Breaking news Mtoto wa Babu Ambilikile amekufa!!

Breaking news Mtoto wa Babu Ambilikile amekufa!!

Nafikiria wale walioko kwenye foleni kule Semunge kijijini, tangia Alhamisi tar. 21 hadi May 2.
 
Sasa kama babu anafiwa inakuwaje sasa? duuuh! nafasi ya Mungu itabaki palepale banadamu tunahangaika tu lakini mwisho wake kila ulimi lazima ukiri.............
 
Tatizo ni nini? mtandao wa Airtel nasikia upo huko tujuzeni jamani ni haya magonjwa 5 ndio yamemwondoa au kapigwa kwa sababu ya hivyo vijisent?
RIP
 
Hakika kweli kila nafsi lazima ionje mauti! RIP son of Babu.
 
Kifo ni lazima kwa binadamu hakuna cha ajabu kifo cha mtoto wa babu, amekufa kama binadamu wengine walivyokufa tusicomment mambo ya ajabu na wala tusihusishe tiba ya babu na kifo cha mwanawe. RIP SON OF BABU.
 
Ninampa pole nyingi Babu kwa kifo cha mwanae. Mungu ampe moyo wa subira na awasamehe wote wanaomdhihaki.
 
Ngoja tumsikie babu atatuambia nini yeye si anaongea na mungu mara kwa mara!

RIP mtoto wa mchungaji.
 
Tutaongea kila lugha, lakini mwisho wa siku tutakubaliana kuwa Babu ni mtumishi tu wa Mungu, na hana uwezo huo wa kuzuia kifo, na hili limetukia ili kuwajulisha watu kuwa hakika Mungu hana upendeleo!
Tusiwe short sighted jamani, na tusiongee kwa kubeza, kifo ni kifo tu, ni kazima tutoe pole kwa babu na kumtakia marehemu alale pema peponi!
Na tusipokuwa makini, sisi ndio tutakaokufuru!
 
RIP Jackson kila mwenye pumzi na uwezo wa kwenda Loliondo nendeni mkaone maajabu na mkawe mashuhuda.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mtoto wa Mungu mwenyewe alikufa, atakua mtoto wa babu?
 
kila nafsi itaonja mauti....... tuache ujinga wa kuhumu kifo watu tusiowajua, hivi wanaokata roho kila sekunde duniani tukiwaumbia vifo kwa namna hii si tunajilaani kwa Mungu?
 
Back
Top Bottom