni makampuni gani bado yanafanya biashara au yamekufa.
-kuhusu kupotea kwa mafaili hicho ni kitu ambacho watu hukifanya kwa matakwa yao binafsi ni kosa la kiofisi.
 
..............ningependa kuhoji inakuwaje NSSF wanasawapa watu uanachama,mathalani wa Norconsult wakati kampuni haijasajiliwa?waliingia nao Mkataba vipi??

...........very good point............na ndio maana nilisema hapo awali kwamba hili soo la Norconsult litaondoka na wengi....lets wait and see
 
Mimi nadhani systems zote (hasa za serikali) zimepooza zinahitaji tiba kubwa. Rushwa, uzembe, mazoea nk vimetawala taasisi nyeti zote. Kinachohitajika ni mabadiliko makubwa kwa kulazimishwa na wengine kujirekebisha. Ili watu wajiriekebishe inahitajika nguvu specifically kutoka kwa president na mawaziri.

I ask President Kikwete to show his terrible face to rescue our beloved land.
 
Mtanzania nakubaliana na wewe moja kwa moja na nikiri sijawahi kufanya kazi na BRELA, mara ya mwisho kusajili kijikampuni kangu ilikuwa kwenye mojawapo ya halmashauri za miji.
 
BRELA inapaswa kuwa mamlaka inayojitegemea kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyo sasa ili iweze kufanya akzi zake kwa ufanisi. Isiwe chini ya mamlaka ya Waziri moja kwa moja.

Nchi nyingine usajili wa kampuni hufanywa na vyombo gani? Mliopo nje ya Tanzania mtusaidie tupate mifano ya nchi nyingine. Sio manispaa kweli? Ujerumani, Chambers of Commerce ndio husajili makampuni.

Kwetu inabidi tuwe makini zaidi. Lets study nchi nyingine

Zitto
 
Nchi nyingi za scandinavia huwa wanasajili manispaa ila kwa wao wanacentralised system ya kupata details za anayetaka kufungua comapny. Mfano criminal records, medical records,jina la company kama linaexists, n.k.

Na hii system yao ya kufungua kwenye manispaa/wilaya ambapo company itaendesha shuguli zake ni nzuri maana inakuwa hata rahisi kufuatilia kama hiyo company inalipa kodi, wafanyakazi wanapatiwa social security, n.k. na kuondoa ukiritimba unaoweza kujitokeza kama hapa Brella kwetu
 
Back
Top Bottom