Breaking news Mtoto wa Babu Ambilikile amekufa!!

Bwana Mungu alitoa na Bwana ametwaa....Pumzika kwa amani mtoto wa Babu!AMEN
 
Mtoto wa Mungu mwenyewe alikufa, atakua mtoto wa babu?

Ndugu yangu,

Umelinganisha visivyolinganishwa. Mtoto wa Mungu alikufa kwa ukombozi wa wanadamu, na huo ndio uliokuwa utume wake na siku ya tatu alifufuka, kumbukumbu hii ni mpya kwa sababu nimesherehekea Pasaka juzi. Mtoto wa babu amekufa kama pure mwanadamu no relations with the son of God.
 
Mtoto wa Mungu mwenyewe alikufa, atakua mtoto wa babu?
Hapa unajaribu kulinganisha ardhi na mbingu! Daaa who's babu jaman mpk alinganishwe na Mungu kihivyo??? Babu sio mungu na hatakaa awe Mungu, huyo ni mchungaji mstaafu, hajamkaribia mungu kwa uwezo hata kidogo! RIP mtoto wa babu, babu alikupenda ila Mungu kakupenda zaidi.
 
Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani tumekua wavivu wa kufikiri.
Hivi kifo cha mtoto wa babu navingine tofauti yake ni nini?
Hivi babu anamamlaka ya kuzuia kifo?
Kwani Babu kasema ukishakunywa dawa yake hautakaa ufe?
Vipi babu nae ikitokea kafa imani yetu itasimama upande gani?
Tusiwe dhaifu kifikira.
Bwana alitoa Bwana ametwaa ''jina la bwana lihimidiwe.
R.I.P. CHALII WA SEMUNGE.
 
Amefarikia hospital babati-hii inanikumbusha nyerere aliwahi sema ktk birthday yake 75yrs,kwa kuwa yeye anakula na kuishi vizuri ana uhakika wa kuishi umri mrefu kuliko mama yake mzazi.kilichotokea haikupita miaka 2 nyerere akafariki!
 
Is it true? Maana watu hawakosi kebehi kwa babu, kama ni kweli basi R.I.P mtoto wa babu.
 
Amekufa kwa sababu ya malaria mkuu. Nadhani ilipanda kichwani maana magazeti yanasema kichwa kilikuwa kinamuuma na amekufa na walipompeleka hospitali Babati walimpronounce dead. Poor Babu busy treating others and his son dies. Pole babu. Haya ni majaribu ya mwovu ibilisi yakitaka kumrudisha nyuma babu. Lakini kazi ya Mungu lazima iendelee.
 
Hajatoa kafara wala nini. Mtoto amekufa kwa sababu ya malaria tu na tunajua malaria ni ugonjwa unaoongoza kuua kuliko ukimwi. Poor babu Mungu akutie nguvu usonge mbele na kazi aliyokuitia!!
naskia amemtoa kafara mwanawe ili biashara isidorore, tunangoja proof.
 
Ninawashukuru wote waliotoa pole zao kwa Mch. Ambilikile Masapila kufuatia kifo cha mwanaye mpendwa. Ningependa kuwaasa wanaotoa kebehi wasifanye hivyo kwani forum hii ni ya watu wenye busara na nionavyo forum itumike kwa busara ili kuwakilisha dhana nzima ya "the home of thinkers." Nawashukuru wote waliotoa mawazo yao kwa busara badala ya kubeza. Ieleweke kwamba Mch. Masapila hatibu kifo wala yeye hajawahi kudai kwamba hatakufa. Anajua ni mwanadamu na anajua kuwa hata yeye siku ikifika atakufa. Mbona watu wanaongea habari za kifo cha mtoto wa Mch. kwa dhihaka namna hii!? Huku ni kukosa utu na haiwafai watu ambao wao ndio chimbuko la hekima na wenye wajibu wa kuifundisha jamii. Please my friends remember this is Jamiiforums!
 
Babu Loliondo afiwa na mwanaye

Monday, 25 April 2011 23:55
Mussa Juma, Samunge
MCHUNGAJI Ambilikile Mwasapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu huko Samunge, Loliondo amefiwa na mtoto wake wa kiume jana. Kutokana na msiba huo, Serikali imesitisha tena tiba anayotoa hadi Ijumaa.

Habari zilizopatikana kijijini hapo jana zimeeleza kuwa mtoto huyo, Jackson Mwasapila (43), alifariki dunia jana asubuhi, nyumbani kwake wilayani Babati, Mkoa wa Manyara.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali aliliambia gazeti hili jana kuwa kutokana na msiba huo, Mchungaji Mwasapila atasitisha tiba kuanzia leo jioni.Mkuu huyo wa Wilaya alifika Samunge jana hiyo hiyo akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, kumpa pole mchungaji huyo.

"Tunapenda kutangaza rasmi kuwa huduma zitasitishwa hadi Ijumaa na tunaomba watu walio mbali wasije hadi Ijumaa," alisema Lali.Alisema Serikali itashiriki msiba huo na inajiandaa kutoa msaada wa kumpeleka Mchungaji Mwasapila, Babati kushiriki msiba huo.

Mchungaji azungumziakilichomsibu mwanaye
Akizungumza na gazeti hili kijijini hapo jana, Mchungaji Mwasapila alisema mtoto wake huyo alifariki jana saa 5:00 asubuhi katika Hospitali ya Wilaya ya Babati baada ya kuugua malaria ghafla.

"Taarifa ambazo nimezipata ni kuwa Jackson alikuwa anasumbuliwa na kichwa na baada ya kufikishwa hospitali, alifariki dunia," alisema Mchungaji Mwasapila.Mchungaji huyo, alisema Jackson ni mtoto wake wa tatu kati ya sita alionao.

Wagonjwa wampa pole
Baadhi ya wagonjwa waliokwenda Samunge jana kupata tiba, walitoa salamu za rambirambi kwa Mchungaji Mwasapila kutokana na msiba huo.Hata hivyo, wakati wagonjwa hao wakimpa pole, mchungaji huyo alikuwa akiendelea kuwapa dawa kama kawaida.

Mchungaji Mwasapila alisema ameamua kuendelea na kutoa tiba kwa wagonjwa hao ili kuwasaidia watu ambao tayari walikuwa wamefika Samunge na wengine watakaofika leo.

"Kesho (leo) jioni nitafunga na kuelekea Babati kwa ajili ya msiba wa mtoto wangu na kama alivyosema mkuu wa wilaya, tutaendelea na tiba Ijumaa," alisema Mchungaji Mwasapila.

Foleni yapungua Samunge
Katika hatua nyingine, msongamano wa magari yaliyoanza kwenda kijijini hapo baada ya Pasaka umeanza kupungua. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mengi ya magari hayo, yalikuwa yamebeba wagonjwa kutoka Kenya.

Serikali ilishafungua vizuizi vya Bunda, Mto wa Mbu, Londigo na Loliondo mjini vilivyokuwa vimefungwa kwa muda wakati wa sherehe za Pasaka.

Source: Gazeti la Mwananchi.
 
wajemeni si mlisema babu hakuwahi kuoa wala hana mke anaishi mwenyewe sasa huyu mtoto katokea wapi tena?
 
jaman kifo kifo tu yaani hapa kifo cha mwanae kufariki sio kwamba muhusishe na tiba ya babu kumbuken babu co mungu hlo wana jf mlitambue ni binadam kama sisi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom